Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
Mwaka 1958 Mao alitangaza maadui wanne wa taifa. Nzi, mbu, panya na Shomoro walitangazwa. Kosa la Shomoro lilikuwa ni kula nafaka. Sasa hawa shomoro hawawezi kuruka kwa muda mrefu bila kupumzika. Watu wa miji mikubwa walichofanya ni kutoka mitaani na mangoma, mabati, mabakuli nk. walianza kupiga makelele mji mzima. Ndege wakatoka viotani mwao wamepanic. Wakitaka kutua watu waliwapigia ngoma, mayowe na kuwarushia mawe, hakuna kutua. Baada ya muda ndege walianza kuchoka na kuanguka. Ndani ya siku tatu waliua shomoro 400,000!!. Mitego pia ilitumika.
Sasa kumbe pamoja na shomoro kula mbegu pia walikuwa wanakula wadudu waharibifu kama nzige. Nzige wakaongezeka na kula mazao na kusababisha njaa iliyoua karibu watu 60m. Baadaye shomoro akatolewa kama adui na nafasi ikachukuliwa na kunguni.