Songa: ujumbe mahususi kwa raisi
Intro
Mtaani hali ni mbaya haya matatizo uyakumbuke, watu hali ni mbaya baba utukumbuke...mtaani hali ni mbaya ohh
watu hali ni mbaya sanaa ya kwetu uikumbuke, mtaani hali ni mbaya matatizo uyakumbuke...
Kwanza pole kwa majukumu ya hapa na pale, sasa na kale yanayokufanya usilale...
Nikwania njema tu wananchi wako wapate, maisha bora kesho wakiamka wawe na mkate...
Kiukweli unapambana na maadui hawaishi, na wale ambao wanajifanya hawajui ni wabishi..
Usiku sio mchana na wala asubuhi haitishi, na ujumbe nao andika ni mahususi kwa raisi...
Tunahitaji wasanii tuwe happy na sisi, kila siku tunalia kuhusu haki miliki...
Wanyonyaji wametanda hata pasi hatupigi, wenzetu nje wanapanda tena kasi inazidi..
Wachache watakupa upendo wakutupe, sijaona wakuziba pengo la ruge..
Waliokua sugu wanakitengo cha ubunge, msisubiri hadi kwenye kampeni ndio mtukumbuke...
Chorus
Mtaani hali ni mbaya haya matatizo uyakumbuke, watu hali ni mbaya baba utukumbuke...mtaani hali ni mbaya ohh
watu hali ni mbaya sanaa ya kwetu uikumbuke, mtaani hali ni mbaya matatizo uyakumbuke...
Inua mkono kama elfu mbili ulipata, noma sana hauwezi nunua hata data...
Hauwezi record hauwezi kula bata, na ndio maana nimeamua kumuandikia kenyata..
Uko wapi? Wasanii tunaumia, hatuko happy...tumejaribu kukufikia, hatukupati...
Hiyo hela tanzania haifiki laki, piga simu moja kama billnasi...
Mi ni mlima wanajua bado na songa, I've been patient lakini sijapona
Starehe ndani ya tabu na tumesota, wanatunyanyasa kila kona...
Msanii bana siwezi kopesha, sina uhuru tafadhali in force presha..
Ikifika ni kampeni njoo tesa, ila tukilalamika ndio mnasepa...
Chorus
Mtaani hali ni mbaya haya matatizo uyakumbuke, watu hali ni mbaya baba utukumbuke...mtaani hali ni mbaya ohh
watu hali ni mbaya sanaa ya kwetu uikumbuke, mtaani hali ni mbaya matatizo uyakumbuke...
End
........written by Scars........