Maoni juu ya rasimu ya katiba,tufikishieni kwenye mabaraza ya katiba mambo haya

Maoni juu ya rasimu ya katiba,tufikishieni kwenye mabaraza ya katiba mambo haya

MMASSY

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2011
Posts
290
Reaction score
196
SURA YA NNE Ibara ya 39 kifungu kidogo cha 3 yaani ib 39.(3).Inatamka kuwa "Raia wa Jamhuri Muungano hatapelekwa katika nchi ya nje yoyote kujibu mashtaka au kufanyiwa mahojiano ya aina yoyote kinyume cha ridhaa yake".Kifungu hiki hakitakuwa na mantiki katika katiba yetu kwa sababu zifauatazo i. Katika rasimu hii ,ibara ya 12 inaeleza kuhusu sera ya mambo ya nje na mwelekeo wa sera za nje za taifa huku ikisisitiza Tanzania itakuwa mastari wa mbele kupambana na makosa ya kimataifa ya kijamii angalia ibara ya 12(g).

Kwa kuwa Tanzania imeridhia mikataba ya kimataifa kuhusiana na hakiza binadamu,za kisiasa na za kijamii,na kwa kuwa Tanzania ni mwanachama wa Umoja na taifa pamoja na vyombo vingine vya kimataifa,si vyema na wala haitakuwa busara kulinda raia wake kukamatwa,kuhojiwa na hata kujibu mashtaka nje ya nchi kwa kuwa kufanya hivi kutakuwa kunakikua mikataba hii ambayo taifa limeirdhia na kuidhinsha.Kwa mfano,Tanzania ni mwanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya ICC iliyopo the Hague-Uholanzi.Ikitokea raia wake anatakiwa kushitakiwa katika mahakama hii kwa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu,Katiba yetu itakuwa inamlinda na kwa hivyo itakuwa inakinzana na sheria za kimataifa na pia kama rasimu hii ikipita kama ilivyo,kutakuwa na kujikanyaga kwa katiba kwa kuwa Ibara za 12(g)na hii ya 39(3) kitu ambacho kisheria kinaleta utata mkubwa kimantiki na hata kiutekelezaji.

Ikumbukwe kuwa Watanzania ni sehemu muhimu ya jamii ya kimataifa na kwa hivyo nao wanatenda makosa kama raia wan chi nyinginezo,kwa hiyo,hakuna haja ya kuwawekea kinga kwa kuwa tutakuwa tunasaliti juhudi za dunia za kupambana na uhalifu.Kwa mfano katika tukio la kulipuliwa ubalozi wa Marekani hapa Tanzania mwaka 1998,Mtanzania mmoja tayari amefungwa kule Marekani kwa tukio hilo.Je kama tungekuwa na katiba inayotamka hili linalotamkwa katika rasimu hii hatuoni kama tungekuwa tunalinda uhalifu?.

Kuna biashara haramu zinafanyika kote ulimwenguni na Watanzania ni wahusika pia,je kama kifungu hiki kikipita si kitachochea biashara ya uhalifu ambayo Tanzania kupitia kuridhia mikataba mbalimbali ya dunia imesaini kukabiliana nayo kwa ushirikiano na nchi nyinginezo?

Sikubalianai na hoja kwamba makosa yaliyofanywa na Mtanzania akiwa nje ya nchi ama hapa nchini anatakiwa kushitakiwa tu hapa nchini kwa kuwa kutokana na wadhifa wake ama nguvu zake kwenye vyombo vya haki nchini anaweza kupendelewa.

Nashauri na kupendekeza kuwa kama Mtanzania amevunja sheria popote pale duniani akamatwe mara moja na kukabidhiwa katika vyombo vya ngazi husika mara moja nah ii itasaidia sana pia kuheshimiana na mataifa mengine duniani.Mikataba yote iliyoridhiwa na Tanzania ina nguvu kisheria na kwa hiyo kama rasimu hii ikipita na kuwa katiba tayari itakuwa inakizana kwa ukali sana na sheria za kimataifa na mikataba mbali mbali ya kimataifa.

