Maoni ya Katiba: Agenda za CCM zinasonga vema mbele!

Maoni ya Katiba: Agenda za CCM zinasonga vema mbele!

Omutwale

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2008
Posts
1,429
Reaction score
1,047
Nimejitahidi kufuatilia kwa ukaribu zoezi la ukusanyaji wa maoni juu ya uandishi wa Katiba linalohitimika sasa kwa Mkoa wa Kagera. Palipo wezekana nimefika na kushiriki kwenye "uwanja wa vita" . Hadi sasa naweza kusema yafuatayo:

ccm inadhihirisha kujipanga vema kusonga kwa mafanikio katika kufikisha hoja zake kwenye meza ya Katiba

Hoja kuu ni tatu ambazo ccm imezishikia kidedea:

  1. CCM inataka mwanafunzi akipewa mimba asikamatwe mwanamme na kushtakiwa au kuwajibishwa peke yake. Bali na msichana aliyevua nguo naye ashtakiwe na kuwajibika
  2. CCM haitaki Serikali za Majimbo. Wasio na uelewa juu ya mfumo huo wamesombwa na marudio ya ushawishi wa kupinga serikali za majimbo. Hivyo wanaohudhuria mikutano wengi wanatoka na chuki dhidi ya serikali za majimbo.
  3. Amini usiamini; ccm inaongoza injili ya kurejeshwa kwa serakli ya Tanganyika na uwepo wa Muungano wa Serikali tatu (3). Nimejihoji juu ya suala hili; inakuwaje CCM ile matapishi yake kimyakimya! Jibu lake nimelipata hapa (NINAKUOMBA USOME): https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ni-sana-kilicho-nyuma-ya-pazia-hiki-hapa.html
3. Katiba ijayo iruhusu serikali tatu na by any means ilazimike kuwa EL awe rais wa Tanganyika, Dr Slaa/CHADEMA wa Muungano (asiye na nguvu yoyote) na Shein aendelee Zanzibar….
Nasema kwa kuthibitisha kuwa hoja hizi zinafanikishwa na CCM kwa kuwa wanaotoa maoni hujitambulisha kabla ya kuchangia. Na mara zote (kwenye mikutano ya Muleba, Karagwe , Kyaka na Kanyigo) hoja hizi zimewakilishwa na watu wa jinsia moja tu; ya kike, wakijitahabanaisha kutoka Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ambayo ni Taasisi ya CCM.
Mengineyo:
Tume inazidi kupata uzoefu na kuboresha ukusanyaji wa maoni. Awali hawakuwa wakitenda haki sawa lakini baada ya kutoka Karagwe wameboresha sana na kiukweli sasa wako fair >90%. Mambo yaliyokuwa yanaondoa usawa na mazingira bora ya kukusanya maoni ni pamoja na:

  1. Wafanyakazi wa Tume kuwa wakali kwa Wananchi na kukosa moyo wa kutoa huduma, kusikiliza, kuelekeza na kuonyesha mlengo wa maoni wanayotaka. Walikuwa kama vile wao ndiyo ndiyo watoa maoni.
  2. Viongozi wa serikali hasa Wakuu wa Wilaya na dola kuambatana na Tume kila mahali wakisindikizwa na misururu ya magari, askari (FFU), na kutanguliza taarifa za vitisho kwa watakao toa maoni ya papo kwa papo.

Uwepo wa viongozi wa serikali na dola mikutanoni uliogofya wananchi wengi kutoa maoni kwa uhuru. Ili limeathiri sana maeneo ya Muleba.

Baada ya Tume kupokea sms nyingi zikilalamikia mazingira haya yenye kujenga hofu ili kuminya uhuru, sasa viongozi wa serikali hasa wakuu wa Wilaya hawaruhusiwi na Tume kuendelea kuwepo eneo la Mikutano na kusikiliza maoni ya Wananchi wao. Pia misururu ya magari pamoja na askari (FFU) wamepunguzwa. Mazingira haya yameonekana kuwa muafana na hoja huru kabisa zilianza kusikika. Mfano Kanyigo watu wamepinga sana mosi uwepo wa Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Mikoa na pili Rais kuwateuwa Wakuu hawa pamoja na Wateule wengine kama Mawaziri.

Nawahi kutoka mjini imebaki Hiace moja tu ya Ta Kahwa.

Nawatakia udadavuzi mwema.

