Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Hivi kitu gani kinamfanya magufuli yeye kutokukaa pembeni????

ILILIINGIZA, ANALIINGIZA NA ATALIINGIZA SN HASARA TAIFA

1. Alikamata kiholela samaki wa magufuli kesi tumeshingwa kwa ujinga wa mtu mmoja

2. Alivunja mkataba wa ujenzi kijingajinga kabisa tumeshindwa kesi

3. Alijiuzia nyumba za serikali

4. Anavunja katiba na sheria za nchi

5. Anavunja sheria za manunuzi na kujipangia matumizi ya raslimari za taifa mfano kujijengea uwanja wa ndege chato, kujinunulia bomberdier kwa maslahi yake binafsi...


MTU WA HIVI ANAFAIDA GANI KWA TAIFA? KWA NN ASIKAE PEMBENI YEYE KWANZA????
 
Wewe kama ni Raiya wa Tanzania na si hawa wingine waliijipenyeza na kujivika Utz humu kwa nia ovu mbili moja ya kutambua fursa mbali mbali za kwetu. Ya pili kumanipulate na ku spin kila jema linaloongekewa au linalotreand kwa lengo la kuchafua nchi yetu na hasa Mkuu wa nchi

Nakushauri geuza thread yako hivyo hivyo ufanye updates iwe unauelekeza kwa Washauri wa wezi wanaotuibia rasilimali zetu. Ielekeze pia na kwa wapinzani ukiwashauri wamuunge mkono Mkuu wa nchi kwa mema anayofanya

Waelekeze pia wapinzani wawashauri wakuu wao wasiminye uhuru wa wanachama wao kugombea nafasi za juu
 


Ni kwa sababu alichaguliwa na asilimia kubwa ya watanzania, Na hakuna kiongozi perfect Duniani..

The best prez in Africa
 
Take this...sbb umeniudhi vibaya,🙁🙁😱 nilidhani unaandika mambo ya msingi kumbe pumba pumbaf..

Ushauri wako & marks.

1: Kiuchumi = 00%

2: Kisiasa = 5%

Poorest advice.. Hapo kwenye Acacia wezi wakubwa unawatetea? Rubbish, ndio hovyo kabisa umeongea.. I deduct more -10%, off. 🙁🙁😳😳🙁🙁🙁
 
mie naona kila wizara iwe na independent body ya directors toka nchi mbali mbali,WENYE ELIMU,EXPIRIENCE AND EXPOSURE.................................utawalipa hela nyingi ndio,lakini utatumia utaaalamu wao kumove forward.
 
muda si mrefu atagombana na WAZANZIBAR anataka kuchukua mapato yao ya viza,,Sijui kashauriwa na nani maana kwenye hilo kama muungano haukuvunjika basi utayumba sana
 
Ushauri mzuri sana Allah akubariki na aibariki Tanzania.
 
Sizonje ndie anaewashauri washauri wake namna ya kumpa ushauri

One term

Sent using North Korean Hydrogen Bomb
 
Kuna uwezekano wa 99% kwamba waliovamia clouds ndio waliofanya jaribio la kumuua Lissu. Siro alipewa u-IGP ili kikosi cha bashite kiweze kutekeleza matendo yake bila bugudha popote nchini. Amani ya nchi hii inaondolewa na bashite.
Acha ujinga usipende kuongea vitu ili mradi umeongea ,una uthibitisho na unachoongea?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna uwezekano wa 99% kwamba waliovamia clouds ndio waliofanya jaribio la kumuua Lissu. Siro alipewa u-IGP ili kikosi cha bashite kiweze kutekeleza matendo yake bila bugudha popote nchini. Amani ya nchi hii inaondolewa na bashite.
Bashite umeishajulikana unajisikiaje?
 
Awali ya yote nawapa pole watanzania na wapenzi wote wa amani na demokrasia Tanzania. Chadema na wananchi wote waliogubujikwa na kushtushwa na shambulio lililompata Mh Tundu Lissu.

Mimi nataka kutoa maoni na sina shaka yatamfkia bwana mkubwa Raisi Dr.Magufuli.

Raisi,mimi sina chama,ila ni mkerketwa na mshabiki namba moja kwako kutokana na ari mpya na uzalendo ulionao juu ya Tanzania.

Kusema ukweli,Tanzania imechezewa na kuibiw a sana. Nakusapoti kile unachofanya na usirudi nyuma.
Lakini pia,katika tendo jema unalofanya mengine unarudi nyuma. Sitaki kukuhukumu kwa jambo lolote lakin junanmanbo yako wazi.

Suala la upinzani Tanzania limekuwa kama uadui. Upinzani sio sawa mchezo wa miguu au kuonekana wewe ni bora zaid ya yule. Tafsiri niijuavyo ya upinzani ni kusaidiana na kuelekezana pale mmoja anapokuwa anakosea kwa hoja za msingi na zenye maslahi chanya kwa Tanzania.

Upinzani sio mangumi,matusi na kejeli kaka watanzania wengi wanavyofanya.Lazima tutangulize maslahi mbele ya nchi bila kupepesa macho au kuangalia pembeni.

Kumekuwa na siasa katika mashule na kazini nk. Vikundi cya chama mashuleni,huku tunatafuta nini? tumeenda kusoma au kufanya siasa. Pamoja hii sio hoja yangu ya msingi sana naona ni wakati kutenganisha siasa na weledi na pia kutoa siasa makazini na mashuleni.

Mh Raisi Magufuli nikufahamishe tu kuwa mkuu,upo katika vita kali sana ya uchumi. Wazungu na wachina na waarabu huko wanakuangalia sana kwa macho mabaya.Hizi ghasia zinazotokea hapa na pale unaweza ukawapa mwanya mkubwa sana wa kuharibu amani iliyopo.
Pia wapo watanzania wengi ambao hawakutaki na wengine wanaona umeleta kauzibe. Nguvu yake unaweza kudharau lakini itapeleka nchi kubaya.
Tanzania ni nchi ambayo imekuwa tulivu na kipekee sana kwa muda mrefu. Kwasbabu hatukuwa tumejitambua. Huko mbele tutarajie misukosuko kwa mfano kibiti ni mfano halisi wa watu wa nje wanaotaka kuharibu amani yetu. Hawa watu wapo wazungu na middle eastern countries na ndio wafadhili wakuu.

Mh Raisi huu ni mchezo wa akili na tumia akili kuwazidi na ujue utapita wapi kabla ya matukio na baada. Wapo hawatakuelewa lakni naamini ipo siku.
Nakushauri kuongea na upinzani na kuwaweka mbele katika vita hii. Usifanye vita hii pekee yako. Hata ukifa leo,Tanzania itarudi kulekule kutokana na kwamba hujatuonyesha njia na haujatufumbua macho au kutusaidia.Ni wewe tu ndio unashika tochi na kusonga mbele.

Nafahamu nia yako ni njema. Najaribu kufikiri kuwa huna wasaidizi wanaona mbali zaidi ya matumbo yao.
 
Unakaaje na wapinzani ambao wanachotwa na haohao maaduizetu wa kiuchumi, wanaomba taarifa kutoka kwa wanyonyaji ili wazitumie kukwamisha mikakati ya taifa kujinasua katika hii mitego tuliyonasa? Kuondoa hili la wanasiasa kuzuiwa kuitisha mikutano, Magufuli yuko sahihi 100%. Upinzani wamethibitisha kuwa hawana hata chembe ya uzalendo. Sad!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…