Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
HISTORIA YA MKOA WA MANYARA
Kwa mujibu wa tovuti ya Mkoa wa Manyara, Mkoa huu ulianzishwa kwa tangazo la Serikali Na. 367 lililotolewa tarehe 27 Julai, 2002 na kuchapishwa katika gazeti la Serikali tarehe 2 Agosti, 2002 baada ya kugawanywa kwa Mkoa wa Arusha ambao kabla na wakati wa kipindi cha Uhuru ulijulikana kama Jimbo la Kaskazini (Northern Province). Miongoni mwa Wilaya zilizounda Mkoa huo ni Mbulu na Maasailand ambazo sehemu kubwa iko katika Mkoa wa Manyara sasa. Wilaya hizo ziligawanywa kama ifuatavyo: Wilaya ya Mbulu ilianzisha Wilaya ya Hanang mwaka 1969 na Hanang ikianzisha Babati mwaka 1985, wakati Wilaya ya Maasailand iligawanywa kwenye Wilaya ya Kiteto mwaka 1974 ambayo pia iligawanywa na kuanzisha Wilaya ya Simanjiro mwaka 1993. Baada ya kugawanywa kwa Mkoa wa Arusha, Wilaya za Mbulu, Hanang’, Babati, Kiteto na Simanjiro ziliuunda Mkoa wa Manyara huku makao yake makuu yakiwa ni Babati mjini.
Mkoa wa Manyara unapakana na Mikoa ya Singida na Shinyanga upande wa magharibi, Mkoa wa Dodoma upande wa kusini, Mkoa wa Tanga upande wa mashariki na Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro Upande wa kaskazini.
Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 yanaonesha kuwa idadi ya watu katika Mkoa wa Manyara ni watu 1,892,502; wanaume 954,879 na wanawake 937,623.
Pia, soma: Orodha ya Nyuzi za Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
MUHTASARI WA MAENEO YA UTAWALA, MKOA WA MANYARA
Mkoa wa Manyara una mfumo wa kiutawala unaojumuisha mamlaka za miji na wilaya zinazoratibu maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Mkoa huu unajumuisha mamlaka mbili za miji na wilaya tano, kila moja ikiwa na muundo wake wa kiutawala unaozingatia kata, mitaa, vijiji, na vitongoji.
HALI YA KISIASA
Uchaguzi mkuu 2020 ulipeleka ushindi kwa Chama tawala CCM na kupelekea wabunge wote wa majimbo ya mkoa huu kutoka Chama Cha Mapinduzi hivyo kudhihirisha ushindani mdogo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. Kuelekea uchaguzI uchaguzi mkuu 2025, inatazamiwa kuwepo kwa kuimarishwaji kwa demokrasia hasa katika kuleta uchaguzi huru na wenye haki ili kuchochea ushindani kwa vyama vyote vya siasa.
MAJIMBO YA KIUCHAGUZI
Mkoa huu una Halmashauri (7) na majimbo saba (7) ya uchaguzi ambayo ni:
- Babati vijijini
- Babati Mjini
- Hanang
- Mbulu vijijini
- Mbulu Mjini
- Simanjiro
- Kiteto
Haya ni Matokeo ya idadi ya kura walizopata wagombea katika majimbo ya uchaguzi yaliyopo mkoa wa Manyara katika uchaguzi wa mwaka 2020.
Katika Jimbo la Uchaguzi la Hanang, wagombea walikuwa John Safari Mandoo wa ACT-Wazalendo aliyepata kura 1,447, Hhayuma Samweli Xaday wa CCM aliyepata kura 50,780, na Magoma Rashid Derick Magoma wa CHADEMA aliyepata kura 20,342. Mgombea aliyeshinda na kuchaguliwa ni Hhayuma Samweli Xaday wa CCM.
Katika Jimbo la Uchaguzi la Kiteto, wagombea walikuwa Kamota Honesty Amasha wa ACT-Wazalendo aliyepata kura 2,229, Olelekaita Edward Kisau wa CCM aliyepata kura 48,632, Pastor Florence Kong'oke wa CHADEMA aliyepata kura 12,384, na Ibrahim Selemani Msindo wa CUF aliyepata kura 782. Mgombea aliyeshinda ni Olelekaita Edward Kisau wa CCM.
Katika Jimbo la Uchaguzi la Mbulu Mjini, wagombea walikuwa Issaay Zacharia Paulo wa CCM aliyepata kura 28,264, Gervas Maiko Sulle wa CHADEMA aliyepata kura 11,630, na Agustino Boay Tarmo wa CUF aliyepata kura 319. Mgombea aliyeshinda ni Issaay Zacharia Paulo wa CCM.
Katika Jimbo la Uchaguzi la Mbulu Vijijini, wagombea walikuwa Herson Nade Baynit wa ACT-Wazalendo aliyepata kura 669, Flatei Gregory Massay wa CCM aliyepata kura 46,737, na Amani Paul Nanagi Gaseri wa CHADEMA aliyepata kura 5,895. Mgombea aliyeshinda ni Flatei Gregory Massay wa CCM.
Katika Jimbo la Uchaguzi la Simanjiro, wagombea walikuwa Ole Sendeka Christopher Olonyokie wa CCM aliyepata kura 54,609, na Landey Emanuel Isack wa CHADEMA aliyepata kura 8,782. Mgombea aliyeshinda ni Ole Sendeka Christopher Olonyokie wa CCM.
6. JIMBO LA UCHAGUZI BABATI BABATI MJINI
- Gekul Pauline Philipo (CCM )
- Sillo Daniel Baran (CCM)
JANUARY
FEBRUARY
- RC wa Manyara Queen Sendiga: Nitashangaa mwanamke unampigia kura mwanaume. Utakuwa umesaliti ajenda ya wanawake
- Ally Hapi amesema CHADEMA wasitumie No reform no election kama njia ya kukimbia mapambano, adai mabadiliko Watanzania wameshayaona
- CCM wasikiliza kero za Wananchi Babati. Ally Hapi atoa elfu 50 kwa mstaafu wa jeshi tangu mwaka 1994 ambaye anadai mafao mpaka leo
- Mama aliyevunjiwa Kibanda apewa mtaji wa TSh. 250,000 na Ally Hapi
- Ally Hapi aonya viongozi Miungu watu akiwataka kuacha kuwaonea wananchi na kupora mali zao