Maofisa ustawi wa Jamii 268 ngazi ya kata, wapo katika kata gani?

Maofisa ustawi wa Jamii 268 ngazi ya kata, wapo katika kata gani?

Kabinti ka ludilo

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2014
Posts
409
Reaction score
468
393819643.jpg


Wakuu,
Mimi nauliza hao maafisa ustawi wapo katika kata ipi. Maana nina uzoefu wa wilaya kama Kyela, Ludewa, Njombe, na Mufindi, zote hazina Afisa ustawi wa jamii hata mmoja ngazi ya kata. Je wapo wapi hao maafisa ustawi ngazi ya kata?
 
View attachment 2187865wakuu,
Mimi nauliza hao maafisa ustawi wapo katika kata ipi. Maana nina uzoefu wa wilaya kama Kyela, Ludewa,Njombe, na Mufindi, zote hazina Afisa ustawi wa jamii hata mmoja ngazi ya kata. Je wapo wapi hao maafisa ustawi ngazi ya kata?
Tumia pesa ikuzoee, miaka miwili mtoto wa mjomba atakuwa anamiliki bodaboda yake na hicho ndicho kipaumbele cha ununuzi kama walivyosema wenyewe!
Tutegemee uchaguzi wa serikali za mitaa CCM itakuwa na bodaboda za kampeni zilizonunuliwa na serikali.
 
Kata nyingi zinao maafisa maendeleo ya Jamii ngazi ya kata sio maafisa ustawi
 
Sijawahi kuwakuta maofisini hata siku moja, wanashindaga saluni ukimsumbua sana anakuambia nipo kikao kwa mkuu wa wilaya.
 
Hapa kuna dili mkuu, kwanza awali walisema zilinunuliwa 68 walipoona mtandaoni kumewaka wakabadili gia angani.
Kwanini zinunuliwe 268 halafu zitolewe 68 tu? Je hizo nyingine ziko wapi? Walipotoa taarifa ya awali ina maana hawakuwa wameipitia ili waone kasoro kabla ya kuiachia?

Kwanini wasiorodheshe hizo kata kwa majina? Na bado hiyo bei iko juu.

Nchi ya wabwia asali hii.
 
Wale "vijana wa halaiki" walikuwa wanatetea pikipiki 68 kwa 11M each kwamba pikipiki za serikali ni Yamaha AG200 siyo Boxer.

Sasa wenyewe wamebadili gia angani kuzima kelele na kusema ziko 268 siyo 68, njooni tena mtuambie kwa nini serikali hainunui tena pikipiki "zake" (Yamaha)?

Hii mikanganyiko itakuwa mingi mno Kipindi hiki.
 
Ukigawanya unapata pikipiki moja ni 2.947M.
 
Kama kuna mwanajamii forum kata yake inamtu anaeitwa "Afisa ustawi wa jamii wa kata " naomba ajitokeze tafadhari
 
Back
Top Bottom