Tuache hizi longolongo za uzalendo sasa,zimepitwa na wakati.Mara wapiga dili sijui mafisadi na wala rushwa mambo ya kizamani hayo. Mhenga mkuu aliyezifanya mbingu na nchi alishasema ni halali kwa mlawi kula vya madhabahuni.
Unategemea nini kuniweka juu ya hazina yako wakati nina kiu na njaa balaa!naanzaje mimi kutunza hiyo hazina bila kuitiatia mkono?
Njaa siyo mchezo,Mfalme Daudi alikula mikate ya wonyesho akijua si halali kwake, Hivi vijichenji mnavyo walipa watumishi wenu havikidhi njaa zao mjue.Lipeni mishahara ya maana muone watu wanavyopiga kazi.Kazi na njaa ni kama mbingu na ardhi bana.
Hebu jaribuni hilo mjionee maajabu.
Post sent using JamiiForums mobile app