Dialogist
JF-Expert Member
- Apr 14, 2014
- 1,167
- 1,872
Mheshimiwa Rais Wetu Mpendwa Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania...
Salaam Nyingi Zikufikie Hapo Ulipo. Natumai nawe umepumzika kwa namna fulani katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka, kama ambavyo sisi tumepumzika hapa Serengeti National Park.
Nisikuchoshe sana Mh. Rais..
Maombi Yangu Ni Haya Yafuatayo...
Kwa kufuata historia ya kipindi kifupi cha uongozi wake, muda huu na muda uliopita, ni wazi kabisa Mh. Paul Makonda ndiye Mkuu wa Mkoa Bora Kabisa Kwa Muongo huu tulionao. Na hiyo ni tathmini yangu mimi mwananchi wa kawaida na tathmini na mtazamo wa wananchi wengi wa kawaida ambao hawana mfungamano wa kisiasa wala sio bendera fuata upepo kwa shutuma na maneno ya wanasiasa bila ushahidi. Kwa maana huyu Mheshimiwa popote anapopelekwa tumeona mabadiliko makubwa sana ya kiuchumi na maisha ya watu wa hali ya chini kwa haraka sana. Kwa sababu ya kubuni miradi mbalimbali vya kunufaisha jamii.. Na ndio sababu ni nadra sana kusikia Mheshimiwa huyu anapingwa na sisi wananchi wa kawaida.
Kwa muktadha huo Mh. Rais, ninakuomba sana huyu Bwana Makonda asikae kwenye mkoa mmoja kwa muda mrefu. Mpe mwaka mmoja tu ili azunguke mikoa yote kuichangamsha na kuinua chumi za mikoa husika na kutengeneza ari ya watu kufanya kazi. Kuna mikoa hapa Tanzania Inamuhitaji sana Makonda, hiyo mikoa ni kama imekufa au haina viongozi wabunifu.
Mheshimiwa Rais, Makonda anahitajika sana Tanga, ule mji umekaa kimwinyi sana. Watu hawafanyi kazi.
Mheshimiwa Rais, Makonda anahitajika sana Shinyanga, huo mji ni kama umekufa kabisa, unahitaji kiongozi mpambanaji na mwenye uthubutu. Hakuna mzunguko pale.
Mheshimiwa Rais, Makonda anahitajika sana Lindi na Mtwara, hao jamaa hawaamini katika kitu kingine zaidi ya Korosho. Siku korosho zikifeli na maisha yao yamefeli.
Mheshimiwa Rais, Makonda anahitajika sana Kigoma, mkoa umepoa sana utadhani haupo mpakani. Hakuna mzunguko wa hela kabisa.
Mheshimiwa Rais, Makonda anahitajika sana Tabora, aiunganishe central zone yote.
Hiyo ni kwa uchache Mheshimiwa Rais, naamini ni mikoa mingi kama sio yote inamuhitaji sana Mh. Paul Makonda au mtu wa kariba yake. Dar es Salaam ndio mahali ambapo ni ndoto za kila Mwana Dar es Salaam, jamaa arudi. Mji umepoa sana Mheshimiwa. Leo Arusha Ndio inajulikana Duniani (kiding kidogo)
Kama ukiona umpandishe cheo zaidi basi Mheshimiwa Rais usimrudishe kuongoza CCM, bali mpe Ubunge na Hatimaye Uwaziri Wa Ujenzi au Masula Ya Vijana. Huyu atakusaidia Sana.
Mheshimiwa Rais ni hayo tu kwa leo na Nakutakia Mapumziko Mema na Baraka Nyingi Katika Kuuanza Mwaka Mpya 2025. Mungu Akusimamie,Akupe Hekima Na Busara Tele Hasa Tunapoingia Katika Mwaka wa uchaguzi.
Ni Mimi..
Dialogist
Mwamba Dia Wamba Kutoka Musoma!!
NB: Maoni Yangu Na Mtazamo Wangu Ni Wa Kijamii, Usifungamanishwe Na Mtazamo Wa Kisiasa.