Maoni yangu kwenye katiba mpya

Maoni yangu kwenye katiba mpya

josam

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2011
Posts
2,252
Reaction score
1,041
MAONI JUU YA RASIMU YA KATIBA MPYA.

1. Kwa vile maoni yaliyokusanywa na tume ya katiba kutoka kwa wananchi yalikuwa mengi na yote yasingeweza kuingizwa kwenye rasimu, naomba kupendekeza yafuatayo.
Maoni ambayo hayakuingizwa katika rasimu na ambayo yaliyotolewa na wananchi walio wengi mfano ardhi, elimu, afya, mifuko ya hifadhi ya jamii nakadhalika, yaingizwe katika sheria zilizopo kulingana na sheria husika. Kama sheria inayohusiana na maoni hayo haipo sheria mpya zitungwekwa maleno hayo.


  1. Kwa vile neno Tanzania lilitokana na kujumlisha jina tan kutoka Tanganyika na zan kutoka Zanzibar, hatuna budi kutunza Historia kwa kubakisha Serikali ya Tanganyika kama ilivyo Serikali ya Zanzibar na ile ya Muungano. Hii itaondoa utata wa kuwa na sherehe za uhuru za Dec 9, 1961 zinazotajwa kwamba ni uhuru wa serikali ya Tanzania Bara. Hakuna nchi iliyowahi kuitwa Tanzania Bara na ambayo iliwahi kutawaliwa na wakoloni na hivyo kupata uhuru.


  1. Ukubwa wa serikali na Bunge la Muungano.
    1. Uteuzi wa Mawaziri na Naibu Mawaziri. Ibara ya 93. Idadi ya Mawaziri itakuwa 15. Idadi hii ni kubwa na kwa vile mambo ya muungano ni saba napendekeza wizara ziwe saba kiasi kwamba idadi ya mawaziri kujumlisha na naibu waziri wao wawe 14 tu.
    2. Pamoja na kwamba ni swala lisilo la muungano, idadi ya mawaziri na naibu waziri, wabunge kwa Serikali ya Tanganyika isizidi ile ya Muungano. Katiba ya tanganyika itamuke idadi ya WIZARA na MUUNDO wake. Sio kila Rais kujiundia Wizara zake. Tuwe na serikali ndogo itakayokuwa na wizara chache zisizo zidi 15 kwa kutaja tu chache mfano Wizara ya fedha, Elimu, mambo ya nje, ulinzi (Majeshi yote), ujenzi, usafirishaji, afya, Maliasili na Utalii, Nishati na madini, Kilimo na Maji, (Sayansi, Technolojia na Mawasiliano), (Wizara ya kazi, Habari na Michezo), nk. Nyingine kati ya hizo zilizotajwa zinaweza kuunganishwa.
    3. Idadi ya wabunge wa bunge la Muungano bado ni kubwa lipunguzwe.
    4. Mipaka ya Bunge. Ibara ya 108 (2). Pamoja na kushauri, ingekuwa vizuri kama bunge la muungano lingechukua hatua iwapo serikali au waziri husika hata fuata au kutekeleza ushauri uliotolewa na Bunge.
    5. Kila nchi iwe na usawa katika mapato au michango kwa serikali ya Muungano kulingana na idadi ya watu wake (Asilimia)
    6. Idadi ya wabunge wa Bunge la Muungano; Katiba itaje idadi ya wabunge kwa namba kuliko namna ilivyoelezwa katika Ibara ya 105 (2) (a), 3 na 4. Pia uanzishwaji wa mikoa mipya usiongeze idadi hiyo. Ikumbukwe kuwa katika hotuba ya ufunguzi wa rasimu ya katiba Mwenyekiti alisema idadi ya wabunge wa bunge la Muungano itakuwa 75 (Bara 50, Visiwani 20 na 5 walemavu) pia kwamba kila jimbo litakuwa na nafasi 2 za ubunge, nafasi moja me na nyingine ke.


  1. Iwapo mbunge atahukumiwa kifungo zaidi ya siku saba atakuwa amepoteza sifa ya kuwa mbunge. Hili linaonekana kama jambo geni, linahitaji ufafanuzi na reference zaidi.


