Mao Zedong alipotangaza vita dhidi ya ndege shomoro(sparrow)!

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Mwaka 1958 Mao alitangaza maadui wanne wa taifa. Nzi, mbu, panya na Shomoro walitangazwa. Kosa la Shomoro lilikuwa ni kula nafaka. Sasa hawa shomoro hawawezi kuruka kwa muda mrefu bila kupumzika. Watu wa miji mikubwa walichofanya ni kutoka mitaani na mangoma, mabati, mabakuli nk. walianza kupiga makelele mji mzima. Ndege wakatoka viotani mwao wamepanic. Wakitaka kutua watu waliwapigia ngoma, mayowe na kuwarushia mawe, hakuna kutua. Baada ya muda ndege walianza kuchoka na kuanguka. Ndani ya siku tatu waliua shomoro 400,000!!. Mitego pia ilitumika.

Sasa kumbe pamoja na shomoro kula mbegu pia walikuwa wanakula wadudu waharibifu kama nzige. Nzige wakaongezeka na kula mazao na kusababisha njaa iliyoua karibu watu 60m. Baadaye shomoro akatolewa kama adui na nafasi ikachukuliwa na kunguni.

 
Mao hakuwa na elimu na alikuwa ana mihemko sana. Ndo maana Deng Xhiaoping alipomrithi alisema 'socialism does not mean poverty'. Deng alikuwa mstaarabu na aliyeelimika, uchumi na maendeleo vilipatikana
 
Naunga mkono hapo kwa kunguni kutangazwa adui.
 
Mao aliwarostisha wachina sana huyo mzee
Ila kitu kimoja positive kwake, aliiungnaisha China na kulinda mipaka yake ipasavyo
 
ecosystem
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…