benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Kijana wa Kimasai rika la Morani, aliyejulikana kwa jina Sabaya Isaskar (31) mkazi wa Njaniodo, wilayani Kiteto mkoani Manyara amedaiwa kujinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba ya manila.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Partimbo, Kimirei Mesiaya amethibitisha kutokea kwa kifo hicho leo Jumatatu Oktoba 23, 2023 akisema marehemu alikutwa porini juu ya mti ananing’inia na wasamaria wema waliokuwa wakipita kilometa 3 kutoka nyumbani kwake baada ya kujinyonga.
"Nilipokea taarifa ya mtu kujingonga porini na baadaye nikafuatilia na kubaini kifo hicho ambacho kwa kweli kinasikitisha sana, kwani aliyepoteza maisha hakuwa mgonjwa bali ameamua kuchukua maamuzi magumu ya kujiua," amesema Mesiaya.
Mwananchi