Maoni yako tafadhali: Biashara ya nafaka

mjenziwakale

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2015
Posts
954
Reaction score
1,469
Wasalaam.
Wakuu nina business idea ambayo nko mbioni kuanza kuifanyia kazi,biashara yenyewe ni ya nafaka ambapo napanga kununua mashine za kufanyia processing mazao ya nafaka especially mpunga, mahindi pamoja na maharagwe.

Mazao nitakuwa nayakusanyia mkoani Mbeya kutoka kwa wakulima nayahifadhi stoo huku nikiendelea kuyaprocess kwa kutumia mashine ntakazozinunua.
Baada ya hapo ntakuwa nasafirisha nafaka ambazo ni tiyari kwa matumizi ya binadamu

Soko langu kubwa nategemea litakuwa mkoani Dar es salaam ambapo nitakuwa nasambaza kwenye taasisi mbalimbali zikiwemo shule, vyuo pamoja na watu wengine watakaokuwa wanahitaji mzigo kwa bei ya jumla.

Mtaji wangu kwa kuanzia nimeandaa millioni 40.

Wakuu tafadhalini naomba mnipe mawazo pamoja na mwongozo zaidi katika biashara hii
 
40 million yaweza kuwa inatosha lakini pia yaweza kuwa ndogo kwa mantiki ifuatayo;
Unanunua mtambo upi wa processing na utaufunga wapi?
Utasafirishaje mali ghafi mpaka kiwandani kwako ?
utawafikishiaje walaji au soko bidhaa yako?
Kuwa na mtaji pekee kama lengo haitoshi lazima ujue unawalenga idadi kiasi gani ya walaji na hivyo uwezo gani wa kuzalisha bidhaa utumike? ..................haya ni machache niliyofikiria kuwa unapaswa wewe mwenyewe uyafanyie kazi kwanza, wenzagu wataongezea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…