Maoni yangu binafsi juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea duniani

Hawa Chadema ni matutusa wanadai katiba mpya wakati yao ni majitaka.

Kamati kuu imejilimbikizia mamlaka kila kitu ni wao matokeo yake wamekuwa mahakimu kwenye kesi zao wenyewe na kuharamisha wao wenyewe upotolo wao.

Sasa wanarukaruka mara maamuzi ya Kamati kuu yako palepale yaani mbavu zangu hoi.


Mara tutawasiliana na Spika awafute ubunge na kauli hizi zinatuthibitishia Chadema hawako tayari kukamata dola sasa na hata milele.

Kifupi tu, tatizo lao ni katiba yao imerundika mamlaka kwa Kamati kuu kinyume na matakwa ya sheria zetu.

Wajirekebishe au jamii itawarekebisha kwenye vituo vya kupiga kura
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…