Linguistic
JF-Expert Member
- Mar 16, 2021
- 3,669
- 8,268
Wakuu haya Maoni yangu kuhusu shughuli za uokoaji.
1. Kwa hali ilivyo sasa hivi utegemezi wa Jeshi la Zimamoto pekee hautoshi kwenye majanga yanayohusisha ndege.
Inashauriwa tuwe na mfumo wa pamoja wa uokoaji (Integrated rescue operation system) utakaokuwa na Kikosi Maalum cha Uokoaji kikihusisha wataaam kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Jeshi la Zimamoto, Jeshi la Maji, Afya kwa ajili ya matibabu ya dharula na huduma ya kwanza na sekta nyungine kadri itakavyoonrksna inafaa.
2. Vikosii hivi maalum vya uokoaji viwepo maeneo yote nchini ngazi ya mikoa hususani kwenye maeneo ya nchi yenye viwanja vya ndege vilivyo karibu na mito mikubwa, maxima na bahari.
3. Vikosi hivyo maalum viwe na wataalam sahihi na wabobezi katika uokoaji na vifaa sahihi na vya msingi katika shughuli za uokoaji kwa ajili ya nchi kavu na majini.
Timu za Uokoaji zinatakiwa kuwa zimeiva kimafunzo na kufanya drills za mara kwa mara.
Pia utaalam wa wenyeji hasa wavuvi ambao wanajua mazingira ya majini kwa kuwa ndio eneo lao la kazi kila siku na wamekuwa na msaada mkubwa kwenye uokoaji unapaswa kuangaliwa upya na kuona unavyoweza kusaidia shughuli za uokoaji.
Kiufupi tunatakiwa kufanya uwekezaji wa kutosha kwenye suala la udhibiti majanga.
4. Utayari wa Vikosi vya Uokoaji kila wakati ni jambo muhimu sana ikizingatiwa kuwa kwa asili ya majanga ya ndege muda huamua mambo mengi ili kuepuka kulipuka kwa ndege, ukosefu wa hewa ya oksijeni ndani ya ndege, maji kuingia kwenye ndege kama imetua majini, n.k.
Utayari wa vikosi unatakiwa uwe wa hali ya juu na wa kila wakati.
5. Uratibu wa majanga unapaswa kuboreshwa ili taarifa sahihi ifike kwa wahusika sahihi kwa wakati muafaka haraka kadri iwezekanavyo.
Kwenye majanga karibu yote yaliyotokea ikiwemo hili la jana kuna "time lag" kubwa kutoka janga linapotokea au inapoonekana kuna mwelekeo wa kutokea janga na wahusika kupewa taarifa ili shughuli za uokoaji kuanza.
Majanga yatatokea ni wajibu wetu kujenga mfumo imara wa kudhibiti athari zake pindi yanapotokea ili tuokoe maisha ya watu wetu kwa kadri inavyowezekana.
Tutimize wajibu wetu, inawezekana.
Kiranga Mshana Jr Retired