Kwa maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.
Nimeanza na huo mstari nikiishauri serikali kuagiza nyaraka zote zilizoandikwa na vikundi mbali mbali na taasisi za dini ziletwe na azipokee kama maoni ya wananchi.
Nimeona mengi yaliyopo kwenye nyaraka hizo na hata kwenye ajenda za Mange yapo ndani ya uwezo wa serikali, sasa nashangaa kwa nini serikali inaziogopa na kutaka kuzificha uvunguni.
Jamii ina hamu ya kusikika, kuziepuka na kuzipuuza au kuzipa mgongo hoja za taasisi hizo au vikundi hakutaondoa duku duku lililo ndani ya mioyo ya watu bali kutaleta fukuto.
Serikali izipokee hizo nyaraka na siye wana mitandao tutawasaidia kujibu hoja moja baada ya nyingine msaada wetu ukihitajika ili jamii ya Watanzania itulie.