Pia ni vizuri kuelewa kuwa sheria ni msumeno na kila mtu yuko chini ya sheria,rasimu kutamka kuwa raia wa Jamhuri hatapelekwa nchi nyingine pale anapofanya kosa kinyume na ridhaa yake,ni sawa na kusema kuwa raia yeyote katika Jamhuri anatakiwa atoe ridhaa yake ndio ashitakiwe kitu ambacho hakipo sehemu yoyote na wala katika mfumo wowote wa sheria duniani.

Ni vizuri tukatazama vizuri sehemu hii na kuondoa kifungu hiki kwa kuwa hakina maslahi kwa taifa wala dunia na badala yake kimejaa maslahi binafsi ya washukiwa wa uhalifu na kukinzana na sheria zetu zenyewe na hata sheria za kimataifa.
Nitaendelea kuweka uchambuzi kadiri ninavyomaliza.Kimsingi ninazungumzia kwanza yale yanayohitaji marekebisho japo nimeikubali rasimu hii kwa 95%

Karibuni
 
UPDATES

SEHEMU YA SITA
MUUNDO WA SERIKALI YA MUUNGANO
Ibara ya 57(1a-c) na (2a-c).Inazungumzia kuwa Tanzania kutakuwa na serikali tatu(3)yaani ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Tanzania Bara.Hili ni wazo zuri sana na kwa kuwa haya ni maoni ya wananchi wengi na tangia siki nyingi,ni vizuri kifungu hiki kikabaki kama kilivyo kwa kuwa ndio njia sahihi na pekee ya kuendelea kuwa na Muungano hasa kwa mazingira haya ya utandawazi.
Ni kwanini tuwe na serikali tatu?
i. Uhuru zaidi kwa serikali za Tanganyika na Zanzibar.Kumekuwa na msuguano wa kimaneno na hata mara nyingine kuibuka nguvu katika suala la kutetea ZANZIBAR kuwa na mamlaka kamili na yote haya yalitokea Zanzibar kwa idadi ya wananchi kutaka kuwa na serikali yao yenye mamlaka.Kuwa na serikali za Tanganyika na ile ya Zanzibar kutawezesha serikali husika kufanya mambo yake kwa uhuru zaidi isipokuwa maswala yale ya Muungano ambayo pia yameainishwa katika Rasimu hii.Kwa kuwa kila upande utakuwa na serikali yake,Mahakama zake na hata Bunge lake,itawezesha nchi husika kuweza kuendesha mambo yake kwa uhuru zaidi na kuyaacha yale yaliyo ya Muungano tu ndio yashughulikiwe na mawaziri wa Muungano.Hili limefanyika katika nchi za wetu kama Marekani na Muungano wao umedumu bila manung'uniko kwa miongo kadhaa nab ado upo imara.
ii. Usimamiaji mzuri na mgawanyo wa Rasilimali za umma.Kwa sasa kuna maswala yanayogombaniwa japo kwa maneno katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusiana na rasilimali za taifa.Baadhi ya wananchi wa Zanzibar wamesikika wakilalamika kwamba wananyonywa katika ugawaji wa keki ya taifa,kuna pia baadhi ya maswala kama Gesi na mafuta yana mvutano kama yawe ya Muungano au la.Katika mazingira na kwa kuwa kila upande utakuwa unasimamia rasilimali zake,ni vyema sasa kwa Rasimu hii kutokanusha uwepo wa serikali hizi tatu ili kutoa fursa kwa kila upande katika Muungano kusimamia ipasavyo rasilimali zao na kuwaletea wananchi maendeleo na kuyaacha tu yale ya Muungano ndiyo yashughulikiwe na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
