Manula alituchomesha mechi na mtani tukala 5

Daah hizi Team bhana zikifungwa sababu nyingi kana kwamba hazitakiwi kufungwa ukiangalia gemu ya big team ikiwa nyuma mpaka Ref anachezesha mpira huku kapanic muda wowote anaweza kutoa Tuta au Red card kwa Team pinzani ili kuondoa lawama kwa Simba au Yanga...
 
Ni ukweli usiofichika kwamba MANULA anatuhujumu, kama mnataka tufike salama, huyuasisogee uwanjani kabisa.

Aidha Ahmed Ally inaonekana unatusaliti Dana shida ni ni? Unaweza ku stepdown kimyakimya na maisha yaendelee.
sio kweli
 
Aliwachomesha nini sasa

1) goal la kwanza musonda anafunga point blank header hii hakuna kipa anatoa

2) goal la pili maxi zengeli anapiga shuti Kali akiwa 1 to 1 na manula hapa kipa unamlaumu Nini

3) mtu mbaad anawapiga toba mabeki na kipa wao... Hapa manula hakuona kitu

4) goal la nne maxi anafanya tap in, yaani uache laumu mabeki kina tshabalala walikua wanamsindikiza mzize kama anaenda panda basi stend ya magufuli unamlaumu manula kweli?..

5) Kono la nyani hili lilipatikana kwa penalty sitaki hata kulitolea ufafanuzi

Manula Leo kachoma goli la kwanza mechi na prison, jamaa katanguliza mpira mkubwa sana Kipa Gani unatoka unasita unaanza kurudi nyuma?
 

Goli la pili kashomesha inonga makusudi kabisa. Pale kilimuangusha nini? Yaani huyu inonga hana tofauti sana na mwamnyeto kiuchezaji. Wachomeshaji sana
 
Goli la kwanza KIBU.
Goli la Pili Kennedy/Manula.
Mpira ni mchezo wa Makosa, mpira ni ajira yao sidhan kama yasemwayo kwa Manula ni kweli, ila kwa timu kubwa kama. SIMBA golikipa kurubuniwa mtu alipwe 30-50M ipo sana tu na Kaseja alishaweka wazi.

Kwahiyo sishangai Endapo kweli Manula yupo kwenye mkeka wa Muuza Magodoro.
 
Ni ukweli usiofichika kwamba MANULA anatuhujumu, kama mnataka tufike salama, huyuasisogee uwanjani kabisa.

Aidha Ahmed Ally inaonekana unatusaliti Dana shida ni ni? Unaweza ku stepdown kimyakimya na maisha yaendelee.
Mkasema majini, kuyategemea haya majini mbona yatawapumbaza akili badaka ya juhudi binafsi za mchezaji mmojammoja ,(individual skills)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…