Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Naunga mkono ila mh profesa muhongo arudi pale pale Nishati na madini ili kukomesha madalali kwa sura ya uzawa
 
Rais ndio huyo tena ameshaapishwa, waliomtaka na wasiomtaka ila wote hawa ndio rais wao wa awamu ya tano.

Je, wewe raia ungependa rais aanze na jambo lipi kulitendea kazi au kulisimamia ambalo unaona ni la muhimu na kwa sababu zipi?
mkuu kuna kasoro naiona hapa kuna rais na makamu wake ambaye huyu ataitwa msaidizi wa rais ,pale nairobi wana mfumo mzuri rais huambatana na makamu wake katika shughuli za kikazi mfano kukagua ,kutoa maelekezo kweli inapendeza hapa kwetu hali ipo tofauti hili mkuu tuliweke sawa
 
Wote ondoa ila prof.muhongo muache
. Ni mtu makini, mkali, anunuliki, msomi na anaogopeka uliza mameneja wa Tanesco, watakuambia. Huwa hana utani, ni the strongest candidate.
Mi ni ukawa pure

We nawe hujielewi kweli, yaani mafisadi ndo bado unawasifia kuwa ni watu makini, kama kweli RAIS aliyeingia madarakani ana dhamira ya kupambana na ufisadi watu wa aina ya Muhongo hawafai katika baraza la mawaziri, na ile mahakama ya mafisadi pamoja na wengine isimusahau huyu muhongo
 
Magufuli waite matajiri wakubwa wazawa,waeleze mikakati yako kuhusu makusanyo ya kodi iliyo rafiki, kufungua miradi mikubwa, ujenzi wa shule zenye ubora na ada nafuu, wenye viwanda jinsi ya kuvipanua/kuongeza mitaji ili vitoe ajira kubwa...nakadhali
 

Nakubaliana Na Wewe Kwa Wenye Namba 2, 5, 7, 9, 10, 11 Na 12 Tu. Ila Hao Wengine Waliobaki Nadhani Umewaonea Mkuu.
 
Wachezaji walewale endapo watabailishiwa kocha na kuletewa mzuri watafanya vizuri!
 
Ni mawazo yako, ila watu wanaoendana na kauli mbiu yake ya hapa kazi tu, Muhongo, Mwakyembe lazima wawepo! Mwigulu bado ana ya kujifunza ila nae lazima awepo!
Mi nina uhakika kuna makatibu jembe awape ubunge kisha uwaziri, kwenye hii list yako sioni wabunge hata kumi wenye sifa. Lukuvi sijui kafanya nini mpaka leo mpaka watu wampigie debe la waziri mkuu, Makamba mawasiliano pamoja na kuwa naibu waziri kaboronga, mitandao ya simu wanabadilisha vitu kila wakijisikia bila ya tcra kufanya lolote!
Majembe hapo ni Muhongo, Mwakyembe, Mwigulu.
Waziri wa biashara na uchumi unachukua Lipumba unaweka, wizara inayohusiana na vijana unachukua Mnyika unaweka, kisha tunasonga mbele.
 

mim ikatika wote huyu tu hafai hafai hafai hafaiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Muhongo kichwa aliingizwa chaka nA wabongo, huyu arudi tena kwenye nishati alisimamia vema tanesco
 

Mwambie arudishe pesa za umma kwanza (Esclow) then ndo urudi hapa kumpigia chapuo ya uwaziri
 
Muhongo kichwa aliingizwa chaka nA wabongo, huyu arudi tena kwenye nishati alisimamia vema tanesco

kuingizwa chaka nako ni udhaifu, nchi za wezetu ukishajiuzulu kamwe hurudi kwenye ulingo, ndo umepotea kwenye game.
 
Wachezaji walewale endapo watabailishiwa kocha na kuletewa mzuri watafanya vizuri!

Hii ni nchi mkuu, sio mpira, hao wote niliowataja hata ashuke yesu hakuna jipyaa hapoi, ukichoka umechoka, kama huwezi, huwezi tuu.
 
Mwambie arudishe pesa za umma kwanza (Esclow) then ndo urudi hapa kumpigia chapuo ya uwaziri

Sawa nitamwambia... Ila ujue kwamba mimi simpigii chapuo mtu yeyote yule ila nimetoa mchango kutokana na mtoa mada alivyowasilisha. Ningekua nimeyasema haya mbele ya rais hapo ningejiona nimempigia chapuo.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…