Maoni binafsi kuhusu muungano na maoni juu ya muundo

Maoni binafsi kuhusu muungano na maoni juu ya muundo

Meddah Sotta

Member
Joined
Oct 31, 2013
Posts
5
Reaction score
1
MAONI BINAFSIKUHUSU MUUNGANO NA MAONI JUU YA MUUNDO.
Binafsi siamini katika kudumu na kuwepo kwa muungano wa Tanzania katikamfumo wa muungano wa serikali tatu kama ilivyo katika mfumo wa serikali mbili,kwangu mimi serikali moja ndio suluhisho la kudumu na muunganiko wa kweli wataifa letu. Kwa mtazamo wangu mfumo wa serikali 3, shirikisho n.k, ni njia yakuelekea muundo wa serikali moja na sio mifumo ya kudumu hata mara moja.
Imani yangu katika serikali moja inatokana na changamoto nazozionazilizozaliwa na mfumo wa serikali 2 na huku nikiamini zitakuwa hata zaidi ndaniya serikali tatu. Ukiziangalia changamoto za muungano (ambazo zimepewa jina lakero za muungano), kama la kodi kwenye bandari ya Dar-es-Salaam kwa vituvianavyotoka Tanzania Visiwani n.k kimantiki, ni hitaji la Watanzania kudaikuunganishwa zaidi, kufanywa wamoja na sawa zaidi hata zaidi ya ilivyo sasa, nakwa maana hiyo kama madai, kimantiki, ni kuunganishwa zaidi, 'jaribio' lolote lakuzidi kuwagawa watu hawa kwa maana yoyote au njia yoyote ile ni wazi kwambaitasababisha matatizo na kuzalisha changamoto nyingi hata zaidi ya ilivyo hivisasa.
Pia, hoja ya Tanganyika kuimezaZanzibar sio hoja mpya na ilifikiriwa hata wakati wa kubuni mfumo wa sasa wamuungano. Hoja hii hii bado inaendelea kusimama hata leo japo inaweza kuwa kwasura tofauti kidogo, lakini ni wazi kabisa mfumo wa serikali tatu utaibua hojahii siku za usoni tena ikawa na nguvu na nzito zaidi ya sasa na hata ilivyokuwahapo awali, muungano kwa mfumo wa serikali 3 au shirikisho katika nchi yenyeidadi ya watu Milioni 43.6 na nchi yenye watu Millioni 1.3 inaweza kutafsiriwakama aina mpya ya ukoloni na 'wajuaji', zaidi inaweza ikawa tishio kubwa nahoja nzito dhidi ya uwepo wa muungano hata zaidi ya hivi sasa na hapo awalinchi zilipokuwa zinaungana ambapo Wazanzibar walikuwa Laki 3 na WatanganyikaMilioni 11.
Kwa maoni yangu, kuungana kwa muundo wa serikali moja, na kuunda taifamoja, Hakutomaliza, moja kwa moja, changamoto za muungano, bali utatufanyatuzifanyie kazi changamoto za muungano na kutafuta masuluhisho yake kama watuwamoja na wataifa moja. Serikali tatu, kwa njia yoyote ile, Haitomaliza, kamwe,matatizo ya muungano, bali itatufanya tujadili na kutafuta masuluhisho yachangamoto za muungano tukiwa kama watu tofauti ndani ya taifa moja, na lawamazote ziwe binafsi au za kikundi cha watu ndani ya muungano kumuangukia bwanamkubwa 'Serikali ya Muungano' kama mfano wa wanandoa wanaoishi nyumba moja nakuamua kuajiri 'msuluhishi' atakaye simama kati yao, ndoa kama hiyo utawaliwana lawama za upendeleo na matatizo yasiyo na majibu za kueleweka, wakati chaguosahihi lilitakiwa liwe kuchagua kukaa pamoja kama watu waliochagua kuishipamoja kwenye shida na raha ili wayazungumze na kutafuta ufumbuzi, au kuachana,na si kuchagua aina nyingine ya uhusiano ambao ni wazi kwamba utaongezamisuguano na hata kupelekea kuachana kabisa.
Mfano huo huo wa wana ndoa unaweza kuwa sawa kwenye muungano wetu, yapomachaguo mawili yaliyo sahihi kabisa, ni au, tunakubali kupambana na changamotozote na kuungana kabisa kama ndugu moja tulioamua kutoitambua mipaka hiiiliyowekwa na wakoloni na kuishi pamoja au kutengana kabisa, na sio kuchaguamachaguo ambayo kimantiki yatatutenganisha zaidi na kuzaa misuguano nachangamoto nyingi na nyingine zaidi, hata kupelekea kutengana kwa nchi zetu. Nivizuri na sahihi kama tumeamua kuungana na kuwa watu wamoja, basi tukachaguamfumo ambao utatufanya tuwe huru kabisa ndani ya nchi yetu kama watu wa moja,bila ya kujali mipaka na matabaka mbali mbali ambayo mengi ni matunda yaukoloni na ukoloni mamboleo.
