Wanatoa ajira kwa wote mimi kuna watu nawafahamu wamekaa kitaa muda na wame pata ajira so kuwa mvumilv
Ni kweli mkuu. Ila subira ina mwisho wake. Njaa haiezi kusubiri.
Mi nadhani wangekua wanawasiliana na wateja wao (wasaka ajira)
Kwa maana ya kutoa public taratibu za ufanyaji kazi wao
Mfano waseme kabisa kuwa ukiapply basi tegemea kuitwa usaili baada ya mwezi mmoja
Ukifanya usaili tegemea kuitwa kazini baada ya mwezi mmoja
Na kisha kweli huo muda uzingatiwe.
Na kama kuna shida bas waseme kuna shida imetokea muda wa majibu umesogezwa mbele
Changamoto unakuta mtu hujui siku ya kuitwa usaili ni lini au placement ya kazi ni lini. Unakaa kwa mashaka mashaka na mambo mengine huwezi kufanya
Mfano unakuta inabid mtu ahame mkoa kutafuta riziki lakin anafikiria hivi akihama au akianzisha ishu flan alafu muda mdogo kaitwa usaili au placement unaacha hiki unashika hiki.
Mawasiliano muhimu sana
Mfano ukifika ofisi flani au hospitali kisha mnapanga foleni masaa yanaenda kama mfanyakaz wa ofis asipotoa taarifa watu wataanza kupanik hasira na kuchoka
Ila akija mwakilishi akasema labda daktar kapata dharura anakuja baada ya masaa mawili au network ya benk imezingua itarud baada ya masaa matatu bas angalau wa kwenda kula ataenda wa kusubiri atasubiri na hakutakuwa na sintofahamu ya kinachoondelea
Yote ya yote ndo nchi yetu ilivo inabd watu wavumilie...wakiamua mda wanaona unafaa basi watatoa hayo majina.