Maoni: Serikali haikuwa sahihi kuiunganisha mifuko ya hifadhi ya kijamii

Maoni: Serikali haikuwa sahihi kuiunganisha mifuko ya hifadhi ya kijamii

Chendembe

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2019
Posts
444
Reaction score
488
Katika maamuzi ya serikali iliyopita ambayo sikufurahishwa nayo ni kuiunganisha mifuko ya hifadhi ya kijamii kwakuwa haukuwa shirikishi na haukuzingatia sababu za kiutafiti zilizopelekea kuundwa kwake.

Nilijiuliza maswali mengi juu ya faida ya uamuzi huo lakini nilipata chache mno na zenye mashaka.

Serikali inapounda maeneo mapwa ya kiutawala Kama vijiji, kata, majimbo ya uchaguzi, wilaya, halmashauri, mikoa, Wizara lengo ni kupanua wigo wa utowaji huduma kwa wananchi kutokana na ongezeko la idadi ya watu linalokuwa sambamba na watumishi/wafanyakazi.

Kama ili lilikuwa sahihi, basi ni sahihi kurudisha wilaya na mikoa na maeneo ya kiutawala waliyotuachia wakoloni. Au tufute local government tubaki na Serikali kuu tuuu.

Ni makosa yalifanyika kulundika watu wengi kwa Afisa masuhuli mmoja. Lazima kuwe na mkwamo wa utoaji huduma na kupelekea malalamiko mengi.

Nashauri serikali kuirudisha mifiko hiliyokuwepo ili kuboresha hudima.
 
... iliunganishwa ili kuwe na kapu moja au mawili hivyo kupelekea urahisi wa kukwapua fedha. Mnaodhani lengo lilikuwa kuboresha huduma kwa wazee wetu wastaafu mnakosea sana!
 
Back
Top Bottom