Maoni yangu mchezo wa marudiano Simba vs Al Ahly Tripoli Libya

Tanzania Norway

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2022
Posts
321
Reaction score
640
Nikianza na vile nimewapima wale Tripoli hawatokuja kupaki basi kwetu kama tulivyofanya sisi ila tu watapunguza possession watatutega kwa mipira mirefu na through balls katikati ya mabeki wetu hasa pembeni katika hili tujiandae kisaikolojia sababu jamaa wanauwezo wa kufanya chochote kwa muda wowote na wakafanikiwa licha ya kutopata ushindi kwao.

Pili ikiwa kocha Fadlu atarudi na mpangokazi wa kutumia mawinga wetu wote Mutale na Balua basi huenda jamaa wakaja kutupa pressure kubwa mara nyingi sababu moja ya jambo linatusumbua Simba ni siku Balua na Mutale wakianza wote lazima Jean Charles au Awesu mmoja aanze benchi hasa Awesu wakati ukitazama uchezaji wetu unahitaji uwepo wake sana na uwepo wa Awesu humfanya Ahoua kuonekana mchezoni sabb Awesu ana tabia ya kupenda kuwa karibu na anaempasia hivo coach aamue kati ya Mutale na Balua mmoja aanze bench au wote waingie middle 2 Okajepha na Awesu...ili Debra Awesu na Ahoua wasifanye sana majukumu ya ulinzi muda mwingi vinginevyo atumie pure stricker 2 Mukwala na Ateba kwa wakati 1 mfumo uwe 442 acheze na viungo wa 4 .

Tatu, viongozi na benchi la ufundi wajikite kuwaandaaa wachezaji kiufundi na kisaikolojia badala ya kudili na hamasa ya washabiki kuingia uwanjani sabb pia aslimia 80 ya wachezaji wetu hizi mechi za maamuzi wengi wao hawajawahi kukutana nazo hivyo pressure inaweza kuwatoa mchezoni kabisa hasa pale tutawahiwa kufungwa goli.

NI HAYO TU.
 
Sawa ila pale hakuna timu ya kimataifa bado sana isee..
Simba maneno mengi kuliko vitendo.
 
MIMI KAMA NNAMILIKI TIMU SIWEZI KUKUAJIRI KAMA KOCHA KWANINI? KWASABABU HAUJUI MPIRA. UKIWA KOCHA KWENYE MECHI NGUMU NA YA MUHIMU KAMA HII HAUTAKIWI KUTUMIA MFUMO MPYA AMBAO HAUJAWAHI KUUTUMIA UTAFUNGWA MAPEMA MNO, UNAKUMBUKA DABO ALICHOKIFANYA DHIDI YA YANGA? KUTUMIA MABEKI WA3? MWALIMU FADLU HAJAWAHI KUTUMIA MASTRAIKA WAWILI WALA VIUNGO NAMBA 10 WAWILI WHY NOW? BALANCE YA TIMU INAPATIKANA VIPI COZ KWENYE MIDFIELD UNATAKIWA NA VIUNGO WA3 WENYE SIFA TOFAUTI KAMA UNATUMIA WINGERS KWA MAANA YA CONNECTOR,CREATOR NA DEFENDER KWA YANGA WAO HAWATUMII WINGERS NI SAWA KUTUMIA NAMBA 10 ZAIDI YA WAWILI
 
Ukocha ni taaluma na watu wanasomea na kila mara wanapiga refresher course kwahiyo Makocha wa JF please mheshimuni Fadlu David kwasababu anaijua kazi yake.Halafu mechi za knock out haziitaji mbwembwe kama hizo mnazozitaka zinahitaji matokeo tu.
 
Sisi ndiyo Simba SC AKA;

1. Makolokolo SC.
2. Mbumbumbu SC.
3. Mipang'ang'a SC.
4. Malalamiko SC.
5. Makelele SC.
6. Madunduka SC.
7. Mikia SC.
8. Mazumbukuku SC.
9. Manyaunyau (mapaka) SC.
10. Manyang'au SC.
11. Miso Misondo SC.
12. Mwakarobo SC.
13. Mazombi SC.
14. Kolokhamsa SC.
15. Kolowizards SC.
16. Kinyume nyume SC.
17. Zuwena SC.
18. Bebwabebwa (Mbeleko) SC.
19. Bahasha SC.
20. Ngada SC.
21. Miso Misonda SC.
22. Kufa Kiume SC.
 
Kutoa suluhu na AL AHLY tripol si ishara njema kabisa kwa wanasimba wote,kwa nn? kwa sababu wageni wakija home ground ya simba watakuja na mitego miwili either wapaki basi watoke suluhu tena waende ktk matuta ama watoe sare yeyote ya magoli wasonge mbele so simba ana kazi kubwa ya kufanya kwani mwenye advantege sasa ni AL AHLY TRIPOL na sio simba sc kama ambavyo wengi mnadhani.
 
Eti mpaka Steven Mukwala anapendekezwa aanze! Hakuna mshambuliaji pale. Ateba walau anaonekana ana kitu. Ila siyo huyo Mukwala.
 
Kibu.
 
Comment ya Kichoko kutoka kwa Ch...
 
uto wenye akili ni wawili tu
Na mtoa mada si miongoni mwa hao wawili.πŸ˜‚πŸ˜„πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜€πŸ˜ƒπŸ˜ƒ Kazi yao kubadili kauli walianza na mabululu ila sasahivi hausikii wakimsema mabululu.
 
Ili Simba apite anahitaji USHINDI tu.

Al Ahly wakipata sare yoyote ya magoli basi Simba OUT
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…