Maoni kutoka kijiwe cha msafisha viatu: Watanzania wengi hawapendi Mabadiliko, wanangoja Magufuli aondoke

Naona wasema wakati wa Mkapa mambo yalikuwa nafuu akaja JK akaharibu.

Hivyo JPM hawezi kulaumiwa kwa hitilafu za miaka 10 kabla yake.
Acha kulinganisha aliyeijenga nchi nzima bila ubaguzi mwingine kajenga Kijiji chake na labda dar pekeee kupitia Kodi za nchi nzima
 
Mimi sina maslahi na magufuli ila naeleza nilichokiona na nachoendelea kukiona.

Sina tatizo na unachokiona, lakini utetezi wako kwa Magufuli vs JK sio wakweli, bali wote ni sawa, bali wanatengenishwa na hulka na mapungufu binafsi. Ila uwajibikaji kimfumo hakuna mwenye afadhali kwa mantiki ya ubora. Kama ni alama, basi mmoja ana C+, na mwingine b-, lakini sio B kwenda mbele.
 
Tatizo ni kwamba, Magufuli hana clear thinking.

Hana political education wala philosophy kama aliyokuwa nayo Nyerere.

Matokeo yake anataka kuwapandishia wakulima wa korosho bei ya korosho kwa command, kwa kutumia jeshi.

Matokeo yake wakulima wa korosho wanalia mpaka leo.

Serikali kuingilia biashara ya korosho kulifuatiwa na mapato ya fedha za kigeni zinazotokana na bidhaa za kilimo kushuka kwa 55% mwaka uliofuatia. Ripoti ya BOT ya September 2019 imebainisha hilo.

Uchumi hauendeshwi kwa maguvu na vitisho.

Nyerere na Sokoine walijaribu wakashindwa.

Magufuli hakujifunza kitu hapo?
 
Jamaa kaandika Sanaa Mambo mengi....

Huyu Jaman anastahili kupewa hata like 💯
 
"Watanzania tulizoea maisha ya kupata bila jasho hivyo sasa twafunzwa kutafuta kwa jasho twaona taabu na shida kubwa"

Nime mnukuu huyu jamaa hapo juu....

Hiyo kauli huwaga si ielewagi ........wanao ielewa wanifafanulie......
 
"....viongozi wengi hawana nia ya kweli ya kumsaidia huyu mzee. Wao wanangojea aondoke kwa matarajio kwamba raisi ajae atakuwa si kama huyu mwamba"
 
Rais ambaye anashindwa kufikisha ujumbe vizuri kwa wasaidizi wake, mpaka akahitaji mkalimani wa kutafsiri anachosema kama yeye katoka nchi nyingine na hajui lugha yetu, ameshindwa kazi rahisi kabisa ya rais, mawasiliano.

Sitegemei aweze kazi nyingine ngumu zaidi.
 
Kazi ya Rais sio mawasiliano,

Kazi yake ni kutoa maagizo tu,

Ni jambo la kawaida kabisa kwa baadhi ya watu kushindwa kumsoma mtu kwa uharaka na kumuelewa anataka nini

Hata huko madarasani sio wote wanaomwelewa mwalimu kwa uwezo wa Kupata A , inatokea anayepata F ingawa mwalimu ni yule yule, hapo huwezi sema kuwa Mwalimu kashindwa kufikisha ujumbe kwakua wapo waliopata F.

Sasa ili huyo wa F Naye aongeze ufaulu anahitaji muda wa zaida, linakuja swala la tuition.

Same applies kwamba kuna baadhi ya watendaji hawajafanikiwa kuelewa filosofia ya kiongozi wao jambo linalopelekea kufanya mambo kinyume na matarajio. Hawa wanahitaji ufafanuzi wa ziada, rejea mfano wa tuition.
 
Ukisema kazi ya rais si mawasiliano, ni kutoa maagizo, hapo kama hujaelewa maagizo ni mawasiliano naweza kuelewa kwa nini Tanzania tuna shida kwenye mawasiliano kuanzia huyo rais mpaka wewe mwananchi.

Pia, kama hujaelewa hitubabanazotoa rais ni mawasiliano hilo ni janga lingine.

Zaidi, kama hujaelewa kwamba rais si mtu wa kutoa maagizo tu, naye anatakiwa asikilize maoni ya wananchi, na kufanya hivyo ni mawasiliqno na wananchi, hilo ni janga lingine la kuleta taharuki.

Ongezeo, kama rais mwenyewe hajui anarudi au anaenda, yuko kushoto au kulia, anawayqwaya tu kama bendera kufuata upepo wa nuda huo, hakuna mtendajibatakayemuelewa na hata yeye mwenyewe hatajielewa.

Magufuli anawayawaya tu. Hajui anataka nini na atapataje anachotaka

Mfano.Anajisema rais wa wanyonge, lakini matumizi yake ya hela nyingi kununua midege ambayo hao wanyonge hawawezi kupanda haioneshi hilo. Tena kanunua kibabe bila ooen tender wala ukaguzi wa mahesabu.

Mfano nwingine. Magufuli kuingilia biashara ya korosho kibabe iki apandishe bei ya korosho kwa wakulima kume backfire na wakulima wa korosho waneumia vibayabsana. Kwa nini? Kwa sababu rais wao kavamia suala hili kwa pupa bila mpango.