Omutwale owa Kanyigo

cc:
Mkandara, Congo, Isalia, MTK, Kibona, koo, Mtoboasiri, Manyi, Mkirua, Democracy999, Tume ya Katiba, Safari_ni_Safari, mgen, Mpita Njia, Ndahani, jogi, Ndahani, Gwalihenzi, Mwiba, Barubaru
abdulahsaf
 
Nimewaona Mkandara, Congo, Isalia, MTK, Kibona, koo, Mtoboasiri, Manyi, Mkirua, Democracy999, Tume ya Katiba, Safari_ni_Safari, mgen, Mpita Njia, Ndahani, jogi, Ndahani, Gwalihenzi, Mwiba, Barubaru
abdulahsaf mkibishana kwenye https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/294612-kila-la-kheri-zanzibar-bye-bye-muungano.html

Hii taarifa ya Kagera itawapunguzia ubishi. Barubaru wiki jana tulikutana Kamachumu, pale kwa kina Jabir (El saqr) njia ya kwenda Ndolage Hosp. Nilifikiri katika tathmini yako ya ziara nchini Tanzania ungekuwa umeyasoma haya na kuuona mkono wa "bye bye" Tanzania na karibu upya Tanganyika na Zanzibar!
 
Suala la katiba ni gumu sana...nilidhani watawaelewesha kwanza wananchi ndio waanze kukusanya maoni ila kwa ninavyowajua wenzangu wengi watarubuniwa na watatoa maoni ambayo hayatakidhi matakwa yao na baadae ndio watajua kuwa wameingizwa mjini na hakuna namna!
 
Wala hata sina mda wa kupoteza kutoa maoni juu ya hii katiba maana NINA UHAKIKA, CCM HAWATAWEZA KUTUONGOZA tutengeneze katiba hii. Kwa anaenipinga anipinge tu, but tutaona 2014. Akina Warioba wanapoteza tu mda. Katiba kielelezo itapigiwa kura ya HAPANA na wananchi 2014, then serikali mpya itakayoingia 2015 itatuletea katiba mpya, not before 2018.
 
Wala hata sina mda wa kupoteza kutoa maoni juu ya hii katiba maana NINA UHAKIKA, CCM HAWATAWEZA KUTUONGOZA tutengeneze katiba hii. Kwa anaenipinga anipinge tu, but tutaona 2014. Akina Warioba wanapoteza tu mda. Katiba kielelezo itapigiwa kura ya HAPANA na wananchi 2014, then serikali mpya itakayoingia 2015 itatuletea katiba mpya, not before 2018.

Una maana MABILLION hayo yote yanayotengwa kwaajili ya tume ya katiba yatateketea bure?! Kwanini basi yasingekuwa invested kuboresha huduma za afya au kununua madawati kwaajili ya wanafunzi au kuchimba VISIMA?

OMUTWALE Je uliweza kufikisha mapendekezo yangu niliyokupatia? Nilisahau pendekezo moja nalo ni: MA-MEYA au WENYEVITI WA HALMASHAURI wasichaguliwe na madiwani bali wapigiwe kura na wananchi WOTE kama vile wabunge.
 
OMUTWALE Je uliweza kufikisha mapendekezo yangu niliyokupatia? Nilisahau pendekezo moja nalo ni: MA-MEYA au WENYEVITI WA HALMASHAURI wasichaguliwe na madiwani bali wapigiwe kura na wananchi WOTE kama vile wabunge.

Bobuk,
Nilifanya hivyo....tafuta gazeti la Mwananchi la leo nafikiri watakuwa wametoa coverage yenye maoni yako. Tulikuwa na Mwandishi Phinias Bashaya na nilimsisitiza alitolee taarifa jinsi watu wa Misenye walivyolichangia juzi. Ukilipata utuwekee na sisi maana Gazeti litafika Bukoba kesho!
 
Una maana MABILLION hayo yote yanayotengwa kwaajili ya tume ya katiba yatateketea bure?! Kwanini basi yasingekuwa invested kuboresha huduma za afya au kununua madawati kwaajili ya wanafunzi au kuchimba VISIMA?

OMUTWALE Je uliweza kufikisha mapendekezo yangu niliyokupatia? Nilisahau pendekezo moja nalo ni: MA-MEYA au WENYEVITI WA HALMASHAURI wasichaguliwe na madiwani bali wapigiwe kura na wananchi WOTE kama vile wabunge.

acha tu hizo hela zipotee maana tunachokihitaji tunakijua. Huwezi mwambia mtu atoe maoni ya kitu asichokijua, ni upuuzi. Katiba wameificha miaka yote hata shuleni hakuna hata sample ya kufundishia. Nimeona kitabu cha katiba baada ya kumaliza f6 na nimeifahamu baada ya kuanza chuo. Huu ni uwoga wa kuogopa watu wakijua haki zao watazidai! Kwa wenzetu mpaka watoto wanaimba katiba huku mpaka mtu anamaliza chuo, masters phd haifahamu. Mi mwenyewe kwa sababu ya uanaharakati chuoni ndo kuna jamaa alinipasia ili kila nnapoongea niwe na evidence za kikatiba. Kuhusu uchaguzi wa mayor au wenyeviti itakuwa na ugumu kidogo kwani itahitaji uchaguzi wa madiwani aafu muitishe uchaguzi mwingine wa hao jamaaa,. Madiwani tunaowachagua wakiwa makini tutapata viongozi wazuri tu.
 
Back
Top Bottom