Maoni yangu binafsi juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea duniani

Gagalo atazitumia hoja hizi hizi kudai haki na damu itamwagika
 
Wengi huwa hawajiulizi kwanini Nyerere alitawala miaka 24 na miezi 8
 
Jaribio la mapinduzi ya kijeshi la mwaka 1964 lilisababishwa na dhuluma dhidi ya wanajeshi wa ngazi za chini
 
Jaribio la pili lilikuwa kupinga itikadi ya ujamaa ambao waliona umeleta matabaka ya walio nacho na masikini
 
Kama kuna bima ya afya basi sheria hiyo itasema ni kosa la jinai fedha za umma kutumika kwa matibabu nje ya nchi kwa mtu yeyote yule.


Wengi wanaokimbilia nje ukiwatafakari sanaaaaaaa utaona ni ukimwi unawapekecha na ni tamaa zao za ngono zinewafikisha huko.

Ni busara wakatibiwa humu humu ndiyo watahimiza khali bora za wauuguzi wetu.

Wakienda nje watakomalia kuwapiga akina Ulimbokha ili kuduwaza huduma za afya nchini ambazo zimeishia kujenga majengo na ndani ya hayo majengo hakuna la maana linaloendelea.
 
Tunasema bajeti ya matibabu ya viongozi nje ya nchi ni ufisadi
 
Kama kiongozi anajua akiumwa yeye na awapendao watakimbilia nje ya nchi kutibiwa ataweza kusimamia na kuboresha huduma za afya ambazo yeye hana imani nazo?
 
Sababu kuu ya kudai uhuru ilikuwa tujitawale wenyewe kwa sababu tunayajua matatizo yetu
 
Ukitibiwa nje ya nchi matatizo yetu unayajua kweli na tofauti yako na mkoloni iko wapi?
 
Watawala wa Cuba wana maadili hakuna raia kutumia hela za serikali kutibiwa nje ya nchi.

Yaani ni fedheha kwa kiongozi wa umma kukimbia huduma za afya ambazo unazisimamia kuziimarisha
 
Kama wewe kiongozi wa umma unaona ni haki yako kutubebesha gharama za matibabu yako nje ya nchi just fika wewe ni fisadi nyangumi na huna soni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…