iii. Kuna hoja zinatolewa pia kuwa kuwa na serikali tatu ni gharama kuziendesha.Kitu ambacho wakosoaji wanshindwa kukianisiha mpaka sasa ni gharama halisi zitakuwa za kuendesha serikali hizo.Wameshindwa kueleza namna serikali hizi zitakuwa na gharama kuziendesha kwa kuwa kuna ukweli kwamba kuwa na serikali ghali ama nafuu inategemea katiba yenyewe inavyosimamia rasilimali za wananchi na namna inavyowabana viongozi waandamizi wa hizi serikali kutokuwa wabadhirifu na kuendesha serikali kwa anasa.Kwa sasa taifa linasumbuliwa na gharama kubwa za uendeshaji wa serikali japo tuna serikali moja tu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ndogo ya Zanzibar.Kwa nchi za wenzetu kama ile ya Marekani inayoongozwa na majimbo makubwa kuliko hata Tanzania 53,kila jimbo linajiendesha lenyewe isipokuwa tu kuna serikali ya Shirikisho(Federal Government anayoongoza Barack Obama ambayo kwa mujibu wa katiba ya Marekani Ibara ya 1(8) inaiwekea serikali ya shirikisho mipaka mikali ya utendaji wa serikali katika matumizi ya fedha za umma katika maswala kama vile Ulinzi wa taifa,mfumo wa mahakama,ujenzi wa barabara,ofisi za posta na kulipa kodi ya taifa.Wenzetu wameiwekea serikali ya Shirikisho mipaka ya matumizi ya fedha ili kuacha mwanya kwa serikali za majimbo 53 uhuru wa kusimamia vizuri maendeleo yao.Hili limefanikiwa sana katika historia ya taifa la marekani kwa kuwa wao hawakutazama uendeshaji wa serikali kama ni gharama kubwa kwa sheria madhubuti walizojiwekea bali walitazama gharama za kulinda muungano.Sisi pia tunaweza kuzuia matumizi makubwa ya serikali hizi kwa kuziwekea mipaka ya madaraka na matumizi ya fedha za walipa kodi.Kuendesha serikali kwa gharama kubwa ama ndogo ni utamaduni tu ambao umezoeleka na tunaweza kama Watanzania kuukataa na fedha au rasilimali nyinginezo za nchi zikatumika kwa maendeleo ya wananchi.
iv. Umoja na ushirikiano;ni ukweli usiopingika kuwa hata wanaopinga serikali tatu wanatambua kwa mazingira ya sasa kuna kundi moja linanyimwa haki zake ama la Zanzibara ama la Tanganyika.Hii ni kwa kuwa unapokuwa na serikali ya Zanzibar na ile ya Jamhuri manake ni kwamba hawa Watanganyika wao hawana serikali ama unaitumia hii serikali ya Jamhuri ya Muungano kama serikali ya Tanganyika kitu ambacho pia kitakuwa si haki kwa Wazanzibari.Kimsingi kwa mfumo ulipo sasa ni kwamba serikali ya Jamhuri inafanya majukumu ya Muungano na yale ya Zanzibar kitu ambacho kimejengea watu wa Zanzibar taswira kwamba wanaamuliwa mambo yao na watu wa Tanganyika(Wabara).Kwa mazingira haya,tunapaswa kuwa na serikali tatu kama rasimu inavyopendekeza ili kuwe na serikali mbili za pande zote mbili za muungano na serikali moja kuu ya Muungano ambayo itakuwa ndiyo serikali kuu(mama).Likipitishwa hili basi tutakuwa na Muungano imara kuliko sasa kwa kuwa kila upande utakuwa na serikali yake lakini kuna serikali moja kuu ambayo itapatanisha pia serikali za washirika pale wakigombana.Kwa muundo wa sasa ukitokea ugomvi kati ya Zanzibar na Bara ni ngumu kuumaliza kwa kuwa kuna mlalamikaji mmoja ambaye ni Zanzibar halafu kuna mwamuzi na mlalamikiwa ambaye ni serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Tumeona siku zote Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo kimsingi inahusika kutatua kero za muungano,miaka mingi imeshindwa kutatua na kumaliza kero za muungano kutokana na aina ya muungano tulionao.
 
Back
Top Bottom