Pre GE2025 Manyara: CV za Wabunge mwaka 2020 - 2025. Mbunge wako ametimiza ahadi zake?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Wakuu,

1. Samweli Xaday Hhayuma – Mbunge wa Hanang

Chama Cha Siasa: Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Matokeo ya Uchaguzi wa 2020: Samweli alipata kura 14,203, akimshinda Kiza Hussein Mayeye kutoka CHADEMA ambaye alipata kura 20,342.

Michango Bungeni: Samweli ameleta michango 34 na kuuliza maswali 68 bungeni.

Safari ya Elimu:

Shule ya Msingi: Bassotughang (1985–1991), alipata cheti cha CPEE.
Shule ya Sekondari: Tanga Technical Secondary School (1992–1995), alipata cheti cha CSEE.

Vyeti na Shahada:

1999: Full Technician Certificate (FTC) kutoka Dar es Salaam Institute of Technology.
2006: Advanced Diploma in Electronic Telecommunication Engineering.
2010: Postgraduate Diploma in Health Technology Management kutoka Chuo Kikuu cha Cape Town.
2014: Pre-Masters Program katika Chuo cha Eulji.

Masters in Biomedical Engineering kutoka Burkina Faso Institute of Science and Technology.

Kazi Zake:

Aliwahi kufanya kazi katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (2008–2014) kama Health Care Technical Service Program Officer na Biomedical Engineer.

Pia aliwahi kuwa Medical Devices and Diagnostics Registration Officer katika Tanzania Food and Drugs Authority (TFDA) kutoka 2014 hadi 2020.

Lecturer katika Dar es Salaam Institute of Technology (2013–2021).

2. Olelelkaita Edward Kisau – Mbunge wa Kiteto

Chama Cha Siasa: Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Matokeo ya Uchaguzi wa 2020: Olelelkaita alipata kura 48,632, akimshinda Florence Kong'oke kutoka CHADEMA aliyepata kura 12,384.

Safari ya Elimu:

Shule ya Msingi: Ndendo Primary School (1987–1993).
Sekondari: Ekenywa Secondary School (kihitimu 2000), na Agape Lutheran Junior Seminary (kihitimu 2003).

Vyeti na Shahada:

2007: Bachelor of Law (LLB Hons) kutoka Tumaini University, Iringa.
2008–2009: Postgraduate Diploma in Law kutoka Law School of Tanzania.
2010: Masters Degree in Law (LLM) kutoka Stellenbosch University, Afrika Kusini.

Kazi Zake:

2010–2020: Wakili katika Ujamaa Community Resource Team (UCRT).
2012–2020: Advocate katika Ramatlaw Advocates & Legal Consultants.

Kuingia Kwenye Siasa:

Olelelkaita ni mjumbe wa UVCCM Central Council Mkoa wa Manyara (2009) na mjumbe wa District General Meeting (2017) ndani ya CCM.


3. Issaay Zacharia Paulo – Mbunge wa Mbulu Mjini

Chama Cha Siasa: Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Matokeo ya Uchaguzi wa 2020: Paulo alipata kura 28,264, akimshinda Gervas Maiko Sulle kutoka CHADEMA ambaye alipata kura 11,630.

Safari ya Elimu:

Shule ya Msingi: Ilawi Primary School (1973–1979).
Shule ya Sekondari: Kasu Islamic Centre Secondary School (2011–2013).
Huduma ya Jeshi: Alishiriki kwenye shughuli za JWTZ kutoka 1980 hadi 1986.

Kuingia CCM:

Paulo amekuwa na nyadhifa mbalimbali ndani ya CCM, ikiwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Wilaya, Mjumbe wa Baraza la Mkoa, na Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Wilaya ya Mbulu.

Kazi Nje ya Siasa:

1990–1995: Alikuwa mwanachama wa bodi mbalimbali binafsi.
1995–2005: Aliongoza Bodi ya Elimu ya Kanisa Katoliki Mbulu kama Mwenyekiti.
2005–2015: Aliwahi kuwa Diwani na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, pia aliongoza ALAT kwenye ngazi ya mkoa na kitaifa.


4. Flatei Gregory Massay – Mbunge wa Mbulu Vijijini

Chama Cha Siasa: Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Matokeo ya Uchaguzi wa 2020: Massay alipata kura 46,737, akimshinda Amani Paul Nanagi Gaseri kutoka CHADEMA ambaye alipata kura 5,895.

Safari ya Elimu:

Shule ya Msingi: Sanu Baray Primary School (1982–1988).
Shule ya Sekondari: Imboru na Chief Sarwat Secondary Schools.
Diploma: Diploma katika Maendeleo ya Jamii kutoka Community Development College - Monduli (2014).

Kazi Zake:

1999–2002: Katibu wa Vijana wa Wilaya ya CCM.
2012–2017: Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM.
Kiongozi wa Mashindano ya Mwenge wa Uhuru.
Aliwahi kuwa mwandishi katika Radio Habari Njema.


5. Christopher Olonyokie Ole Sendeka – Mbunge wa Simanjiro

Chama Cha Siasa: Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Matokeo ya Uchaguzi wa 2020: Ole Sendeka alipata kura 51,452, akimshinda Landey Emanuel Isack kutoka CHADEMA ambaye alipata kura 8,782.

Safari ya Elimu:

Shule ya Msingi: Naberera Primary School (1974–1980).

Shule ya Sekondari: Monduli (1981–1984) na Old Moshi High School (1985–1987).

Diploma: Alipata Diploma ya Maendeleo ya Jamii kutoka Kimmage Manor, Dublin, Ireland (1994–1996), kupitia mafunzo ya Ms-TCDC.

Kuingia Kwenye Siasa:

Ole Sendeka alianza kujihusisha na siasa akiwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Simanjiro (1989–1994) na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya UVCCM.

Alikuwa Diwani wa Kata ya Naberera (1994–2000) na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Simanjiro (1993–2007).

Alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (1997–2007).

Kazi za Serikali:

Afisa Tarafa: Alifanya kazi chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (1991–1993).
Mkuu wa Mkoa wa Njombe: Aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe (2016–2020).
Msemaji Mkuu wa CCM: Aliteuliwa kuwa Msemaji Mkuu wa CCM Makao Makuu mwaka 2016.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…