Mlalamikaji daily
JF-Expert Member
- May 19, 2014
- 744
- 1,621
Haya ni maoni yangu binafsi baada ya kutafakari kwa kina, kwanza siamini kwamba suala hili la kukaa miaka 7 bila kupandishwa madaraja na miaka 6 bila nyongeza ya kila mwaka kuwa ni suala la bahati mbaya! HAPANA! Upo msemo kuwa in politics nothing happen by accident!
Sasa twende sawa hapa, kama tujuavyo kamwe! kamwe! huwezi kumtawala mtu na kumfanya afanye unavyotaka huku akiwa ameshiba! Hivyo ukitaka mtu akunyenyekee, mnyime chakula, mnyime maji, halafu mletee chakula kidogo kidogo na maji kidogo kisha muahidi utamboreshea chakula chake wakati ujao! Hakika ataendelea kukutii na kukuheshimu kwa sababu mbili:
1. Kwanza atataka kulinda chakula chake hiki kidogo anachopata ili asife
2. Ataendelea kufanya kazi akiamini kuwa ipo siku ataboreshewa chakula chake
Nasikia eti wakati wa JK wafanyakazi walikuwa jeuri sana! Ndio maana haya yanawakuta.
Kwasasa hata kunyanyua shingo wengine hawawezi na wanafanya chochote kile ambacho BOSS atasema ili kulinda vibarua vyao.
Waliokwenda kusimamia uchaguzi kule Zimbabwe waliambiwa kuwa fanya ufanyavyo MWENYEWE ASHINDE, ole wako asishinde hivyo vyeti vyako utaenda kufungia mandazi.
Wewe unadhani wangefanyaje?
Kwa njaa hii wafanyakazi wanaweza kujikuta wanafanya chochote waambiwacho ili kulinda ugali huu mdogo.