Maoni: Tunapoteza pesa au thamani yake bila kujua

Maoni: Tunapoteza pesa au thamani yake bila kujua

KIMOMWEMOTORS

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2018
Posts
358
Reaction score
675
Salam ndugu wana bodi.

Imekuwa ni kawaida yetu sisi Watanzania tulio wengi kununua gari jipya na kutumia kwa zaidi ya miaka 2.

Sisi kama waagizaji wa magari kutoka nje tumeshuhudia wamiliki wengi wakiulizwa kwa nini hawabadirishi gari, jibu huwa jepesi tu kwamba analipenda hilo gari husika.

Lakini ukweli ni kuwa iwapo utaagiza gari yako kutoka nje kwa gharama halali kabisa, kuna uwezekano mkubwa ukiamua kuu gari hii kati ya miezi 3 mpaka 12 utaiuza kwa bei sawa na uliyoagizia na wakati mwingine utaiuza juu kidogo kwa sababu gari hizo zikiwa mpya na zilizoingizwa nchini zinauzwa juu zaidi.

Ndani ya hiyo miezi 3 hadi 12, inaaminika gari yako itakuwa katika muonekano wake mzuri, hali nzuri, namba mpya, kilomita chache na sifa zote nzuri ambazo mtu mwingine atavutiwa kukurudishia pesa uliyotumia kuagizia.

Wengi wetu tunapenda tutumie gari muda mrefu zaidi kwa kuhisi kwamba pesa ya kuongezea ni kubwa bila kufanya utafiti wa kutosha, lakini pia wengine hudumu na hizi gari kwa sababu ya kupenda Brand na kusahau kwamba hizo gari ni nyingi hivyo unaweza kuuza hii unayodai kuipenda leo na ukaleta kama ile ile lengo likiwa ni kutunza thamani ya pesa yako lakini pia kuendesha gari lililo bora muda wote.

Kwa wanaonunua gari za mikononi pia kanuni ni hiyo hiyo kwamba ukinunua gari kwa 7m usisubiri ishuke thamani mpaka kuuzwa kwa 3m, tumia kwa muda mfupi kama miezi 6 una nafasi ya kupata mteja kwa 7m au 6.5m na hivyo thamani ya pesa yako ikaendelea kuwa hapo hapo.

Huwa inasikitisha mtu kaagiza gari kwa 20m anaitumia kwa miaka 5 na siku akitaka kuuza anaambiwa atalipwa 10m au 9m, swali la kujiuliza, hicho kiasi kingine cha pesa kimekwenda wapi? Jibu ni kuwa muhusika unakuwa umepoteza thamani ya pesa yako wewe mwenyewe kwa kuhisi huwezi kupata gari bora kama hivyo au kwa kuaminishwa kuwa utatakiwa kuongeza pesa nyingi kupata gari kama hivyo.

Wakati nipo Chuo rafiki yangu mmoja alikuwa akibadili simu kila toleo jipya linavyotoka, usipomuelewa unaweza kuhisi jamaa ana pesa nyingi, lakini ukweli ni kuwa alianzia simu ya chini na akawa anatumia muda mfupi, likija toleo jipya anauza ananunua na kuongeza pesa ndogo sana kupata hilo toleo jipya.

1F30D1DB-8AB5-4B10-800C-44BA654E0CA5.jpeg


7032529C-D6D0-4FBA-B9C2-82EB0E02D8FE.jpeg
 
Maamuzi ya kununua gari si kama manunuzi ya pipi dukani. Ni mchakato unaohitaji muda na kuumiza kichwa. Si kila mtu angependa kuumiza kichwa kila baada ya miezi sita.
 
Wazo lako ni sahihi kabisa kama unapata pesa yenye mzunguko mkubwa sometimes unakuta mtu anaagiza gari na anabakia mweupe mfukoni kama alinunua gari ya milion 13 basi atabakiwa na laki 5 Tu mfukoni...

Ila Kwa wazo lako naona Lina faida kubwa Sana Kwenye minimize cost kwasabb unakuwa unaongezea pesa kidogo Tu unavuta mnyama mwingine kuliko Ile ya kukaa na gari za miaka 5 huku ukitumia spare parts nyingi(chukulia Kwa mwaka mzima unatumia kiasi gani kununua spare parts?)
 
Hii haiendani na ALINUNUA BABU MPAKA MJUKUU ANALITUMIA
 
Sidhani kama tunanunua gari ili tuuze. Me nanunua gari ili nikae nalo ata miaka 10. If possible ata wanangu waje walitumie.
Umesahau mtoa mada Ni Dalali Maarufu jijini anatafuta kazi za kuuza magari kabla hajachakaa
 
Back
Top Bottom