Godlisten9
Member
- Jul 14, 2021
- 7
- 5
MAJANGA YA MOTO
Asalaam aleikyum, Bwana Yesu asifiwe, Tumsifu Yesu kristo wadau wa JF, ahsanteni wadau, jukwaa na uongozi wa Jamii Forum nimeona nilete mjadala huu mbele yenu kwakuwa ndio tatizo kubwa linaloikumba hii nchi na kuleta madhara makubwa kimaendeleo, katika nyanja zote ikiwemo afya ya binadamu, uchumi, siasa, na hata kijamii
Nakukaribisha kutoa maoni yako na ushauri na nyongeza yoyote ile ahsanteni na msichoke kusoma.
Mwanzo
Moto ni moja ya nishati kuu tumizi na yenye faida katika ulimwengu ni chanzo cha joto na husababishwa na kuungua kwa mafuta ama fueli.
Kuendana na shughuli mbalimbali za maendeleo ya binadamu, kuna umuhimu wa kuwa na elimu juu ya usalama wa moto na namna ya kukabiliana nao mara tu unapotokea kwa kuwa moto husababisha upotevu wa maisha,ulemavu na uharibifu mkubwa wa mali na hata kusababisha watu kuishi katika hali kubwa ya umaskini.
Katika miaka ya hivi karibuni kumeripotiwa majanga ya moto katika maeneo mbalimbali ya duniani na ya nchi yetu tanzania ambapo vyanzo vingi vya moto huo havijagundulika, kama ifuatavyo:
Picha:chanzo BBC.
watalii huenda walipasha vyakula moto na kuacha moto ukisambaa.
Katika mkoa wa morogoro kumewahi kutokea ajali ya lori la mafuta mwaka 2014 na mtu mmoja kufariki.
Mnamo 10/8/2019 ajali ya lori la mafuta ilitokea maeneo ya Msamvu mkoa wa morogoro na kusababisha vifo takriban 104 na majeruhi huku majeruhi wakizidi kufariki kutokana na lori kuungua moto baada ya kupata ajali na kipindi wananchi wanachota mafuta lori likalipuka.
Picha:na millard ayo.
Julai 11 2021 ghorofa mbili za mabweni ya shule ya wasichana ya kiislamu ya AT-TAAUN kuungua
Picha kutoka mtandaoni.
moto hakuna vifo vilivyoripotiwa na chanzo cha moto hakijagundulika.
Moto huo umewaacha wafanyabiashara takribani 225 na kuzidi wakipoteza mali zao, vilevile Serikali ikipoteza kodi pamoja na fursa za biashara
Vyombo na kamati za uchunguzi zilitakiwa kuwepo muda wote sio ziundwe baada ya janga kama waziri mkuu mh. Kassim majaliwa alivofanya katika soko la kariakoo
Na mh Hamis kigwangala alivofanya katika mlima kilimanjaro alipokuwa waziri wa maliasili na utalii.
Picha kutoka firefighting twitter.
Picha kutoka facebook.
ziwekwe kwenye mabarabara haswa barabara kuu ya kuingia katika soko na malango makuu ya kuingilia au eneo lolote la biashara au lenye msongamano.
MATOKEO/RESULTS
UCHUMI NA MAENDELEO YA JAMII
Pato la taifa litaongezeka kutokana na kuepuka matumizi ya fedha kwa kudili na majanga, ukusanyaji wa kodi hautaingiliwa na majanga kama yalivyotokea katika soko la kariakoo na utalii katika mlima kilimanjaro.
Pato binafsi litaongezeka kwakuwa ajali nyingi huleta umaskini na ulemavu ambao ni tegemezi mfano katika soko la kariakoo wafanyabiashara wamepoteza mali na muda wa kutengeneza fedha, ajali ya lori pale msamvu morogoro imeacha yatima na majeruhi walemavu ambao ni tegemezi.
AFYA
Miti na uoto unapoungua inapunguza mzunguko wa hewa ambao ni muhimu kwa afya ya mwanadamu.
Moshi mkubwa una athari katika afya ya binadamu na viumbe hai, magonjwa ya mapafu kama TB yanaweza kusababishwa na kuungua kwa vitu vya plastiki ama mpira.
Moto huleta ulemavu na maumivu na hata kifo kama ilivyotokea morogoro katika ajali ya lori.
Hivyo kupambana na majanga ya moto ina umuhimu mkubwa katika kuilinda na kuimarisha afya kwa viumbe hai.
SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Mifumo ya kisasa ya kupambana na majanga mfano kuwa na visima na mifumo ya maji ya chini ya ardhi, makoki makubwa barabarani na alamu kwa ajili ya dharura ni mifumo mipya inayoendana na sayansi na teknolojia ya sasa ya nchi zinazoendelea na zinazoendelea.
DEMOKRASIA NA UONGOZI
Kuwajibika kwa viongozi haswa wa majeshi ya zimamoto na viongozi wa wizara husika pale wanapofanya uzembe katika sekta zao hutokana na mifumo ya uongozi wa nchi haswa katiba.
Katiba iliyopo ni ya zamani na imepitia marekebisho mengi ni vyema sasa kuwa na katiba mpya yenye vielelezo vya kuwawajibisha ikiwemo kuwaachisha kazi viongozi wazembe na wasiowajibika.
Ukweli na uwazi katika vyombo vya usalama vinavyofanya uchunguzi miaka na miaka bila kuja na suluhisho na ushahidi wa vyanzo vya majanga.
KWA UJUMLA
Katika mawanda mapana na maslahi ya Taifa katiba mpya inayoweza kuwawajibisha viongozi wabovu pale wanapofanya madudu katika sekta zao itaongeza uwajibikaji na kupunguza ajali na majanga yasiyotarajiwa. Viongozi wasisalie madarakani pale wanapofanya ubadhirifu au kuwa na tuhuma zenye ushahidi na wanadhidi kubaki katika madaraka hayo hii inaumiza wananchi na hivyo hitaji la katiba ni kubwa na la muhimu sana.
Imeandikwa na kuandaliwa na:
Godlisten E. Mwasha

- Moto mkubwa ulishawahi kuripotiwa katika msitu mkubwa zaidi wa amazon uliwaka kwa mda mrefu bila kuzimikana kuharibu mazalia ya viumbe na maliasili ya msitu huo huko amerika ya kusini
Picha:chanzo BBC.
watalii huenda walipasha vyakula moto na kuacha moto ukisambaa.
Katika mkoa wa morogoro kumewahi kutokea ajali ya lori la mafuta mwaka 2014 na mtu mmoja kufariki.
Mnamo 10/8/2019 ajali ya lori la mafuta ilitokea maeneo ya Msamvu mkoa wa morogoro na kusababisha vifo takriban 104 na majeruhi huku majeruhi wakizidi kufariki kutokana na lori kuungua moto baada ya kupata ajali na kipindi wananchi wanachota mafuta lori likalipuka.
Picha:na millard ayo.
Julai 11 2021 ghorofa mbili za mabweni ya shule ya wasichana ya kiislamu ya AT-TAAUN kuungua
Picha kutoka mtandaoni.
moto hakuna vifo vilivyoripotiwa na chanzo cha moto hakijagundulika.
- Moto uliolipuka katika Soko Kuu la Kariakoo 10 julai 2021na kuteketeza mali za wafanyabiashara umeonyesha kuwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini lina changamoto nyingi, ikiwemo ukosefu wa vifaa vya kukabiliana na majanga ya moto na rasilimali watu
Moto huo umewaacha wafanyabiashara takribani 225 na kuzidi wakipoteza mali zao, vilevile Serikali ikipoteza kodi pamoja na fursa za biashara
- Hivi karibuni hadi kufikia tarehe 14. 7.2021 kumekuwa na matukio ya mara kwa mara ya moto katika shule ya sekondari ya Geita. Na kupelekea shule kufungwa kwa muda wa wiki mbili. Ndani ya siku saba matukio yameripotiwa mara tatu.
- Picha kutoka JamiiForums.
- 👉Kumekuwa na visa vingi katika mashule mbalimbali katika hii nchi huku huhuda mbalimbali zikitolewa pamoja na hatua za kisheria kuchukuliwa kwa wanafunzi pamoja na walinzi wa shule hizo. Japo kwa ujumla bado chanzo kikuu cha moto katika shule nyingi za kulala hakijawekwa bayana na vyombo vya uchunguzi na ulinzi.
Vyombo na kamati za uchunguzi zilitakiwa kuwepo muda wote sio ziundwe baada ya janga kama waziri mkuu mh. Kassim majaliwa alivofanya katika soko la kariakoo
Na mh Hamis kigwangala alivofanya katika mlima kilimanjaro alipokuwa waziri wa maliasili na utalii.
- Vituo vikubwa na vidogo vya utalii viwe na vifaa vya kuzimia moto ikiwa ni pamoja na helkopta kwa ajili ya sehemu zisizopitika na magari ya zimamoto kwa sehemu zinazopitika, vifaa hivyo viwe tayari na vikiwa na maji muda wote.