  1. Katiba itamke kuwa kila chama lazima kifuate dira zilizoainishwa katika katiba. Kwamba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaongozwa na serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia na utawala wa sharia, kujitegemea na isiyokuwa na dini" Haya yafanyike kwa vitendo na jamii ione yakitendeka na kuamini hivyo. Itikadi zibaki kuwa huru kwa kila chama.


  1. Wajibu wa kutangaza mali na madeni. Ibara ya 16 (1). Kila kiongozi atanganze mali zake kabla ya kuapishwa au kuacha kazi.


  1. Uhuru wa mtu. Ibara ya 26 (2) a na b. Sheria zilizopo zibadilishwe kukidhi matakwa ya katiba hii.


  1. Haki ya mtuhumiwa. Ibara ya 38 (1), mtu apewe haki ya kudhaminiwa hata kama atakamatwa siku za mapumziko. Ilivyo sasa mtu hukamatwa siku za mapumziko kwa malengo ya kumnyima dhamana.


  1. Haki ya mtuhumiwa. Ibara ya 38 (1) (e) iwe siku zisizozidi 7.


  1. Haki za wazee. Ibara ya 47 (d). Haitoshi. Kutungwe sheria ya kutunza wazee. Kwa vile Tanzania inaendelezwa na watanzania wote, wazee wote (wakulima na wafugaji) wenye umri kuanzia miaka sabini walipwe pensheni na serikali.


  1. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Ibara ya 86. Kazi zake zitajwe katika katiba


  1. Itajwe kuwa itachukua muda gani mabunge kutunga sheria, kanuni au masharti kukidhi matakwa ya katiba hii.


  1. Naibu Spika. Ibara ya 130 (1), 131 (2). Kuna mkanganyiko.


  1. Ushirki katika vyombo vya uwakilishi. Ibara ya 180(4). Hii itachangia kesi nyingi. Ongezea ufafanuzi


  1. Ibara ya 187 (2). Sifa za msajili wa vyama vya siasa zitajwe.


  1. Ibara ya 187 (4). Watendaji wa umma kusimamia uchaguzi. Hili limelalamikiwa sana hususani Wakurugenzi wa Wilaya, Watendaji wa Vijiji na Kata nk. Kulingana na mazingira yaliyopo ya kiutendaji na mfumo wa vyama ingi, watendaji hawa hulinda masilahi ya chama kilichopo madarakani hivvyo kuminya upande pinzani. Kuwepo utaratibu wa kuhakikisha kuwa hakuna upendeleo na indapo itabainika hivyo mtumishi huyo asimamishwe kazi mara moja.

MAMBO MENGINE YANAYOSTAHILI KUWEKWA KATIKA SHERIA HUSIKA AU KUTUNGWA.

