Juzi wakati napita kwenye mataa ya morocco nikitokea mwenge-kariakoo niliona bango linaloashiria uwepo wa maonesho ya kilimo ambayo nimeona neno machinery kama uwepo wa vifaa vya kilimo. Sikulisoma vizuri lile bango na nimeshindwa kupata muda wa kwenda tena pale kwa ufuatiliaji. Naomba mwenye taarifa ya hii kitu ani/tupe hapa jamvini. Ningependa kama taarifa zitapatikana zilizo sahihi kuwashauri member wenzangu wenye uchu wa ujasiriamali kuhudhuria kwa wingi kupata taarifa mabalimbali huko.
Natanguliza shukrani.