DOKEZO Manyanyaso Dawasa Ubungo/Kimara

DOKEZO Manyanyaso Dawasa Ubungo/Kimara

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

manyanyasodawasa

New Member
Joined
Sep 7, 2022
Posts
1
Reaction score
1
Nawasalimu katika Jina la Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania,

Dawasa ni Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira mkoa wa Dar es salaam, ikiwa na mikoa ya kihuduma mbalimbali likiwamo tawi letu la Ubungo. Tawi hili ofisi zake zipo Kimara matangini.

Katika tawi letu kumekuwa na manyanyaso sana, wafanyakazi tunaingia ofisini saa MOJA asubuhi na kutoka saa NNE usiku kinyume cha utaratibu, kufanya kazi weekend bila malipo yoyote tunayolipwa kwa kufanya kazi nje ya muda wa kazi, likizo tunanyimwa, tunatishiwa kufukuzwa kazi.

Viongozi wetu wa tawi hawaambiliki, hawashauriki! hatuna pa kuhemea. Kupitia waraka huu tunaomba jicho la tatu litazame unyanyaswaji huu unaofanywa na Meneja wa tawi na wasaidizi wake ukomeshwe mara moja. Haki na ustawi wa wafanyakazi ipatikane.
 
Kwani nyie si ndio mamlaka namba moja nchini? na mkurugenzi mkuu wenu anazidi kupewa mavyeo kwa utendaji uliotukuka? sasa mbona mnalalamika tena? poleni lakini ndio tozonia hiyo
 
Kwa uzoefu wangu katika utumishi wa umma ni kwamba kuna baadhi ya viongozi kufanya ni fashion kufanya kazi hadi muda wa usiku au baada ya muda rasmi kupita.

Viongozi kama hawa wana tabia ya kuzurula zurula muda wa kazi wakijifanya wako busy kumbe wanafanya shughuli zao binafsi na kupenda visafari vya hovyo lakini vyenye posho. Hivyo huwa na tabia ya kupanga vikao kuanzia saa 9 jioni, yaani nusu saa kabla ya muda wa kazi kuisha. Pia wanapenda kutumia muda huo kuwapangia watumishi wengine kazi ambazo wangeweza kuwapa wakati wa muda wa kazi na zikafanyika kwa ufanisi zaidi.

Jambo hili halikubaliki hata kidogo kwa sababu ni mateso kwa watumishi wengine na wala halina tija kwani muda wote watumishi wanakuwa wamechoka.

Bahati mbaya viongozi wengi wa vyama vya wafanyakazi ni watu wanaojikomba sana kwa viongozi wa taasisi hivyo kamwe hawawezi kuisema hii kero.

Sasa huu ni ufisadi sawa na ufisadi mwingine! Nawashauri andikeni barua TAKUKURU kuelezea huu ufisadi unaofanywa baada ya muda wa kazi. TAKUKURU watawahoji na wahusika watatoa utetezi wao. Nafahamu hakuna atakayechukuliwa hatua lakini message itakuwa imewafikia wahusika na watachukua hatua ya kurekebisha jambo hili. Vinginevyo mtaendelea kuumia kwa ajili ya kulinda ajira zenu!

Msichoke kupeleka kwa njia za kificho malalamiko yenu sehemu mbali mbali ikiwemo hata kwa Waziri na katibu mkuu.
 
Usituchoshe... watu kibao wako kitaa wanatamani hiyo kazi unayoiona ina manyanyaso...kama vipi ipotezee ufanye mishe zingine
 
Hapo nikuomba mamlaka iongeze watendaji mafundi kwa sababu inaonekana waitaji huduma ni wengi ukichanganya na mivujo watendaji ni wachache hapo ni kumuonea tu Meneja hana jinsi lazima mfanye zaidi ya saa za kazi kukizi mahitaji ya wananchi..
 
Nawasalimu katika Jina la Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania,

Dawasa ni Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira mkoa wa Dar es salaam, ikiwa na mikoa ya kihuduma mbalimbali likiwamo tawi letu la Ubungo. Tawi hili ofisi zake zipo Kimara matangini.

Katika tawi letu kumekuwa na manyanyaso sana, wafanyakazi tunaingia ofisini saa MOJA asubuhi na kutoka saa NNE usiku kinyume cha utaratibu, kufanya kazi weekend bila malipo yoyote tunayolipwa kwa kufanya kazi nje ya muda wa kazi, likizo tunanyimwa, tunatishiwa kufukuzwa kazi.

Viongozi wetu wa tawi hawaambiliki, hawashauriki! hatuna pa kuhemea. Kupitia waraka huu tunaomba jicho la tatu litazame unyanyaswaji huu unaofanywa na Meneja wa tawi na wasaidizi wake ukomeshwe mara moja. Haki na ustawi wa wafanyakazi ipatikane.
Ndugu. Yangu nchi hii huwezi kumshinda boss kwenye kesi,una mawili,uache kazi au uvumilie,
Hapo ni serikalini,ukimshitaki huyo boss wako,unakuwa umemshitaki mwanasheria mkuu wa serikali,maana ndie atakae Fanya utetezi!!!upo hapo!!sasa kazi kwako!!unasuka au unanyoa
 
Hili siyo suala la kukosa maadili au nidhamu bali ni suala la kuheshimu haki za mfanyakazi! Mwanasheria mkuu wa serikali hahusiki katika utetezi bali ni suala la utendaji ndani ya taasisi!
 
Back
Top Bottom