Maoni: Ni hatari kumlea mtoto kimayai endapo huna kazi / biashara nzuri ya yeye kuja kurithi au huna ndugu wanaoweza kumlea kimayai ukiondoka

Maoni: Ni hatari kumlea mtoto kimayai endapo huna kazi / biashara nzuri ya yeye kuja kurithi au huna ndugu wanaoweza kumlea kimayai ukiondoka

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Hii tabia ya kulea watoto kimayai mayai tofauti na maisha ya kiuhalisia ya hapa kwetu wanayoyaishi wengi inaweza kuja kum gharimu sana mtoto.

mtoto anafuliwa nguo, mtoto haoshoi vyombo, mtoto anakula vyakula vya sherehe kila siku, shule ipo umbali wa dakika 10 anapelekwa na school bius, n.k

Kuna watu wapo katika haya makundi hawafai kulea watoto kimayai:

1. wenye ajira na vyeo wasivyoweza kuwarithisha watoto, mzazi ana kazi nzuri yenye mishahara, posho na njia za panya za kumuweka mahali pazuri kiasi kiuchumi lakini hawezi kumrithisha mtoto hii ni hatari, wenye nafuu ni watu wazito hasa mawaziri influential, wanajeshi wenye vyeo vkubwa, wanasiasa, n.k. hawa wana connections nzito za kuwaweka watoto wao ajira nzuri bila hata interview na wakaendelea maisha yao ya dezo. kama huna uzito huo usimlee mtoto kimayai maana ni wazi kabisa anaweza kuja kukosa ajira akashindwa kuyaendeleza maisha yake ya bata mwishowe ajiingize kwenye uhalifu.

1664738664424.png



2. Wafanya biashara wasioshirikisha watoto wao kuwaandaa kuja kurithi biashara, siku akifariki watoto hawaijui biashara kinachobaki ni kuuza mali kwa bei ya hasara, pesa zikiisha wanaanza kuishi maisha ya msoto. kama unataka kulea watoto kimayai kiongeze uwe kama waarabu na wahindi shirikisha watoto wako tangu wadogo ili hata ukifa waendelee kuishi maisha ya kishua kupitia biashara.

1664738997639.png


-3. Ambao hawana ndugu wanaoweza kuwalea watoto wao kimayai endapo wakitoweka, yawezekana ukawa na ndugu maajiri lakini hawapo tayari kukulelea mtoto wako wakampeleka kijijini aanze kula msoto, hapa yafaa uwe na ndugu wa karibu sana kiufupi watu kama wahindi na waarabu ndio huweza maana wanaishi wote sehem moja
 
Back
Top Bottom