Magufuli kajaa pupa, hana mpango wa kueleweka.

Mtu kama huyo hata yeye mwenyewe hajielewi anataka nini na anachokitaka atapataje. Anakwenda kwa "reflex action" tu.Sasa hao wasaidizi wake watamueleea vipi?
 
Angalia tu isijekuwa wewe ndio hauelewi ukawa unapotosha na kuzua taharuki.

Kuna tofauti Kati ya mawasiliano na kutoa maagizo (amri).
 
Angalia tu isijekuwa wewe ndio hauelewi ukawa unapotosha na kuzua taharuki.

Kuna tofauti Kati ya mawasiliano na kutoa maagizo (amri).
Unavyowaza ni moja ya sababu Tanzania ina watu masikini wengi.

Rais ni kijakazi wa wananchi. Anatakiwa kujieleza kwa wananchi wananchi wamuelewe.

Hawezi kufanya hivyo bila kuwasiliana na wananchi.

Ndiyo maana marais waliopita kina Kikwete na Mkapa walikuwa wanafanya hotuba za kila mara. Kila mwezi mara nyingine. Walijua umuhimu wa kuwasiliana moja kwa moja na wananchi.

Mwinyi ndiyo kabisaa, alikuwa anakutana na wananchi moja kwa moja Lumumba anawasiliana nao.

Wewe unamfanya rais kuwa kama mfalme wa kizamani anayetoa amri tu.

Hata Wafalme siku hizi hawatoi amri tu.
 
Donald Trump ndiye aliwashawishi watu waandamane, huku akiwaita ni watu mhimu sana. Siku hii ya jana katika hotuba yake anasisitiza kuwa Marekani inaendeshwa kwa mujibu wa sheria na Katiba, na watu wote waliofanya maandamano na kusababisha MADHARA watachukuliwa HATUA


Trump akili zake sometime kama za Bashiru wa ccm
 
Umebarikiwa kwa Majungu mkuu Hongera sana
 
Katika marais walioiharibu nchi ni magu...
Ameshindwa kuifanya serikali iwe inapelekewa kodi na wafanyabiashara matokeo yake serikali ndio inafuata kodi.

Moja ya eneo ambalo anafanya kosa kubwa sana ni kujenga uadui na wafanyabiashara huku akijua ndio sekta muhimu sana kwa taifa, kila siku anabuni mbinu za kuinyonya badala kuisaidia izidi kukua
Mfano sasa hivi wametakiwa kuweka barcord kwenye risiti za mashine ya EFD na gharama yake ni laki na nusu si wizi kabisa huu?

Umezungumza habari ya wamachinga, hawa wapo kwa kazi rasmi ya kuua wafanyabiashara wakubwa na ni mpango mkakati maalumu na wala usitarajie waondolewe awamu hii,
Ndio maana wao hawalipi kodi zaidi ya kitambulisho tu haijalishi ana mtaji mkubwa kiasi gani, wala hawatakiwi kutoa risiti wakati sheria inasema risiti inatolewa kuanzia bidhaa ya sh 500,

Akikamatwa mwenye duka hajatoa risiti hata ya 1000 faini milioni 3 mmachinga hata auze bidhaa ya laki haina shida,

Mwenye duka analipa kodi lukuki
1)kodi ya mapato,
2)leseni ya biashara,
3)huduma ya jiji (service leavy)
4)mkataba wa frem au stoo nao unalipiwa kodi.
5)fire extingisher
6)huduma za taka
7)kodi ya frem na stoo kama anayo
Mmachinga hapo analipa elfu 20 kamaliza kazi.
Biashara za maduka nchini zimedorora sana, yaani mfanyabiashara serikali hii anadharauliwa sana hasikilizwi tena yaani kifupi ni adui wa serikali.

Ukiona tawi ya benk kubwa kama NMB kkoo senta tangu lifunguliwe 2012 wanatoa huduma hadi siku za jumapili lakini sasa hivi hawafungui ujue kuna shida pamoja maduka ya kuabadili fedha kufungwa watu wanabadilisha bank lkn bank zinafungwa,
Ukiona bank zinafunga matawi yao katikati ya mji kama kkoo ujue ipo shida mahali tena kubwa sana.

Kuna mengi ya unyanyasaji wa wafanyabiashara tunayajua lakini siwezi kuyaandika hapa sababu sasa hivi jf ni kama fb haina uhuru tena nisije kupelekwa kusikojulikana.

Kwa mkakati wake huu wala hatushangai maana alishasema mapemaaa "WAFANYABIASHARA NA MATAJIRI WATAISHI KAMA MASHETANI"

Kwa hiyo kwa mfumo huu ni kusubiri tu atoke madarakani hakuna namna, mfumo wake wa kiuongozi hauzoeleki wala haiwezekani kwenda nae sawa ndio maana hata viongozi wenzake wanamuogopa sio kumuheshimu.
 
Alieharibu nchi kwa 80%ni mkapa huo ndio ukweli usiosemwa na wengi.
 
Mjumbe Dock upo Dar es Salaam "kikazi"? Kazi gani hiyo Brooks? Uko Dar es Salaam, umetokea wapi? Kazi yako huko wapi ni nini? Unamtafuta mshona viatu City centre na kariakoo na gongo la mboto, ndiyo kazi yenyewekutupa sera za mshona viatu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…