Omary 1998
New Member
- Jun 20, 2024
- 3
- 3
MAONI JUU YA SERA YA "KATA MTI PANDA MTI"
Serikali ya Tanzania ilianzisha sera yenye kauli mbiu ya KATA MTI PANDA MTI kwa lengo la kuzuia ukataji wa miti hovyo ili kuweza kupambana na mabadiliko mbali mbali ya tabia ya nchi yanayoweza kujitokeza .
NINI MCHANGO WA SERA HII ?
Kwa upande wangu naona sera hii Bado ina mchango mdogo Sana katika kupambana na janga la upotevu wa misitu Katika taifaletu la Tanzania. Hali inayopelekea kuzidi kuendelea Kwa uharibifu wa misitu ukilinganisha na idadi ya miti inayopandwa na hatimae imepelekea maeneo mengi yakibaki kuwa meupe pabila miti Hali inayohatarisha katika kizazi hichi na kijacho kutokana na majanga ya mabadiliko ya tabia ya nchi.
NINI MADHAIFU YA SERA HII ?
Mapungufu makubwa ya Sera hii ynatokana na namna sera hii ilivyoegemezwa zaidi ambapo utaona kua wanaotambulika zaidi kama vinara wakubwa wa uharibifu wa misitu.katika taifa letu ni wachana mbao , wachoma mkaa, na wakulima Hali imeyopelekea mamlaka za misitu kuchukua hatua madhubuti juu ya makundi haya haya tu. Hali imeyopelekea miongoni mwa watu kuhukumiwa vifungo na hata kutozwa faini Kwa kosa la uharibifu wa misitu.
NINI MTAZAMO WANGU ?.
Kwa upande wangu naona kua pamoja na kua makundi haya ya wakulima , wachana mbao na wachoma mkaa ni miongoni mwa waharibifu wa misitu katika taifa letu.
Ila serikali inapaswa kutambua kua wizara za serikali, makampuni na taasisi mbali mbali Hawa ndo vinara wakubwa katika uharibifu wa misitu katika taifa letu.
Makundi haya yamekua yakipelekea upotevu wa mamilioni ya miti pindi wanapoanzisha miradi mbali mbali ya maendeleo katika maeneo mbali mbali hapa nchini kama vile ujenzi wa viwanda , bara bara , reli, shule , vituo vya afya nk. Ambapo utaona kua miti yote iliyoko katika maeneo ya mradi huangushwa . Hivyo ni wazi kua makundi haya ni wana mchango mkubwa Sana katika upotevu wa miti katika nchi yetu Kwa mifano mbali mbali kama ifuatavyo;
(a). Unakuta mkulima anakata miti 20 ili apande ekari la mahindi ila unakuta wizara ya ujenzi imejenga barabara kama 200KM ambayo inapelekea upotevu wa miti kama laki Tano (500,000) je nani hapo muharibifu zaidi ?
(b) Unakuta mkata mkaa kaangusha miti 2 ili achome mkaa ila wizara ya ardhi imeuza zaidi ya ekari 20 ambapo wateja wake huangusha miti yote ili wajenge je nani hapo muharibifu zaidi?
(c). Unakuta mchana mbao kakata miti kama 10 ili achane mbao ila unakuta wizara ya wiwanda imejenga kiwanda ukubwa wa zaidi ya ekari 20 ambapo Mamia ya miti iliyopo yote huangushwa , je nani muharibifu zaidi?
Hivyo basi Kwa kutumia mifano hii michache utagundua kua makundi haya ni yenye kupoteza miti mingi Sana ukilinganisha na idadi ya miti inayopandwa katika taifa letu .
NINI KIFANYIKE KUTATUA TATIZO HILI ?
Kwa upande wangu napenda kutoa mapendekezo Kwa mamlaka ya misitu nchini ianzishe sera madhubuti ambayo sera hii iwe ni yenye kauli mbiu ya LIPIA MTI, KATA MTI, PANDA MTI ambapo sera hii yapasa iwe ni e ndelevu katika taifa letu.
