Mkuu sijui unaishi pembe gani ya Tanzania, ingekuwa vizuri kama ungekaa kimya maana kitendo cha kuamua kuba humu na kuanza kuandika utumbo usio heleweka mimi naona umejihaibisha mwenyewe tu.
Uamuzi uliochukuliwa na Rais Magufuli wa kuleta sera ya elimu bure kwa watoto wetu kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha nne, hiyo peke yake ni hatua kubwa sana ya maendeleo ambayo yanamgusa kila mwananchi wa kila kijiji. Uamuzi huu sio mdogo kwenye kwenye kuchangia maendeleo ya watanzania.
Napende kukukumbusha kitu kimoja, hizo barabara ambazo unada Rais Kikwete amezijenga kwa lami na kuzisambaza nchi nzima, msimamizi wa hizo barabara alikuwa Rais Magufuli ambaye wakati huo alikuwa waziri wa ujenzi, usafiri na mawasiliano. Wewe unafikiri kwa nini anajulika kwa jina la Bulldozer?
Arusha ni mji maarufu kwa sekta ya utalii Tanzania, kukiwa na usafiri wa uhakika kwa watalii kwenda kwa ndege Arusha, namaanisha Kilimanjaro, huoni mwananchi
wa Oldadai -Arusha naye atafaidika kwa namna moja au nyingine kama atajishughulisha na mambo ya biashara au kutafuta ajira?