  1. MALENGO MUHIMU NA MISINGI YA MWELEKEO WA SHUGHULI ZA SERIKALI


  1. Sera ya Taifa ni Mlengo wa Kati Ujamaa, Kujitegemea. Ubeparia hautakuwa na nafasi isipokuwa shughuli za uchumi zitaendana na Utandawazi wenye mipaka.
  2. Kwamba sera kuu za nchi zitaingizwa kwenye katiba kusudi anayetaka uongozi atawambia wananchi atakavyotekeleza sera hizo.
    1. Tanzania kama Taifa lianishe vipaumbele vya taifa ambavyo vitaungwa mkono na wananchi kupitia Bunge, mfano Elimu bure kwa wote, Huduma ya afya itolewe bure kwa wote, Maji kwa wote nk.
    2. Vipengele hivyo vitakuwa vya kuanzia miaka mitano na kuendelea. Kila baada ya miaka mitano vitapitiwa upya na kupima utekelezaji wake kila mwaka. Bila kujali ni chama au kiongozi gani atakayeshinda urasi au uwaziri yeyote lazima atekeleze vipaumbele hivi.
  3. Huduma zote za jamii zisimamiwe na serikali yaani (elimu, afya, maji, umeme na usafirishaji). Viongozi wote tunaowachagua ndio wasimamizi wa huduma zote. Viongozi kwa kuwa ndio wasimamizi wa huduma hizo ni marufuku na ni mwiko kwa viongozi kwenda kupata huduma hizo kwenye taasisi binafsi au ngambo. Ni lazima wao na famila zao kupata huduma hizo kwenye taasisi za umma.
  4. Serikali iwekeze katika shughuli za madini, viwanda, kilimo, umeme na usafirishaji. Serikali iwekeze si chini ya asilimia 50.
  5. Serikali iweke taratibu za kukusanya mapato yatokanayo na rasilimali za Taifa, kama Madini, Gas, Mafuta, Ardhi, Mifugo, Misitu na rasilimali zingine zote za thamani za nchini.
  6. Hukumu kwa viongozi wabadhilifu wa mali za umma (Ufisadi)
    1. Kiongozi au mtumishi yeyote wa serikali au mashirika ya umma atakaye tumia vibaya madaraka au atakayejihushisha na vitendo vya kupokea au kutoa rushwa ajiuzulu au kupisha uchunguzi huru. Serikali ichukue hatua mara moja.
    2. Pawepo na kikomo cha uchunguzi na uendeshaji wa kesi hizo (4) (a)
    3. Ahukumiwe kifungo kisichopungua miaka kumi na isiyozidi miaka 50. Hakuna kutoa faini
    4. Afilisiwe na mali zirudishwe serikalini.
  7. Ardhi isimilikishwe kihorera kwa wageni. Wazara wamilikishwe ardhi lakini pia kwa utaratibu maalum kupuka kumilikisha ardhi kwa wasio walengwa. Kwa idhini maalum umiliki wa ardhi kwa wawekezaji unaweza kutolewa kwa muda na si zaidi ya miaka 25. Watanzania wanaongezeka lakini ardhi haiongezeki.
  8. Kama ni swala la Muungano ama la, Mwenge wa uhuru unatugharimu sana hivyo sioni tija kwa maana ya faida ya kukimbiza mwenge. Ukikokotoa gharama za kukimbiza mwenye na kulinganisha na faida zake sioni kama kuna faida bali HASARA kubwa kwa taifa. Kati ya hasara zinazopatikana kutaja kwa uchache tu ni pamoja na,

  1. Upotevu wa rasilimali watu, vitu/magari na muda. Gharama zinazotumika kuanzaia maandalizi hadi kukamilika zoezi zima nchi nzima.
  2. Serikali inakosa fedha ya kutosha hadi kuchangishana vijijini/wilayani/mkoani.
  3. Vitendo vya kukiuka maadili kwenye mikesha,
  4. Wakimbiza mwenge mkoa hadi taifa wana athirika na vumbi nk. Madhara yanaweza kuwa madogo ngazi ya wilaya.
  5. Uchafuzi wa manzingira kwenye kambi za mikesha
  6. Ajari za magari ya msafara ambazo husababisha vifo kwa watu na uharibifu wa magari na mazingira
  7. Miradi mingi hufanya kazi siku chache ama siku ya uzinduzi tu kwasababu ya ubora halifu.
  8. Rushwa na ubadhirifu katika kandarasi/miradi inayokusudiwa kufunguliwa na mwenge.

Mapendekezo mbio za mwenge zifutwe, mwenge uwekwe makumbusho kwa ajili ya historia.


  1. HAKI NA WAJIBU MUHIMU

  1. Askari wa usalama barabarani waondolewe madaraka makubwa waliyonayo ya kukamata gari, kumnyanganya dereva funguo na leseni


  1. RAIS

  1. Kinga ya rais ya kutoshitakiwa akiwa madarakani au baada ya madaraka iondolewe
  2. Kuwepo na utaratibu ambapo anapochaguliwa Rais mpya, mabalozi (ambassadors) wanaowakilisha Tanzania nje ya nchi ajira yao isitishwe. Kila rais apate fursa ya kusuka upya timu nzima ili kutimiza yale aliyoahidi kwenye kampeni. Huwezi kuwa na ambassador ambaye ni swaiba wa mshindani wako na alipewa kazi na msindani wako.
  3. Safari za Rais nje ya nchi ziwekewe ukomo ili kutotumia fedha nyingi au kutokufuja mali ya umma mfano safari zisizidi 15 kwa mwaka nje ya nchi. Hii iandane na msafara wake, kuwepo na idadi inayofahamika mfano isizidi watu 10 na daraja la usafiri lianishwe.


