Maoni yangu juu ya wimbo wa KADOGO wa Ali Kiba.

sangujoseph

Senior Member
Joined
Nov 30, 2015
Posts
164
Reaction score
183
By Sangu Joseph
.
Kiukweli nimepata nafasi ya kuusikiliza na kuutazama kiundani wimbo wa @officialAlikiba wa #Kadogo tuache tu utani na ushabiki wimbo ni mzuri ni moja ya nyimbo ambazo zimenivutia kwa mara moja kwa sababu umeangalia nyakati tulizokuwepo kwa sasa, unajua kwa uzoefu wangu nafahamu inapofika kipindi kama hichi cha sikukuu hasa za mwisho wa mwaka mashabiki wengi huwa tunapenda kusikia nyimbo ambazo za kucheza na kufurahia kwa sababu tuko kwenye msimu wa furaha HONGERA sana kwa hilo Kingkiba.
.
Pili nilichokipenda kwenye wimbo wako umekuwa mbunifu hasa kwenye lile neno #YEBABA mimi naamini wakati unatunga huu wimbo uliwafikiria sana mashabiki wataimbaje hasa ukizingatia umekuwa mtu ambaye una tabia yako ya kukaa mda mrefu bila kutoa wimbo, na kuwafanya mashabiki kukumiss, ukiangalia nyimbo za nyuma licha ya kuwa kali lakini ulikuwa huwafikirii wanaokushabikia ila kwa huu wimbo umefuta makosa HONGERA tena kwa hilo.
.
Ushauri wangu wa bure kwako unapokuwa unatoa nyimbo kama hizo hasa za kucheza jitahidi utuletee na style ya kucheza wimbo huwa zinapendeza zaidi na inakuwa rahisi sana kwa sisi mashabiki kutukaa midomoni kwa kutamani kucheza style ya wimbo, nikupe mfano wimbo wa #Malwedhe ni wimbo ambao ulikubalika zaidi kwa staili ya kucheza, pia achana na zile nyimbo nyingine za kinigeria, na Tanzania ambazo zilifanya vizuri zaidi kwa staili ya kucheza.
.
So naaamini ungetujia na style ya kucheza kwenye tungeipenda zaidi ngoma yako.
.
Mwisho kuna kipande cha mwanzoni kwenye video kama sijaelewa lengo lake nini ulipomwambia video vixen utampa kinywaji fulani halafu akasema anataka Mzinga, halafu ukakubali nadhani kibiashara haikukaa poa naona kama kile kinywaji cha Mtanzania mwenzetu umekionesha sio bora kuliko Mzinga japo najua haikua lengo lako lakini ungeangalia namna nyingine ili kinywaji cha mtanzania mwenzetu kisitafsiriwe vile.
.
All in all ngoma kali sana na imeendana na mazingira ya mwisho wa mwaka.
.
#kijanamzalendo #maoniyangu #ilovetz
 
Wimbo naupenda hata mimi,japo wadada waliocheza kwenye video hawajautendea haki kabisa walikuwa wauza sura zaidi.
Wimbo unachezeka kabisa ila dada warembo wala hawakuwa serious Wimbo wako hauna tofouti na Iokote wa Maua Sama wale waliweka ulimbwende pembeni wakapiga kazi,siku ukifanya remix tafuta madem watuzungushie mauno
Anyway Wimbo hakika umeukaribisha 2019 kiutamuuu,hongera
 
uko sahihi.

ila sasa ngoja waje wale ambao hawajui maana ya 'tafasri.' hii

"listen in order you understand ,dont listen in order you reply.
 
Ngoma kali kutoka kwa King kibwa
Hio ndio nyimbo ya kufungia na kufungulia mwaka
 
Uzi wako ngoja udode, alikiba hana fan base kubwa kama domo alikiba hata anye ikulu itakuwa sio habari kubwa.
 
Kitu kimoja cha kushangaza yaani mtu hawezi kumsifia mmoja bila ya kumponda mwingine.Kwani ukimsifia mmoja kuna tatizo hayo mapenzi ya kishabiki yasije kupelekea ndoa ya kishabiki.
 
ile ye baba ndo huwa nafurahi sana.
 
Kama kila mtu akiupenda wimbo flani aje kuanzisha thread humu, JF itakuwa haitoshi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…