Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Mchimbaji wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro mkoani Manyara, Erick Peter (36) anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumpa mimba mwanafunzi wa shule ya sekondari Tanzanite wa kidato cha nne.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Manyara, Benjamin Kuzaga akizungumza leo Jumanne, Septemba 6, 2022 amesema Erick anashikiliwa kwa tuhuma za kumpa mimba mwanafunzi wa shule ya sekondari Tanzanite ya mji mdogo wa Mirerani.
Kamanda Kuzaga amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa Septemba 1, 2022 akiwa mtaa wa Msikitini mji mdogo wa Mirerani.
"Tulimkamata mtuhumiwa huyo akiwa nyumbani kwa baba wa mwanafunzi huyo na kulazwa mahabusu kituo cha polisi Mirerani na tunatarajia kumfikisha mahakamani uchunguzi ukikamilika," amesema Kuzaga.
Baba wa mwanafunzi huyo, Shabani Khamisi ameiomba Serikali kuhakikisha mtuhumiwa huyo Erick afikishwe mahakamani ili kujibu shtaka hilo linalomkabiki.
"Huyu why not amempa mimba mtoto wangu kisha anaita wazee ili anilipe fedha na kumaliza juu juu, hili jambo nami sijakubali itabidi aende mahakamani akashtakiwe huko," amesema Khamisi.
Amesema lengo lake ni kuhakikisha mtuhumiwa huyo anahukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa kumpa mimba mtoto wake ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha nne anayetarajia kufanya mtihani Novemba 2022.
MWANANCHI