WENYELE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 1,433
- 1,442
Wakuu mi nikiri ni moja ya waTz niliyesoma shule za jamii kabla ya shule za kata,lakini nilibahatika mpaka nilifika elimu ya juu na kuhitimu shahada ya kwanza pale SUA.
Kwa sasa niko kazini nafanya kazi na kampuni flani hapa nchini ni kampuni inahusisha wazungu,na waafrika na watu kutoka Asia.
Changamoto hapa ni Lugha tunayotumia,kwa kua kiingereza ndo business language,hapa ofisini kwetu tunatumia kiingereza kwa kazi zote.
Tunatumia kiingereza coz hata hawa wazungu nao wametoka mataifa yasiyotumia kiingereza km lugha ya taifa.Wako kutoka Hispania,Canada,Colombia,Uholanzi na USA.Wale wa kutoka Asia ni kutoka India,hapa Afrika niko mimi kutoka Tz na wengine kutoka West Africa yaani Nigeria na Senegal.
Wakuu kuna kazi ndogo ndogo zinatoka watanzania hapa wanakuja kwenye interview wanashindwa kwa sababu hawajui kiingereza,inabidi watu kutoka kenya waje kufanya hizi kazi...yaani mimi inaniuma sana kwa maana kwenye interview nakuaga nipo na huwa napewa nafasi kubwa kufanya mahojiano....cha ajabu wadogo zetu hawa kiingereza hawajui kabisa yaani inaniwia vigumu hata kumpendelea mtu,maana kujieleza tu kwa kiingereza ni shida!
Hivyo basi,mimi nashauri tubadili mfumo wetu wa elimu,kiingereza kianze kufundishwa kwa masomo yote toka shule za Msingi kama wanavyofanya Kenya,ila kwetu iwe tofauti kidogo,badala ya kuanza kufundisha masomo yote kwa kiingereza kuanzia chekechea basi tuanzie Darasa la tatu au la nne.Hii itasaidia sana watoto kuwapa uwezo wa kukabili changamoto za lugha kwenye soko la ajira.Yaani watoto wawe wanauwezo wa kujieleza kwa kiswahili na kiingereza fasaha pale wanapokua wanamaliza shule za msingi.Jamani inatia aibu kweli mataifa mengine km Spain wanaongea kiingereza vzuri kabisa ili hali wanalugha yao ya kihispania!
Nawasilisha kwa mjadala wakuu