Maoni yangu kuhusiana na Pablo Franco

Boss la DP World

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2021
Posts
2,318
Reaction score
8,464
Ndugu zangu wanasimba wenzangu kwanza niwape pole kwa kuendelea kupoteza mwelekeo kwenye ligi na kuzidi kupishana na mpinzani wetu Yanga.

Kuna mambo kadha wa kadha nataka kuyaweka sawa ambayo tumeanza kupotoshwa na baadhi ya viongozi wa club...

1. Wameanza kusikika wakisema kombe la NBCPL halina mashiko, ndugu zangu wanasimba tusiwe wajinga kiasi hiki, kombe la ligi kuu lina maana kubwa sana na hadhi kubwa, msimu huu ilipaswa tulichukue mara ya 5 mfululizo, uzembe na ubishi wa baadhi ya viongozi wetu ndiyo umetufikisha hapa tulipo sasa.

2. Ahmed Ally asiingie kichwa kichwa na kutupa matumaini hewa eti bado tuna nafasi ya kutwaa ubingwa, hizo ni ndoto za mchana na kutufanya sisi ni watoto wadogo, anapaswa kuheshimu mashabiki maana bila sisi hata kibarua chake kitaota nyasi, wakati mwingine ni bora angechagua kukaa kimya kuliko kutupa matumaini hewa, ni Ahmed Ally ndiye alituhakikishia kuwa mechi ya jana tutashinda, baadhi ya mashabiki tumejikamua, tumesafiri mpaka Mwanza matokeo yake tumepata tulicho kipata.

Baada ya mchezo wa jana anaendelea kutuaminisha tuwe na subira tutashinda tarehe 28, namimi namuuliza kwa kikosi kipi na kocha yupi? Kwanini wanatuumiza hivi au nayeye anatumwa na Yanga? Maana akisimama mbele ya camera anaongea anacheka cheka utadhani tunaongoza ligi.

3. Pablo Franco sio kocha mwenye kiwango kinachotosha kuifundisha club yetu. Hapa tulipigwa pakubwa sana.

4. Mashabiki tunaumizwa sana na mwenendo wa timu, sisi sio wa kuitwa MAKOLO na watani, hili jina linakera ni lazima tuangalie cha kufanya vinginevyo mnatuumiza, tunalipia uana chama, tunasafiri Kwa pesa, tunalala hotel za gharama, tunakula chakula kwa gharama mwisho tunapata matokeo ya kijinga kabisa.

Viongozi wa SIMBA kama mmeshindwa tuachieni timu yetu, nimenusa aibu kubwa mbele yetu, msifanye tuamue kuamini maneno ya Haji Manara.

PABLO FRANCO SIO KOCHA, TAFUTENI KOCHA MCHUKUENI HATA JULIO JAMANIIII

Aaagh.
 
Pablo ni kocha mzuri tatizo ni kuwa timu inajengwa bado na Presha ni kubwa
 
Kwani si tulikubaliana tangu awali ya kwamba kocha Pablo Martinez ni kocha bora kabisa kuwahi kutokea katika klabu yetu pendwa ya simba!

Tena wote tunafahamu fika kocha wetu huyu ameshawahi kuzifundisha timu bora kabisa za ligi kuu kule Hispania za Real Madrid na Getafe! Sasa iweje leo tumseme vibaya? Eti ana uwezo mdogo! Kweli???
 
Tulio onyesha mashaka na CV yake tulionekana wasaliti wa club, sasa anaua timu halafu viongozi wanasema hawana shida na kombe la mbuzi sasa sijui mapinduzi ni kombe la UEFA
 
Ata mie nina wasiwasi kweli huyu alitoka madrid....maana ata adebayor pamoja na ufala wake alivyoemda madrid tuliona alibadilika akawa ana shine. Sasa huyu kocha katoka madrid ata vionjo vya tactical acumen hatuoni bwana....anakera sana.

Kwanza subs zake zinachelewa sana. Mie nakubaliana nawe timu tume julio tuu...hamna maana ya kuleta kocha wakigeni alafu hatuoni mambo ya madrid ata punje
 
Simba hakuna kocha wa viungo pia
Hakuna nidhamu na benchi la ufundi
Mambo ya kulazimisha fulani acheze fulani assicheze
Wachezaji waliowapa ubingwa msimu uliopita na mkawa mnajisifu mnayo timu imara na ya ushindani afrika ukimtoa Chama na yule wa msumbiji sasa hivi mnaona hawafai lakini hamuoni ni tatizo
Mfano wachezaji hawa
P.Wawa
Tadeo lwanga
Hawa watu walikuwa ni nguzo ya timu inapohitaji matokeo wasipokuwanayo na kulinda matokeo walionayo
Kwa sasa naona kuna utani mwingi tu wa kitoto hapo wanabodi wawe makini na timu mliyopewa dhamana nayo.
 
Pamoja na Uchawi na Ushirikina wote mlio nao bado Makolo mnalialia? [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hakuna furaha wala huzuni ya kudumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…