Kuna hoja, ambayo imekuwa ikisemwa na wanasiasa, taasisi na watumbalimbali, nayo ni kwamba,'Serikali tatu katika rasimu ya Katiba mpya nimawazo ya Watanzania'. Inaweza ikawa iko sahihi kwa dhana ya 'Mawazo yaWatanzania' wanazozijua wasemaji, lakini mimi binafsi siamini kama 'Miundo yaSerikali' ndio hasa 'Maoni ya kweli ya Watanzania'. Hii ni kwasababu, wasomi nawanasiasa wa nchi yetu wameigeuza hoja ya Muungano kuwa Muundo wa Serikali,kana kwamba, Muundo wa Serikali ndio hasa Muungano wenyewe, na huku wakijuakabisa Watanzania wengi hatuna uelewa wa kutosha wa miundo hii ya serikalikwahiyo ni rahisi kuwadanganya watu katika misingi ya uongo, au yenye maslahibinafsi, vyama au taasisi zao.
Kila Mtanzania anajua ni Muunganiko ganianautaka na ndugu zake, lakini si kila Mtanzania anajua Miundo ya Serikali, nawengi wetu tumejikuta, tukiacha kujadili muungano wetu ambao hasa ni muunganikowa watu, kuongea ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa huru na wamoja ndani yaJamhuri yetu na kujikuta tunaongelea habari za serikali moja, mbili, tatu, nnen.k ambazo wengi wetu, ama hatuzijui kwa ufasaha, au hatujui tunachokiongea amatuna wazo la muundo wa muungano lakini hatujui linaangukia wapi hasa katikamiundo hiyo inayotajwa. Mfano mzuri unaweza ukawa, mtu anaetafuta maoni juu yanjia za kutunga sheria harafu anasimama mbele za watu na kuwauliza,"Ndugumnapenda sheria zitungwe vipi? Je mngependelea zaidi mfumo wadelegeted/subsidiary legislation au principal legislation?" Au mtuanaetaka maoni ya uchumi kutoka kwa watu halafu anauliza,"Ndugu, mnadhani'demand and supply' ina athiri vipi bei ya mafuta?". Ni wazi kwamba majibuya mifano hiyo yanahitaji mtu mwenye uelewa wa mambo hayo tofauti na kamaangeuliza,"Sheria zitungwe na bunge moja kwa moja au bunge pia liwelinauwezo wa kuzipa mamlaka idara nyingine ziweze kutunga sheria?" Hapo niwazi kila mtu angeweza kutoa mawazo yake.
Mifano hiyo hapo juu, naweza ifananisha na mjadala wa muungano katikakatiba mpya, mjadala wa Muungano, umekabiliwa na istilahi za kitaalamu au kamanikiazima maneno umekuwa 'subjected to technical jargons' na kuwaaminishawananchi kwamba wanapoongelea muungano basi ni miundo ya serikali na hawanamachaguo zaidi ya kutaja idadi ya serikali ndani ya muungano na wengi wetutukijikuta tukikosa machaguo japo tunataka muungano au kuishia kutaja muundoambao mwanasiasa, chama au msomi flani kausema, na hatimaye mjadala kuhama tokakwenye kujadili muungano 'katika mantiki ya kuungana kwa watu' na kuingiakwenye mfumo wa serikali kana kwamba 'mfumo wa serikali ndio hasa muunganowenyewe'.
Ni mtazamo wangu na imani yangu ya dhati kabisa kama Mtanzania mwenyeweangeachwa aongee na sio baadhi ya watu, vyama au taasisi kukaimu nafasi na hakihiyo ya Mtanzania, angesema anataka taifa ambalo anaweza akaenda kuishi,kutembea na kwenda kokote pale bila kuulizwa hati ya kusafiria au kibali, nchiambayo atajisikia yuko huru ndani ya mipaka yake na bila ya kubaguliwa,kutengwa n.k na hapo watalamu na wasomi wetu wangetusaidia kutujuza sifa hizozinapatikana wapi hasa katika miundo ya muungano au serikali, na sio kumuulizaMtanzania anataka 'Muundo gani wa serikali?' mana kwa kufanya hivyo ni sawa nakuwaambia Watanzania wasiojua Miundo ya Muungano au Serikali kwamba hawana hakiau nafasi ya kujadili muungano wa nchi yao.
Asanteni!
 