JE, MAMLAKA ZIFANYEJE BAADA YA KUUNDWA SERA HII ?.
Baada ya kuundwa sera hii mamlaka ya misitu nchini Kwa kushirikiana na mamlaka zingine ziweze kufanya maboresho katika usimamizi na ulindaji wa misitu katika taifa letu ambapo maboresho yafuatayo yanaweza kufanyika ;
(a). Mradi wowote uwe wa serikali au sio serikali kabla ya kuanza ujenzi wake mamlaka ya misitu iwe inafanya tathmini ya idadi ya miti yote itakayopitiwa na mradi katika eneo husika .
(b). Baada ya kufahamu idadi ya miti yote itakayopitiwa na mradi basi wamiliki wa mradi huo wawe wanalipa fidia ya miti yote iliopo katika eneo Hilo la mradi mfano mamlaka inaweza kuweka Kila mti Tsh 2000/=
JE MAMLAKA ZIFANYEJE BAADA YA KULIPWA FIDIA ?.
Baada ya mamlaka kupata pesa hiyo ya fidia mamlaka ya misitu Kwa kushirikiana na mamlaka zingine ni vizuri zitafute maeneo yote yaliyokumbwa na uharibifu wa misitu kama vile milima, pembezoni mwa mito na sehemu mbali mbali ambazo hazifanyiwi shughuli za binadamu.
Baada ya kupata maeneo hayo basi Kila kipindi Cha mvua mamlaka inaweza kua inatangaza Kwa wananchi au taasisi mbali mbali vibarua vya upandaji wa miti katika maeneo mbali mbali ncini ili kufidia miti iliyokatwa kutokana na ujenzi wa miradi mbali mbali ncini, mfano wanaweza Sena Kila mti utakaopandwa na kushika malipo ni Tsh 500 au 1000 naimani itachochea upandaji wa miti mingi Sana Sana katika nchi yetu.
Kipindi Cha upandaji wa miti hii ni vizuri iwe inatengwa wiki maalumu Kwa Kila mwaka na iwe msimu wa mvua ambayo wiki hiyo inaweza kuitwa TANZANIA REFORESTATION SEASON (TRS) nchi mzima itakua ikitenga mida huu kulingana na Hali ya hewa ya mkoa na wilaya husika .
JE, NAMNA GANI SERA HII INAWEZA KUTEKELEZWA ?.
Ili sera hii iweze kutekelezwa inapaswa serikali ifanye yafuatayo;
(a). Kukutanisha mamlaka zote nchini na kukubaliana juu ya mabadiliko haya ili Kila kundi like tayari kushiriki ipasavyo Kwa lengo la kuleta mapinduzi ya mazingura katika taifa letu.
(b). Mamlaka ya misitu ipewe nguvu ya kuweza kutoruhusu ujenzi wa mradi wowote Hadi itakapolipwa fidia ya miti yote iliyoko katika eneo ambalo mradi unatarajia kupitia.
(c). Mamlaka ya misitu iwe inatoa hati ya uanzaji wa mradi wowote Kwa mmiliki wa mradi ikiwa atakua kalipa fidia.
(d). Miti yote iliyoko nchini iangaliwe Kwa jicho la ulinzi zaidi ili kuhakikisha inaweza kua ni yenye kudumu .
NINI FAIDA YA MABORESHO HAYA ?
(a). Maboresho haya yatasaidia upandaji wa miti mingi Sana ndani ya mwaka Hali itakayochochea kiweze kurudisha maeneo mbali mbali ambayo yalikwisha athirika zaidi katika Hali yake ya asili kama vile milimani, na pembezoni mwa miti.
(b). Maboresho haya yatachangia utengenezaji wa ajira nyingi Sana Kwa wasomi na wasiokuwa wasomi mfano watengeza vitaru vya miti pamoja na wapandaji wa miti hiyo .
(c). Pia maboresho haya yatachochea nidham ya misitu mana naimani ukataji wa miti utapungua ili kukwepa fidia hii.

Upvote
3