NewDawnTz
JF-Expert Member
- Nov 15, 2010
- 1,667
- 362
:embarrassed:
Ninachofahamu ni kuwa Tanzania ni nchi inayoongozwa kwa mfumo wa Katiba. Kwa mantiki hii ni lazima kila kiongozi, iwe kwa kupenda au kwa kutokupenda awe anaifahamu katiba kabla ya kuridhia kukubali wajibu wake.
Hii ndiyo sababu hulazimika kula kiapo kwa kutumia katiba hii ikimaanisha ya kuwa tayari wanaifahamu katiba na wako tayari kuitekeleza katika utendaji wao wa kazi wa kila siku. Naamini hata ndugu yangu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (Director of Criminal Investigation - DCI) Bwana Robert Manumba alikula kiapo hiki wakati anakubali jukumu hili kubwa sana katika nchi yetu ya Tanzania.
Alichokiongea leo kwenye kipindi cha Siasa asubuhi Star TV kimenipa mshituko mkubwa wa uwezo wa Manumba katika kutekeleza majukumu yake.
Akitakiwa kujibu swali aliloulizwa na Baruan Muhuza kuwa Je kitendo cha Polisi kutumia nguvu nyingi zisizokuwa na sababu ni matokeo ya mapungufu ya katiba, DCI Manumba alianza kujibu kwa kujiamini na kusema ya kuwa "Japo kuwa mimi si mtaalam sana wa Mambo ya katiba....". Hii ni kauli dhaifu sana kutoka kwa mtu kama Manumba.
Alikuwa ana maanisha nini kusema sio mtaalam wa mambo ya katiba? Je alitaka umma wa Watanzania ujue ya kuwa hana Shahada au Masters ya Katiba? Je alitaka tujue ya kuwa haifahamu katiba? au alitaka kumaanisha nini??
Na mtu kama yeye kutoa kauli kama hiyo hapo Je Sio ishara ya kuwa wako wengi wa aina yake waliokula kiapo cha katiba lakini hawaijui na hivyo hawawezi simamia itekelezwe?
Kwa kauli hii nimemtoa Manumba na hata alipozungumzia kurekebisha jeshi la Polisi nilijiuliza zaidi, analirekebisha kivipi wakati katiba yenyewe "Hana Utaalam Nayo"? Au ni marekebisho ya kuendelea kuisigina na kutokuitekeleza katiba?
Hii inamaanisha wazi tu ya kuwa tusitegemee kuwa na jeshi lenye kulinda katiba (japo ina mapungufu lakini yako mengi ya msingi ya kutekelezwa na ya kawa na manufaa kwa jeshi letu) kwa kuwa wenye jukumu la kuliunda Jeshi hili la Polisi lifanye kazi yake kikatiba hawaijui katiba.
Manumba kwa upungufu wa kutokuwa na "utaalam" na katiba uliyoapa kuilinda, nakushauri uachie ngazi...la sivyo, Mheshimwa JK timua kazi huyu mteule wako maana amekuabisha kwa kukutania kula kiapo kwa katiba asiyo na "utaalam" nayo