Maonesho na mnada wa ng'ombe yanaanza leo Ubena Zomozi

JS Dairy Farm

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2022
Posts
331
Reaction score
744
Maonesho na mnada wa ng'ombe yananza leo Julai 15, 2022 na yataisha Julai 17, 2022.

Yanafanyikia Ubena Zomozi, kilometa chache kutoka Chalinze kama unaelekea Morogoro kwenye viwanja vya Highland estates ambavyo vipo pembeni ya barabara ya Morogoro, upande wa kulia Kama unaenda Morogoro.

Wote mnakaribishwa,mtapata fursa ya kujifunza masuala mbalimbali kuhusu ufugaji bora wa ng'ombe wa nyama na aina mbalimbali za ng'ombe wa nyama.

Pia utapata fursa ya kukutana na wafugaji waliofanikiwa, mabenk, taasisi mbalimbali zinazoshughulika na ufugaji wa ng'ombe wa nyama nk.

Kwa taarifa zaidi tembelea kurasa za mitandao ya kijamii ya JS Forms.


 
Nenda kwenye pages za Instagram za mbogo_ ranches na tccs_tanzania(Tanzania commercial cattle society) wameweka picha kibao ,kuna ng'ombe wenye kilo 900 na mbuzi wanaouzwa milioni sita.
Poa poa Mkuu ntapitia nitupie Macho
 

Tunaomba mrejesho kuhusu haya maonyesho kwa sie ambao hatukupata bahati ya kwenda...ikiwa na picha itapendeza zaidi!
 
Nimeona minada mingi ya Ng’ombe kama Zimbabwe na South Africa na hata Ulaya jamaa wanajitahidi sana kwa kutunza Ng’ombe zao
Yaani unakuta wana mpaka 1000 kg wengine na zaidi ingawa ni mbegu ila pia matunzo

Mkuu Naomba uambatanishe na picha kidogo ila tuhamasike na kujua tunakuja kuona Ng’ombe wa aina gani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…