Kwanini nasema Raisi yuko sawa?
1. Anaonekana ni kweli anapigania kile wananchi wanataka,
2. Sio Mwoga wa maamuzi kiasi fulani,
Siwezi kumwelezea Raisi zaidi kwabasabu kile watanzania tunataka anakifanya yeye kama yeye, si kisheria, kwasababu Sheria tayari CCM wameshaharibu.
CCM wametengeneza Sheria mbovu ambazo zinampa tabu Raisi kutete Rasilimali za Nchi, Tuliona Mpambano ya Wabunge wa CCM na Upinzani kuhusu Sheria za Madini na Gesi ziweje? mpaka walifikia hatua ya kutishiana maisha na Upinzani kususia kupitisha Sheria hizo.
CCM walipitisha na Mikataba ikasainiwa na kutwambia ni Siri. Nampongeza Raisi kwa sababu katuonyesha kati ya Wabunge wa CCM na Upinzani nani alikuwa anapigania masirahi ya Nchi.
Mpaka hapo mmenielewa vizuri.
Ila Raisi nakuomba utumie sana Hawa wanasheria wako, ili kufuata utaratibu wa Kinchi na Kidunia usiweze kukwama mahali.
UVCCM mnatia aibu kama Baba zenu CCM, hivi mlifanya sherehe ya kumpongeza Raisi na Chama chenu,
Hamkusikia aibu?
kwanini msingempongeza Raisi bila kutaja Chama chenu?
Hamjaona kilichosababisha Mchanga kusafirishwa?
Hivi kabla ya kumsifia Raisi, hamkufanya uchunguzi ni nani aliingia Miakata na kutengeneza Sheria za kuwaruhusu Wawekezaji kusafirisha Mchanga?
Msiwe kama mashabiki wa Soka kushangiria Chenga na Magoli, yafaa mjue nini maana ya Nchi na matendo ya Kinchi, Chama chenu kimeferi, yafaa mfate ya Magufuli sio ya CCM, Mkitaka kutamba na CCM wafundisheni kazi Baba zetu Bungeni jinsi ya kutunga Sheria za masirahi kwa Nchi, sio kwa matumbo yao, maana Sheria wanazotunga haziifaidishi hata CCM yenyewe.
Yangu ni hayo
Tanzania mbele, CCM, CHADEMA, CUF baadae.