Meddah,

Mwanzoni nilikuwa simuungi mkono mwanakijiji na wazo lake la Serikali moja. Ila sasa hivi baada ya uchunguzi wangu wa muda mrefu nachelea kuwa wanaotaka muungano wa serikali ya mkataba au tatu hawataki muungano. Kwanini nasema hilo:-
a. Muungano wa mkataba huja kwa makubaliano yanayotaka kila mjumbe wa nchi husika awe amesurrender baadhi mamlaka waliyonayo kwa serikali ya muungano. Muungano wa nchi ambazo hazitaki kuruhusu baadhi ya mamlaka kuwa katika serikali ya muungano ni muungano mfu.

b. Muungano unataka mchango wa kila mjumbe wa muungano. Sasa kama mshirika mmoja wa muungano anasema hana hela ya kuchangia katika muungano je serikali ya muungano itaendeshwa na nani?

Kwa ufupi hakuna muungano ndani ya serikali 3 wala mkataba. Ni vema wavunje muungano au wakubali muungano wa serikali moja biashara iishe.
 
Muundo wa sasa siyo Serikali mbili kwa kumaanisha kila mshirika na serikali yake. Kuna Serikali yao na yetu. Mshirika mmoja ni mwenye yake na yetu wakati mwingine ni mwenye yetu tu. Huu siyo Muungano bali ni kiinimacho cha muungano. Kwa lugha hiyo na uhalisia Muungano wa sasa ni wa Serikali moja, ya Jamhuri, ndiyo inayounganisha Bara na Visiwani. Serikali ya Zanzibar siyo ya Muungano. Kinachogombewa ni au Bara nao waunde yao na hapo hapo waendelee kutawaliwa na Muungano (Serikali ya Jamhuri) au Zanzibar Wauwe Serikali yao (kama ambavyo walishafanya Bara tangu enzi) wabaki na Serikali moja (ya Muungano). Ni Zanzibar ndiyo wana Serikali mbili, si Bara.
 
SOMA HII SENTENSI HALAFU NYAMBULISHA BADALA YA 'YA' IWE 'WA' 'JAMHURI YA MUUNGANO YA(WA) TANZANIA,halafu niambie nani anaibiwa hapo,tuwaachie wanzanzibar jamani taifa lao tusiwagande kama ruba
 
Back
Top Bottom