Maoni na Ushauri kuhusu Biashara ya Maji Kigamboni

FAJES

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2017
Posts
720
Reaction score
644
Wakuu, heshima kwenu.

Kutokana na changamoto ya upatikani wa maji yasiyokuwa na chumvi Kigamboni nimeona hii ni fursa ya biashara.

Wazo langu:
Ni kununua SIMTANK yenye capacity kuanzia 5000 liters kisha kulisimika mahali ambapo wateja watanunua kwa bei kati ya Tshs 250 -300 @ ndoo ya lita 20. Kwa sasa watu wananunua kupitia jamaa wa mikokoteni kwa bei kati ya Tshs 500 -300. Sehemu ya kutolea Maji ni maeneo ya Kigamboni Kisiwani. Bei ya kununulia ndoo ya lita 20 ni Tshs. 50.

Ili kifanikisha mradi huu, nitalipa kodi ya eneo la kusimika SIMTANK, kumpa ujira kijana atakayesimamia kazi hiyo, kulipia gharama za usafirishaji wa maji hayo kupitia kukodi Gari itakayokuwa inaleta maji hayo.

Wakuu, naombeni mwenye ushauri au mawazo tofauti juu ya wazo hili la biashara.
 
Serikali itakuita mlanguzi wa maji la sivyo uwauzie bei ya huduma ndoo kubwa lita 20 kwa sh. 50
 
Serikali itakuita mlanguzi wa maji la sivyo uwauzie bei ya huduma ndoo kubwa lita 20 kwa sh. 50
Mkuu, mbona hawa jamaa wa Mikokoteni, Punda na Bajaji hawajaitwa Walanguzi.? Je, kuna misingi yoyote ya kisheria juu ya jambo hili? Kama ipo misingi ya kisheria hakuna budi kutii.
 
Wakati wewe ukiwa unasubiri ushauri, kuna mmoja huko ameshapata idea kupitia thread hii na anaandaa mikakati ya kuanzisha. We jitose mkuu, maji watu lazima wanunue tu hata hali iwe ngumu kiasi gani
 
tatizo la kigamboni vikifungwa vyuo vya mwal nyerere,Ifm,cbe,dit,dmi, na magogoni hamna biashara inayoenda utaishia kupiga miayo plus mfungo Wa ramadhani
 
Wakati wewe ukiwa unasubiri ushauri, kuna mmoja huko ameshapata idea kupitia thread hii na anaandaa mikakati ya kuanzisha. We jitose mkuu, maji watu lazima wanunue tu hata hali iwe ngumu kiasi gani
Mkuu, hata kama kuna mtu atalichukuwa hili wazo na kulitumia bado ni njema tu. Nadhani ndio maana halisi ya Jukwaa hili. Hata hivyo, riziki kila mtu kapangiwa kulingana na mtu mwenyewe. Hata kama tutafanya kitu kimoja tukiwa wawili, bado ile sehemu ambayo ni riziki yangu haiwezi kubadilika.
 
tatizo la kigamboni vikifungwa vyuo vya mwal nyerere,Ifm,cbe,dit,dmi, na magogoni hamna biashara inayoenda utaishia kupiga miayo plus mfungo Wa ramadhani
Mkuu, naona mchango wako ni wa thamani sana. Muhimu hapa ni kuwa na strategic plan kulingana na soko lenyewe. Kuwa mauzo makubwa yawe targeted wakati wanachuo wakiwepo. Wakiondoka, ni muda pia wa kubuni wazo lingine tofauti.
 
you're right
 
Wazo zuri Sana na ukitolea temeke no karibu kuliko ubungo.
Piga vizuri hesabu zako za Usafiri.
 
Wazo zuri Sana na ukitolea temeke no karibu kuliko ubungo.
Piga vizuri hesabu zako za Usafiri.
Mkuu, sijakupata vizuri. Mie nilisema plan ni kutolea Kigamboni Kisiwani ila siyo Ubungo.
 
Mkuu, sijakupata vizuri. Mie nilisema plan ni kutolea Kigamboni Kisiwani ila siyo Ubungo.
Basi karekebishe, Ila fuatilia mipango ya serikali kuhusu vile visima Vya MAJI somangira.
 
Basi karekebishe, Ila fuatilia mipango ya serikali kuhusu vile visima Vya MAJI somangira.
Nashukuru sana Mkuu. Tayari nimerekebisha. Naomba pia ushauri wako. Zaidi kama unafahamu chochote kuhusu mpango huo wa Serikali juu ya Visima vya maji Somangira..
 
tatizo la kigamboni vikifungwa vyuo vya mwal nyerere,Ifm,cbe,dit,dmi, na magogoni hamna biashara inayoenda utaishia kupiga miayo plus mfungo Wa ramadhani
Kwa akili ya kawaida unategemea hivi vyuo vitafungwa? Kwasababu gani? Unajua vilianzishwa lini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…