Elections 2010 Maoni ya Tendwa Kuhusu Uchaguzi

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790


Huyu jamaa ameongea jambo moja zuri kuhusu katiba mpya. Ila melezo yake kuhusiana na lowa turnout si ya ukweli unless aseme kuwa wanachi wa leo ni mbumbu kuliko wa miaka iliyopita, in which case atakuwa ana-imply kuwa uongozi wa sasa umewapumbaza sana raia kiasi cha kutokufahamua hata umuhimu wa kupiga kura. Tangu nchi hii inapata uhuru, haijawahi kuwa na low turnout, na wakati huo ndipo tulikuwa na umma wa wasiokuwa na elimu yoyote. Leo hii kila kijana anapata elimu ya msingi, na hiyo ingemwezesha kabisa kujua umuhimu wa kupiga kura. Sehemu zote ambazo CHADEMA imeshinda, ni kwa sababu vijana walilirinda kura kwa karibu sana. Imani yangu ni kuwa pamoja na vitisho vilivyotolewa na vyombo vya usalama siku chache kabla ya uchaguzi, na njia makusudi zilizofanywa na Tume kuvuruga daftari la wapiga kura ili vijana wasipige kura, bado kuna kura nyingi sana zilizopigwa, ila tume haikuzitangaza zote kusudi ionekane kuwa wanapenzi wa CCM pamoja na uchache wao, walipga kura za kuipa CCM ushindi wakati wale wapenzi wa vyama vya upinzani pamoja na wingi wao hawakupiga kura za kutosha kuvipa vyama vyao ushindi.


Ni afadhali jamaa hawa wasiongelee tena swala la upigaji kura wa Oktoba 2010 kwa vile wote walishirikiana kuhakikisha CCM inashinda kwa njia yoyote hata bila kupigiwa kura
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…