  1. SERIKALI
    1. Tufute Mikoa ya sasa badala yake tuwe na mikoa mipya mikubwa (majimbo) kwa malengo ya kupunguza idadi ya wabunge katika Serikali ya Muungano na Tanganyika au Zanzibar.
    2. Mawaziri wawekewe ukomo katika utumishi wao. Ukomo uwe vipindi viwili vya miaka mitano mitano vinavyofuatana.
    3. Serikali ya umoja wa kitaifa: Katika kuunda uongozi wa nchi hususani viongozi wa kuteuliwa mfano mawaziri, katibu wakuu, wakurugenzi nk.; chama kinachoshinda kiteue viongozi hao kwa asilimia ya ushindi wao na chama cha pili, nk wateue wawakilishi wao kulingana na ushindi wao.


  1. BUNGE:

  1. Mgombea ubunge lazima awe na digrii moja na diwani na diwani awe amemaliza Form IV.
  2. Spika wa Bunge na Naibu wake lazima wawe na degree ya sheria kutoka katika chuo au taasisi inayotambulika.
  3. Katibu wa Bunge lazima awe na degree ya sheria lakini pia awe na uzoefu katika mambo ya sheria.
  4. Wabunge wasichaguliwe kuwa Mawaziri, RCs, DCs nk.
  5. Mbunge asichaguliwe au kuteuliwa kushika nyadhifa nyingine katika serikali au taasisi za umma.
  6. Utaratibu wa kupitisha bajeti ya serikali au maamuzi mengine ndani ya bunge, kuwepo na utaratibu wa kupiga kura. Mfumo wa sasa wabunge wanaitikia kwa mkumbo tu "ndiyoooo". Na kura hizo ZISIWE za siri. Wananchi wawe na haki ya kujua mbunge waliyemchagua amepiga kura gani ili akirudi kwao nao waweze kumwajibisha pale inapobidi.
  7. Bunge liwe ndicho chombo kikubwa zaidi cha kutoa maamuzi na sio rais. Bunge liwe na madaraka ya kuwajibisha mtendaji yeyote wa serikali ikiwa ni pamoja na rais.
  8. Wabunge wakutane na wapiga kura wao katika majimbo yao ili kupata maoni na vipaumbele vyao vya kuwasilisha katika i vikao vya Bunge. Wabunge watoe mrejesho wa majadiliano Bungeni kwa wananchi wao majimboni.
  9. Wananchi wawe na uwezo kumuondoa madarakani mbunge wao endapo atakuwa hatekelezi ahadi zake na kuwahudumia ipasavyo
  10. Viongozi wa Bunge (Spika, Naibu spika, katibu wa Bunge, kamati nk) wasiendeshe shughuli za kwa upendeleo. Kanuni zitumike kwa usawa bila kupendelea au kukomoa upande wowote.
  11. Rais na mawaziri wote wawajibishwe na bunge na Rais asiwe na mamlaka ya kuwajibisha bunge. Utaratibu wa Rais kuvunja Bunge kama Bunge limekataa kupitisha jambo lililowakilishwa na serikali uangaliwe mpya.
  12. Kila waziri lazima ahojiwe na kamati husika ya bunge (kila mwaka) kuhusu utendaji wa kazi wizarani kwake. Na mahojiano hayo yawekwe wazi.