- Kuwepo na soko kubwa na linalotoa huduma bora zinazofanana na hata kuzidi ubora wa soko kuu la kariakoo (wengi walitoa maoni kabla ya soko kuungua) MFANO soko lingehamishiwa BUNJU
- Majengo ya zamani kama soko kuu la kariakoo lingeshafanyiwa marekebisho kwa kuweka mifumo ya kisasa mfano;
- alamu ya moto/fire alarm
- mitungi ya gesi ya kuzima moto na mchanga/working fire extinguishers and sand.
- mifumo ya maji ya chini yaani visima/underground water systems
- jeshi la zima moto linalowajilbika na linalopatikana mda wote bila kuchelewa na vifaa vya kutosha ikiwemo:
nguo za kuzima moto na nguvu kazi ya kutosha
Picha kutoka firefighting twitter.
Picha kutoka firefighting twiter. ComHelkopta za maji/drones na magari ya kuzima moto
Picha kutoka twitter kwa wadau.fire extinguishers na michanga na fire blankets.
- Koki kubwa za maji ya dharura/fire hydrant na visima vilivyofunikwa
Picha kutoka facebook.
ziwekwe kwenye mabarabara haswa barabara kuu ya kuingia katika soko na malango makuu ya kuingilia au eneo lolote la biashara au lenye msongamano.
- Soko au eneo la biashara au eneo lenye msongamano liwe lina nafasi au njia za kutosha kuweza kupita gari la zimamoto.
- Itolewe elimu ya zimamoto na majanga mengine kwa msisitizo mkubwa mashuleni na hata katika taasisi za dini ikiwemo kanisani na misikitini.
- Kuwekwe sera(strong policy) ngumu kuhusu uwepo wa vifaa vya kujikinga na moto karibu maduka na ofisi zote za serikali na binafsi ikiwemo shuleni, kanisani na misikitini, ulazima utiliwe msisitizo na sheria ichkue mkondo wake.
MATOKEO/RESULTS
UCHUMI NA MAENDELEO YA JAMII
Pato la taifa litaongezeka kutokana na kuepuka matumizi ya fedha kwa kudili na majanga, ukusanyaji wa kodi hautaingiliwa na majanga kama yalivyotokea katika soko la kariakoo na utalii katika mlima kilimanjaro.
Pato binafsi litaongezeka kwakuwa ajali nyingi huleta umaskini na ulemavu ambao ni tegemezi mfano katika soko la kariakoo wafanyabiashara wamepoteza mali na muda wa kutengeneza fedha, ajali ya lori pale msamvu morogoro imeacha yatima na majeruhi walemavu ambao ni tegemezi.
AFYA
Miti na uoto unapoungua inapunguza mzunguko wa hewa ambao ni muhimu kwa afya ya mwanadamu.
Moshi mkubwa una athari katika afya ya binadamu na viumbe hai, magonjwa ya mapafu kama TB yanaweza kusababishwa na kuungua kwa vitu vya plastiki ama mpira.
Moto huleta ulemavu na maumivu na hata kifo kama ilivyotokea morogoro katika ajali ya lori.
Hivyo kupambana na majanga ya moto ina umuhimu mkubwa katika kuilinda na kuimarisha afya kwa viumbe hai.
SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Mifumo ya kisasa ya kupambana na majanga mfano kuwa na visima na mifumo ya maji ya chini ya ardhi, makoki makubwa barabarani na alamu kwa ajili ya dharura ni mifumo mipya inayoendana na sayansi na teknolojia ya sasa ya nchi zinazoendelea na zinazoendelea.
DEMOKRASIA NA UONGOZI
Kuwajibika kwa viongozi haswa wa majeshi ya zimamoto na viongozi wa wizara husika pale wanapofanya uzembe katika sekta zao hutokana na mifumo ya uongozi wa nchi haswa katiba.
Katiba iliyopo ni ya zamani na imepitia marekebisho mengi ni vyema sasa kuwa na katiba mpya yenye vielelezo vya kuwawajibisha ikiwemo kuwaachisha kazi viongozi wazembe na wasiowajibika.
Ukweli na uwazi katika vyombo vya usalama vinavyofanya uchunguzi miaka na miaka bila kuja na suluhisho na ushahidi wa vyanzo vya majanga.
KWA UJUMLA
- Vifo na uharibifu utokanao na ajali ya moto vitapungua kwa kiasi kikubwa
- Uwajibikaji katika nchi utaongezeka kwa raia pamoja na viongozi
- Matukio ya moto kwa ujumla yatakuwa ya kima cha chini na hayatakuwepo kiujumla.

Upvote
2