Maofisa wa TFF wafikishwa mahakamani na TAKUKURU kwa tuhuma za rushwa

RUCCI

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2011
Posts
1,701
Reaction score
1,714
Baada ya tetesi za muda mrefu na tuhuma za baadhi ya viongozi wa shirikisho la soka Tanzania TFF kudaiwa kuomba rushwa ili waweze kupanga matokeo ya mechi za Ligi daraja la kwanza ili wa wapande Ligi Kuu.

Leo November 9 2016 Taasisi ya kupambana na kuzuia Rushwa TAKUKURU wamekamilisha uchunguzi wao na kuwafikisha mahakamani maofisa wawili wa TFF Juma Matandika ambaye ni msaidizi wa Rais wa TFF Jamal Malinzi na Frank Chacha.

Matandika na Chacha wamefikishwa mahakama ya Kisutu kwa tuhuma za kuomba rushwa ya Tsh milioni 25 kutoka timu ya Geita Gold ili waisaidie kupanda Ligi Kuu kutoka Ligi daraja la kwanza.

Kwa pamoja Matandika na Chacha wamekana mashtaka na wapo nje kwa dhamana ya Tsh milioni 5 kila mmoja na kesi yao imeahirishwa hadi November 30, wawili hao wanadaiwa kutenda kosa hilo February 4 2016 katika ofisi za TFF.
 
Huyu Frank Chacha ndio alifungua kesi kuzuia mkutano wa Yanga ?
 
Hata lile li-nzi likubwa limeiibia na kuidhulumu tff sana mbona lenyewe wameliacha? Hata kwenye upangaji matokeo nzi alikuwemo lakini sijasikia akishughulikiwa.
 
Baada ya tetesi za muda mrefu na tuhuma za baadhi ya viongozi wa shirikisho la soka Tanzania TFF kudaiwa kuomba rushwa ili waweze kupanga matokeo ya mechi za Ligi daraja la kwanza ili wa wapande Ligi Kuu.

Leo November 9 2016 Taasisi ya kupambana na kuzuia Rushwa TAKUKURU wamekamilisha uchunguzi wao na kuwafikisha mahakamani maofisa wawili wa TFF Juma Matandika ambaye ni msaidizi wa Rais wa TFF Jamal Malinzi na Frank Chacha.

Matandika na Chacha wamefikishwa mahakama ya Kisutu kwa tuhuma za kuomba rushwa ya Tsh milioni 25 kutoka timu ya Geita Gold ili waisaidie kupanda Ligi Kuu kutoka Ligi daraja la kwanza.

Kwa pamoja Matandika na Chacha wamekana mashtaka na wapo nje kwa dhamana ya Tsh milioni 5 kila mmoja na kesi yao imeahirishwa hadi November 30, wawili hao wanadaiwa kutenda kosa hilo February 4 2016 katika ofisi za TFF.
Lisemwalo lipo. Kwa miaka mingi watu wamekuwa wakilalamika kuhusiana na rushwa kwa viongozi wa mpira na wamekuwa wakikana. Sasa tuone mpira huu wa takukuru utaishia wapi.
 
Yote haya ni kwa sababu ya uroho na ujingaujinga wa bwanyenye mulinzi the big taahira
 
"mpokeaji na mtoaji wote wana hatia"

sasa hapa mbona naona wamewashika "wapokeaji" tuuu??

wapo wapi "watoa" rushwa hii akina "kulunge"??

TAKUKURU viongozi wa GGS pia ni wahusika msiwaache njee!
 
Back
Top Bottom