  1. UONGOZI BORA

  1. Huduma za kijamii Elimu, Afya, Maji viwe sawa kwa wananchi wote. Viongozi na watunga sera wote na wananchi wote kwa ujumla wapate huduma hizi hapa nchini bila ubaguzi wa aina yoyote. Kwa upande wa afya, viongozi wote watibiwe nchini. Kiongozi apelekwe nje tu pale inapodhihirishwa na Daktari. Viwango vya karo na gharama nyinginezo zinazohusu uendeshaji wa shughuli za elimu (shule/vyuo) ziangaliwe na ziwe na udhibiti.
  2. Viongozi wa serikali wote ikiwa ni pamoja na rais watofautishe shughuli binafsi, za kichama, kuabudu na utendaji wa shughuli za kiserikali.
  3. Magari kwa ajili ya viongozi wa serikali na taasisi za umma yawe ya kawaida na yasizidi cc 3000. Mashangingi yafutwe. Yatengwe kulingana na ukubwa wa injini, aina ya gari na hadhi ya kiongozi husika. Mfano madaraja matatu
    1. Rais,
    2. Mawaziri, Makatibu wakuu, Wakuu wa taasisi
    3. Maofisa wengine
Magari ya serikali yasitumike kwa shughuli binafsi hususani kwenda na kutoka baa, sherehe za kifamilia au ndugu nk.

