benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Serikali imekabidhi magari 51 kwa maofisa elimu wa sekondari wa halmashauri, kuongeza ufanisi, usimamizi na ufuatiliaji wa slimu nchini. Akizungumza katika hafla ya kukabidhi magari hayo jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Angellah Kairuki alisema ni matarajio ya serikali vombo hivyo vitakuwa nyenzo muhimu kwa maofisa elimu katika usimamizi na ufuatiliaji wa elimu.
Kairuki alisema serikali ya awamu ya sita inatambua jukumu la usimamizi wa elimu linahitaji uwajibikaji na usimamizi thabiti katika ngaziyataifa, mikoa, halmashauri, katanashule. Alifafanua mafanikio yanatokana na usimamizi mzuri wa elimu, bidi, weledi, ubunifu, uaminifu na utifu ambavyo pia vinategemea uwezeshwaji
wa vifaa na vitendea kazi kwa maofisa husika.
"Magari nitakayogawa leo ni awamu ya pili ya ununuzi na awamu ya nne ya sehemu ya ugawaji wa magari kwa maofisa elimu wa sekondari," alisema.
Aliongeza: "Katika awamu tatu za awali jumla ya magari 95 yalipokewa na kugawiwa, pia magari 89 yalipokewa ngazi ya halmashauri, manne ngazi ya wizara, moja Shirika la Elimu Kibaha na kwa Katibu Tawala Msaidizi (elimu) Mkoa wa Lindi."
Alisema ununuzi na ugawaji wa magari hayo ni mwendelezo wa juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kuboresha elimu. Waziri Kairuki alisisitiza matarajio ya serikali magari hayo yatatunzwa kuongeza ufanisi na ubora wa elimu katika utekelezaji wa majukumu ya elimu ya sekondari kwa ngazi ya halmashauri.