Manyara: Binti ajinyonga baada ya kugombezwa na dada yake

Manyara: Binti ajinyonga baada ya kugombezwa na dada yake

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Binti mwenye umri wa miaka 14, Silvan Tumaini Isdori Mkazi wa Mtaa wa Majengo ya zamani Babati Mjini Mkoani Manyara amejiua kwa kujinyonga na chandarua chumbani kwake mara baada ya kugombana na dada yake aliyekuwa anaishia naye.

Chanzo cha Ugomvi kimeelezwa kuwa ni baada ya dada wa Marehemu Victoria Tumaini kumuagiza marehemu sahani na kijiko ili wapakue chakula marehemu akaleta sahani bila kijiko.

Baada ya kuagizwa tena kijiko ndipo marehemu akamwambia dada yake kuwa nimechoka kutumwatumwa, ugomvi ukaanzia hapo na marehemu akachukua uamuzi wa kususia chakula na kwenda chumbani kwake na kujinyonga.


Source: Azam TV
 
Hizi kesi za watoto kujiua mbona zimekua nyingi?
 
Wangejinyonga kina junior nisingeshangaa

Sasa hadi watoto wa mbwa nao

Hapo kuna visa nyuma na depression
 
Balehe kwa vijana na kuvunja ungo wa wasichana huwa ni balaa !! mabadiliko ya mwili huletaniza mambo mengi - ujeuri na kujifanya ushakuwa mkubwa na unajua kila jambo ndicho chanzo kikuu.
 
Matatizo ya akili ni tatizo kubwa hii nchi
Mkuu ile takwimu ya 5:3 yawezekana ina ukweli 😀 yaani katika watu 5 basi 3 wana matatizo ya akili, madishi hayakamati network.
 
Back
Top Bottom