LAPSE RATE
Member
- Oct 18, 2015
- 79
- 98
MAONI YANGU JUU YA KUAHIRISHWA KWA MECHI YA WATANI WA JADI KATI YA YANGA DHIDI YA SIMBA MAARUFU KAMA KARIAKOO DERBY YA TAR. 8/03/2025
Naanza kwa kuwasalimia wadau na wapenzi wa soka.
Naomba nieleweke kwamba ninaandika makala hii nikiwa nimeweka ushabiki wangu pembeni.
Iko hivi, yaliyotokea tarehe 8 March na kupelekea mchezo kuahirishwa ni mwendelezo wa utamaduni wa watanzania kuvumilia mambo mengi yanayoenda kinyume na taratibu. Hii ni tabia yetu ya muda mrefu ambapo kundi Fulani lenye mamlaka huwachukulia raia kama wasio na akili ya kutambua penye makosa na kuamua kwa matakwa yao. Si tu katika michezo bali ni katika mambo yote yakiwemo kwenye utumishi wa umma viongozi kupuuza matakwa ya sheria na kanuni za utumishi, yapo ktk dini, yapo katika siasa na yapo kila mahali.
Tuachane na hayo mengine turudi kwenye kiini cha andiko langu kuhusu hii derby iliyoletewa kipengele. Simba na viongozi wake wamefanya hivi kama kuwaamsha TFF na Bodi ya Ligi hata jamii kwa ujumla kutoka usingizini. Tumekuwa na tabia ya kutokuwajibishana kwa kigezo cha kutumia busara badala ya sheria au kanuni katika maamuzi mengi. Hii imefikia hatua ya kuleta double standard kwenye michezo hasa pale timu kubwa zinapokabiliana na timu ndogo. Bahati mbaya sauti za timu ndogo hupuuzwa na huwa wakionewa hazifiki popote. Tumeshuhudia mara kadhaa maamuzi ya kuwaonea timu ndogo na hakuna anayejali. Hili limevuma sana kwasababu limewagusa wengi.
Nini kinafanya haya yatokee?
Hapa nani wa kulaumiwa ni TFF/Bodi ya Ligi.
Hawa hawana namna ya kujitetea kuwa hawahusiki maana wao ndiyo waliopewa dhamana ya kusimamia hizi kanuni zao na sheria za Mpira wa miguu. Inashangaza kuona wao ndo walitengeneza kanuni alafu wanaogopa kuzitekeleza, yaani unachonga kinyago mwenyewe alafu kinakutisha. Haya mambo ya kukosa meno dhidi ya timu kubwa huwezi kuyaona kwenye vyama vya soka kama FA ya Uingereza, Hispania, Ufaransa, Ujerumani au Italia. Kuna kipindi timu maarufu Italia (Juventus) iliwahi kushushwa daraja kwa tuhuma za kupanga matokeo, Msimu uliopita Chelsea ilifungiwa kufanya usajili wa wachezaji, hali kadharika Barcelona ilifungiwa kusajili ila kwetu tunaleana tu. Jamii yoyote isiyo na utamaduni wa kuwajibishana haiwezi kuendelea katika mambo mengi.
Viashiria vya kuonesha kuwa soka letu haliko salama ni:
1. Mmiliki wa timu Moja na mdhamini Mkuu wa hiyo timu kuwa na Uhuru wa kudhamini timu zingine zaidi ya 7 katika ligi Moja. Hapa lazima utokee mgongano wa kimaslahi.
2. Viongozi wakubwa wa kisiasa kuonekana hadharani wakitoa matamko ya kutoa zawadi kwa timu Fulani ikiifunga timu nyingine. Haya yote yanaharibu ligi yetu.
3. Kuruhusu mambo ya kishirikina kufanyika ktk Mpira wetu. Utaskia sijui Mzee mpili amepewa kazi ya kumaliza wapinzani, sijui Mzee nani, n.k.
Kosa lilianzia wapi
Ukifuatilia kwa kina bila ushabiki utagundua Yanga walikosea kanuni kwa kuzuia timu mgeni kufanya mazoezi ya mwisho. Na kama Simba walitoa taarifa kwa kamishina wa mchezo akashindwa kusaidia basi lazima tatizo lingetokea.
Kuruhusu mabaunsa kuvunja taratibu. Haikubaliki hata kidogo.
Simba kukataa kuleta timu na ikasikilizwa bila kufuata kanuni napo ipo shida.
Yanga kuandika barua ya kukataa kucheza mchezo utakaotangazwa huku bodi ya ligi imeshatoa tamko la kuahirishwa kwa mechi ni utovu wa nidhamu.
Yanga iliwahi kukataa kucheza mchezo wa derby kisa muda ulisogezwa mbele.
Yote hayo yanaonesha ni jinsi Gani TFF na Bodi ya Ligi wameshindwa kuvisimamia vilabu hivi vikubwa ili vizingatie kanuni. Hali hii isipofanyiwa kazi, basi soka letu liko hatarini kuharibika maana kila mwenye cheo anaweza kuamua mechi iweje. Pia kila timu kubwa inaweza kuwagomea TFF na isifanywe Chochote.
Nini kifanyike?
Nashauri mamlaka za soka zisimamie sheria. Ukitaka kumuua nyani usimwangalie usoni, tuachane na msamiati busara tubebe msamiati kanuni. Kama timu kikanuni inatakiwa inyang'anywe points basi iwe hivyo, kama timu inatakiwa kushushwa daraja ishushwe bila kuangalia ina mashabiki wengi kiasi gani. Hayo yakifanyika Mpira wetu utakuwa wa mfano afrika nzima. Namalizia kwa kusema, huyu anayedhamini timu nyingi huku akiwa mdhamini Mkuu na mmiliki wa timu anyang'anywe haki ya multiple sponsorship abaki na timu Moja anayoimiliki.