lee Vladimir cleef
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 9,571
- 35,475
Lissu anastahili na anafaa kupitishwa na CHADEMA kuwa mgombea wao wa Urais
Sababu kuu kabisa ni mpinzani wa dhuluma halisi tangu utoto wake, hapendi watu kuonewa Wala kuonea,anapenda Haki na ndio maana akasomea sheria ili kutetea.
Alitetea watu wengi sana waliokuwa na kesi za kuonewa au kudhurumiwa bure bila malipo kwa wasiokuwa na uwezo.
Lissu ni mpinzani asilia, alianzia CCR Mageuzi na akajiunga CHADEMA. Lissu ni mfia chama, nadhani wote ni mashahidi kwa hili
Lissu sio mhamiaji hivyo anayajua mateso ya Upinzani kuliko mpinzani yeyote Tanzania. Lissu kwa kuwa mpinzani amelipa gharama kubwa kuliko Mtanzania yeyote.
Ni Bora CHADEMA wampitishe Lissu hata kama akishindwa(kihalali) kuliko kumuachia Membe.
Tulimpisha Lowassa leo hayuko nasi katika mateso yetu.
Kuna watu walikufa,walivunjwa,walipoteana na familia zao kwa ajili ya Lowassa lakini leo karudi kwao,lakini Lissu tumeumizwa naye pamoja na tutaendelea kuwa naye pamoja.
Kwa madhira aliyoyapata kumuacha Lissu na kummpa Membe ilhali Lissu ana nia ya kugombea ni makosa makubwa sana.
Lissu anastahili kulipwa kama alivyolipwa Mandela, alikuwa jela miaka 28 kwa kazi aliyoifanya alistahili kuwa Rais wa SA.
Vivyo hivyo kwa Lissu kwa machungu aliyoyapata CHADEMA mnastahili kumpitisha mtu huyu.
Uzuri wa Lissu siyo mzigo Kama Lowassa,Lissu anajua kujieleza,anaijua sheria,anajua kujenga hoja,anayajua matatizo ya Watanzania wa Juu,Kati na wa chini kabisa.
Kupitia Uwakili wake na kesi nyingi alizofunguliwa,kuwekwa ndani amejua matatizo mengi Sana katika mifumo yetu ya kutoa Haki kuliko Mtanzania yeyote yule.
Lissu inaijua Tanzania vema,
Lissu alikuwa mwanakaharakati wa mazingira ametembea vijijini anayajua maisha halisi ya watu wa chini.
Lissu ni mwanasheria makini,amewatetea watu wengi sana na aliwahi kujitetea kesi yake ya kuvuliwa ubunge kwa uonevu akashinda kisha akatokwa machozi ya uchungu pale alipotangazwa Mshindi akiwa ndani ya mahakama huko Singida.
Lissu anajua lugha ya kiingereza kwa ufasaha mkubwa,hili kwangu sio muhimu,lakini vijana wa Kitanzania huwa wanamhusudu sana mgombea anayejua Kiingereza.
Lissu Aliwahi kuishi USA au UK Kama sikosei,hivyo anayajua maisha ya nchini na maisha ya nje. Ni rahisi kwake kujua ni nini Watanzania awafanyie kinachofanyika nje chenye manufaa na nini asiwafanyie kisicho na manufaa.
Kwa uchache Sana Ni hayo,naomba CHADEMA msifanye makosa.
Kwa Tanzania
Watanzania Kama Lissu akipitishwa na CHADEMA atatufaa sisi waumini wa Taasisi imara kuliko mtu imara.
Lissu pamoja na vyama vya Upinzani vyenye Nia njema atatengeneza Taasisi imara Kama Mahakama huru,
Polisi huru Wanaofata taratibu halali za kipolisi.
Bunge huru,
TISS huru,Majeshi huru,
TAKUKURU huru,
Tume ya Uchaguzi huru,
CAG huru.
Uhuru wa shughuli za kisiasa.
Huyu jamaa Ni muumini wa utawala wa sheria hivyo atasimamia uundwaji wa Katiba endekezwa.
Kwa hiyo tutakuwa na Tanzania mpya na njema kabisa kuliko nchi nyingi za Afrika.
Lissu ana misimamo,anajiamini na ni mkweli kwelikweli,sio muoga Wala sio katili.
Amekubali kuhatarisha maisha yake kwa ajili ya Tanzania
Nyalandu anafaa kuwa Rais lakini kwa sasa Lissu anatufaa zaidi. Nyalandu bado kijana anaweza kuja kugombea baada ya Lissu.
Hata Kikwete alisubiri miaka kumi baada ya Mkapa.
Nyalandu sio kama Lowassa, alitoka baada ya kuona uonevu aliofanyiwa Lissu,Nyalandu ni mtu mwema kabisa tofauti Lowassa na Membe.
Nyalandu awe kama Thabo Mbeki aliyepokea Urais toka kwa Mandela.
Nyalandu alikubali kuacha raha zote za kubebwa na CCM na kuja kwenye mateso.
Kwa hali halisi ni vema tukampa Lissu kwa Sasa baada yake Nyalandu anana nafasi ya kugombea u Rais.
Nyalandu amuunge mkono Lissu Ili kuweka nguvu.
Watanzania tukiletewa na CHADEMA Lissu tusifanye makosa.