Manyara: Bashungwa amvaa mkandarasi wa stendi ya Katesh

Manyara: Bashungwa amvaa mkandarasi wa stendi ya Katesh

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
BASHUNGWA AMVAA MKANDARASI WA STENDI YA KATESH - HANANG

OR TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa Kituo kipya cha Mabasi Katesh katika Halmashauri ya Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara.

Akikagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Hanqng leo 26, Septemba 2022. Bashungwa amesema kasi ya Mkandarasi Erelai Construction Company Limited wa Arusha ni ndogo na itasababbisha mradi huo kutokukamilika kwa wakati uliopangwa.

Waziri Bashungwa amesema kuwa Serikali tayari imetoa kiasi cha shilingi bilioni 2 kwa ajili ya kuanza ujenzi tangu mwezi Feburuari, mwaka huu lakini mpaka sasa ujenzi huo una sua sua na kulingana na Makubaliano ya Mkataba.

“Hivyo naagiza kama mkandarasi ameshindwa kufanya kazi atolewe na awekwe mkandarasi mwingine atakayekamilisha kazi kwa wakati ili wananchi kuweza kunufaika na matunda ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan”, ameagiza Mhe. Bashungwa

Vile vile, Bashungwa amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Manyara kuhakikisha anasimamia kitengo cha manunuzi hasa katika suala zima la kuwapata wakandarasi wenye uwezo kwa kuangalia weledi na uzalendo katika kutekeleza miradi ya maendeleo.

Aidha, Ameviagiza vitengo vya manunuzi vihakikishe vinachambua kwa kina wakandarasi wanaoomba kazi za ujenzi ili kuwapata wenye weledi wa kifanyakazi kwa thamani ya fedha inayotolewa iendane na kazi iliyofanyoka.

Mradi umekamilika kwa asilimia 27 ambapo ulianza kutekelezwa 25 Feburuari, mwaka huu na kutakiwa kukamilika mnamo 25 Feburuari, 2023.

IMG-20220926-WA0110.jpg

IMG-20220926-WA0109.jpg

IMG-20220926-WA0112.jpg

IMG-20220926-WA0111.jpg

IMG-20220926-WA0113.jpg
 
Huyu waziri awe na tabia ya kuchukua hatua sitahiki mara ubadhirifu unapotokea kwenye eneo la kazi la wizara hii ya OR - TAMISEMI. Kuna ubadhirifu mwingi na mkubwa humo lakini hatua zinazochukuliwa hazieleweki eleweki! Kuna laxicity ya aina fulani ndani ya wizara hii au hata uwepo wa uzembe katika kuchukua hatua za kinidhamu kwa wabadhirifu ndani ya wizara hii.
 
INJINIA ANASUTWA KAKAA KIMYA KIKUBWA MKONO UENDE KINYWANI.
 
Nani alimpatia hiyo kazi kazi huyo mchaga mwizi anaitwa Lema Magufuli alimpiga ndani miaka. Kwanini hii Serikali haijifunzagi?
Acha kutoa mapovu, waziri angetuambia mkandarasi kalipwa kiasi gani Vs kazi iliyofanyika ndipo ungeweza kutoa shutuma, otherwise unaonyesha chuki binafsi za mentor wako.
 
Kwann Bashingwa amvae mkandarasi wakati yeye kupitia wizara yake ndiye alipaswa kumsimamia? Viongozi waache kujikosha.
 
Mwanangu stuka hapa JF mchagga hasemwi kwa ubaya ukifanya hivyo uzi unapotezewa au unapotezwa. Mark my words
We umechanganyikiwa, mchaga ndiyo mdudu gani. Mi nawaonaga km mazuzu flani mnajisifu kipumbavu. Nani anazingatia nyie maskini wa rasilimali mnaoishi km wakimbizi ndani ya nchi.
 
Back
Top Bottom