Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Familia ya watu sita wilayani Monduli, mkoani Arusha kwa siku nne imelala nje, baada ya nyumba zao kuchomwa moto na wanaodaiwa kuwa maofisa maliasili.
Watu hao wanaoishi Kata ya Monduli Juu wanadaiwa kuishi ndani ya hifadhi ya msitu wa jamii katika Kijiji cha Emairete.
Akizungumza na Mwananchi jana Januari 10, 2025 katika kijiji hicho, baba wa familia hiyo, Faraja Mephoroo amesema Januari 7, saa 12:00 asubuhi walifika watu aliodai aliwatambua kuwa wanafanya kazi kitengo cha maliasili walioambatana na mgambo na viongozi wa kijiji waliochoma nyumba zake tatu walizokuwa wakiishi na wake zake.
Akizungumza na Mwananchi ofisa maliasili Wilaya ya Monduli, Adili Mwanga amesema suala hilo liko ofisi ya kijiji ndio wanaoweza kutoa maelezo.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Emairete, Mboyo Kaiyai amesema wameamua kuchukua hatua hiyo baada ya juhudi za mawasiliano ya kawaida ya kumhamisha mwananchi huyo kugonga mwamba.