  1. Mishahara na marupurupu vipangwe kwa usawa kwa watumishi wa kada moja na viwango hivyo visiachane kwa kiwango kikubwa. Marupurupu yatolewe tu kama ni nje ya kituo cha kazi zaidi ya km 100.
  2. Kwa sasa serikali inatenga bajeti ndogo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi karibu chini ya 30% na kutenga zaidi ya asilimia 70 kwa ajili ya matumizi ya serikali (mishahara nk). Hivyo Serikali itenge asilimia 50 kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya serikali (mishahara nk) na 50% kwa ajili ya maendeleo.
  3. Malipo kwa ajili ya viongozi wanaojiuzuru kwa kashifa, kusimamishwa au kufukuzwa yasitishwe. Siyo sahihi wananchi kuendelea kutoa kodi zao kumlipa mtu aliyefuja kodi zao. Hili likifanyika litalinda mali za umma na viongozi watafanya kazi zao kwa uadilifu mkubwa. Malipo yatolewe kwa wale wanaomaliza muda wao kwa uaminifu lakini pia viwango vya ukokotoaji wake uangaliwe upya. Si busara mtu aliyestaafu kazi kulipwa aidha karibu au sawa na mtu anayefanya kazi, hii inamaana kwamba Taifa linagharimia mtu zaidi ya mmoja kwa nafasi moja.
  4. Siku za matukio ya kitaifa kama sensa, kupiga kura, sherehe za maadhimisho mbalimbali zote zifanyike siku za kazi ili wanachi washiriki badala ya sasa ambapo zinafanyika siku za Jumapili amabapo watu wanakuwa wameenda katika ibada kukutana na Mungu wao. Kwa hiyo zifanyike siku za kazi kama Jumatatu hadi Alhamisi.
  5. Ili kuondoa tatizo la rushwa kwenye mikataba mikubwa, mikataba yote isitiwe saini bila kupitia bungeni. Vivyo hivyo kwa halmashauri ipitiwe na baraza la Madiwani. Kiwango cha chini gharama ya mradi kisichotakiwa kupitia katika hatua hizi kiainishwe bayana ili kuondoa utata.
  6. Usalama wa raia na mali zao. Hili ni jukumu la Majeshi yote ya ulinzi na usalama hususani Polisi.
    1. Polisi wapunguziwe nguvu waliyonayo tangu wanapomkamata mtuhumiwa mpaka kufikishwa mahakamani, asipigwe wala kuonewa.
    2. Kuwepo na mipaka ya vyombo vya dola kwa wabunge wa vyama vyote sawia
    3. Kuwepo na ukomo wa kufanya upelezi wa kesi ili kuepuka kutumia muda mwingi kwa malengo yasiyo na tija kwa umma.
  7. Mihimili mikuu Bunge, Mahakama na Serikali na taasisi zake kila moja itakuwa huru na haitaingilia utaratibu wa kikazi wa muhili mwingine isipokuwa tu kutoa ushauri pale inapobidi.
  8. Kiongozi awe na uhuru kwa kuhama chama chake cha siasa bila kupoteza nafasi yake ya uongozi, mfano Malawi Mutharika alijiondoa UDF ya Muluzi akaanzisha DPP, makamu wake Joyce Banda naye baadaye akajiondoa DPP akaanzisha PP.
  9. Kwa vile Makao makuu ya nchi Tanzania ni Dodoma basi rais, waziri mkuu na wizara zote wahamie Dodoma. Au kama haiwezekani basi tufute mara moja mpango wa uendelezaji wa mji wa Dodoma mambo yote yafanyike Dar es Salaam. Haiwezekani kujenga mji mkuu kwa miaka ishirini pia kuendelea kufanya ukarabati wa Ikulu ya Dar Es Salaam kila mwaka. Kuwa na miji mikuu miwili ni kuongeza gharama bila sababu yeyote ile.
  10. Sheria ya usalama wa taifa iboreshwe na ijadiliwe na wataalamu mbali mbali, wabunge. Iendane na hali ya sasa, ili TISS ifanye kazi ya usalama wa taifa. Taasisi nyingine zinazotakiwa kuamuliwa na kuangaliwa upya kimfumo ni pamoja na TAKAKURU.
  11. KULIPA kodi:
    1. Katiba itamke kwamba mtu yeyote katika jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia Rais, Bunge hadi mwananchi wa kawaida lazima alipe kodi.
    2. Malipo yoyote au posho za aina yoyote halali isipokuwa padiem lazima ikatwe kodi.
    3. Yeyote atakaye bainika kukwepa kulipa kodi ashitakiwe kwa mujibu wa sheria na kifungo kisiwe chini ya miaka kumi jela. Hakuna faini.
  12. Enzi za chama kimoja hadi sasa viwanja vya michezo, nyumba nk vinamilikiwa na Chama Cha Mapinduzi. Mali hizo zirudishwe serikalini kwani ni mali ya umma kwa vile vilijengwa au kutengwa na ama kwa ajili ya umma siyo chama.
  13. Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) lipunguzwe, ni kubwa kulingana na kazi zao, tuweke idadi ndogo na vifaa vya kisasa.
  14. Mshahara na mapato ya viongozi wa wakuu wa kitaifa yajulikane kwa walipa kodi / Watanzania
  15. Viongozi wote wa kitaifa wastaafu wanaoendelea kuhudumiwa na kodi za wananchi wasijihusishe na siasa. Hii ni pamoja na Rais, waziri mkuu wastaafu, nk. Wawe washauri kwa rais na serikali bila kujali chama anachotoka Rais.
  16. Kiinua mgongo kwa wazee. Wazee wa nchi hii walipwe kiinua mgongo wanapofikisha umri zaidi ya miaka 60. Hii iwe kwa waliokuwa watumishi na wakulima. Hii ni muhimu kwa sababu hata wakulima wanajenga uchumi wa nchi kwa hiyo kuwanyima kiinua mogongo kwa vile hawakuajiliwa siyo sahihi.
  17. Wakuu wa Majeshi ya ULINZI na USALAMA mfano CDF, IGP, Magereza, FFU nk. Wasijihusishe na SIASA za vyama hata baada ya kustaafu.
  18. Ukomo wa umri wa kuchaguliwa au kuteuliwa kushika wadhifa wowote kisiasa au serikalini
    1. Ukomo wa umri kuchaguliwa kuwa Rais, Mbunge, Waziri, Mkurungezi, Katibu Mkuu, Jaji Mkuu, Mwanasheria Mkuu, na nyazifa nyingine kisiasa au serikalini uwe ni mika 60. Mwenye umri zaidi ya mika sitini asiruhusiwe kuchaguliwa au kuteuliwa kushika wadhifa wowote katika serikali na taasisi zake.
  19. Nchi ipate muda wa kutosha (miaka 20 ijayo) kabla ya kuamua hatima ya Uraia wa nchi mbili.
  20. Mtu yeyote mwenye umri zaidi ya miaka sitini asiteuliwe au kuchaguliwa kushika nafasi yoyote ya uongozi ndani ya serikali na mashirika ya umma. Umri wa juu uliotajwa juu ya Raisi, Jaji mkuu na viongozi wengine wa Kimahakama hauathiriwi na matakwa haya.
 
Back
Top Bottom