Maoni yako kama Mdau wa Siasa za Tanzania kuhusu katiba mpya

Protector

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2019
Posts
422
Reaction score
893
Kwa maoni yako binafsi bila kuangalia upo upande gani wa siasa, ukaambiwa utoe maoni yako juu ya upatikanaji wa katiba mpya ungechagua yapi kati ya haya:
1. Serikali moja, Rais wa JMT bila kuwepo Raisi wa Zanzibar
2. Serikali mbili, mfumo ubaki kama ulivyo sasa hivi
3. Serikali tatu, Awepo Rais wa JMT na Raisi wa Tanganyika na Zanzibar
 
SERIKALI tatu kama Rasimu ya Warioba iandikavyo!!serikali mbili ni kubariki uharamia na maruwe ruwe yaitwayo kero za muungano!!
 
Kwa maoni yako binafsi bila kuangalia upo upande gani wa siasa, ukaambiwa utoe maoni yako juu ya upatikanaji wa katiba mpya ungechagua yapi kati ya haya:
1. Serikali moja, Rais wa JMT bila kuwepo Raisi wa Zanzibar
2. Serikali mbili, mfumo ubaki kama ulivyo sasa hivi
3. Serikali tatu, Awepo Rais wa JMT na Raisi wa Tanganyika na Zanzibar
Serikali 3 itafaa zaidi, Kila mtoto ale Kwa JASHO lake.
 
Serikali 3 na Tanganyika iwe na mfumo wa majimbo. Nchi kubwa kama yetu number muhimu kuwa na maamuzi kieneo na hii inaleta ushindani Kati ya majimbo.
 
Serikali moja tu. Mbali na kupunguza gharama italeta utulivu. Hofu ya kwamba Zanzibar wakishinda wapinzani muungano utakuwa mashakani itatoweka.
 
Kwa maoni yako binafsi bila kuangalia upo upande gani wa siasa, ukaambiwa utoe maoni yako juu ya upatikanaji wa katiba mpya ungechagua yapi kati ya haya:
1. Serikali moja, Rais wa JMT bila kuwepo Raisi wa Zanzibar
2. Serikali mbili, mfumo ubaki kama ulivyo sasa hivi
3. Serikali tatu, Awepo Rais wa JMT na Raisi wa Tanganyika na Zanzibar
Inshu ni serikali moja..mana ndio lilikua lengo la tangu awali la muungano.

Kuipa zenji mamlaka kamili ni kuhatarisha uhuru wa wananchi kote bara na visiwani.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom